Hawa Jamaa ni wapuuzi sana ,watanzania wasasa sio wajinga ,watu wameelimika,yaani Temesa na waziri wanajitokeza hadharani kutetea wizi inafikirisha sana.
Mh Rais embu zuia kwanza huu wizi ,huu ni upigaji wa waziwazi ,wananchi tunachukia kwasababu mnatutoza mikodi ya kila aina ambayo haina kichwa wala miguu halafu kumbe fedha mnawapa wezi wanazibanjua tu,mnamuongezea mwananchi ugumu tu wa miasha.
Eti waziri anajitokeza na kusema eti kivuko gharama yake ya sasa ni 25B ,hes serious? Hivi meli ya mwaka 2008 iliyokuwa na thamani ya 8.5B kwasasa inauzwa 25B? Its utter non-sense ,Fukuza huyo waziri maana anatufanya waTZ wote ni Mapoyoyo.
Kipindi Range Rover zinaingia hapa TZ tena enzi hizo alikuwa nazo Nimrod Mkono zilikuwa zinauzwa 200m+ ,je kwasasa hizo range gharama yake ni 600m+?
Kipindi Murano zinashika kasi nakumbuka Mwanadada Lady JayDee alinunua kwa mil 50+ ,Je kwa soko la sasa zinauzwa 150m+? Kwa kifupi nataka kusema kwamba devices huwa inashuka thamani kutokana na muda kwasababu ladri muda unavyoenda devices za kisasa zinaundwa na kuifanya ile ya nyuma isiwe na soko hivyo inapunguza price,hii ni kwa vitu vyote hata S9 wakati zinaingia price yake ilikuwa hatari lakini sasa hadi mchunga ngombe akizichanga anamiliki s9.