KUNA UFUFUO, MWILI UMEKUFA ROHO I HAI
1Wathesalonike 4:15-17 "Hapa ni kwamba walio hai mpaka kuja kwake Kristo, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala Mauti, na ujue kuwa waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza."
Yohana 14:1-3. "Yesu alienda kuandaa makao kwa ajili ya watu waliokufa na walio hai katika Kristo"
1Wakorintho 15:51-52 "Paulo anaongelea juu ya wafu kufuliwa na kubadilishwa, pamoja na wale watakao kuwa hai, "
Matendo 24:15 "Kutakuwa na ufufuo wafu wenye haki na wasio haki"
Matendo 2:34 "Biblia inathibitisha kuwa Daudi hayuko mbinguni"
Ayubu 14:12 "Ni hivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke, hata wakati wa mbingu kutokuweko tena."
Yesu Mwenye alipokufa pale msalabani hakuenda mbinguni hadi alipofufuka na kupaa. Yohana 20:17.
Ndugu yangu mpendwa somo litaendelea na cha msingi ujue kwanza wafu wamelala, pili hawajui lolote wala hawana msaada kwetu, tatu hawana uhusiano wowote na Mungu, hivyo usitishwe na roho za wafu hiyo ni mizimu tu ukimwamini Yesu Kristo huwezi sumbuliwa na pia usijisumbue kuwaombea marehemu au kuwaomba marehemu kwa maana wao huwa mavumbi na hawajui lolote!