Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia

Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia

Huenda ikawa ni fake news ,nigerians news hakuna hii taarifa imeanzia ghana

Screenshot_20210606-101310_Gallery.jpg
 
Kaenda kulipia gharama za aliyemtumikia na kumpa umaarufu. Note: Mtumishi wa kweli wa Mungu hafi ghafla ghafla
Binadamu bhana?!!! Mnapenda sana kuhukumu. Hebu tuambie ww unaejua utaratibu wa kifo cha mtu wa Mungu kinakuwaje???
 
Alitabiri kifo cha Michael Jackson, akatabiri tena atakayekuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.
Ajabu kashindwa kujitabiria yeye mwenyewe au kumtabiria kifo jiwe.
Kwa aina ya kifo cha ghafla kilichomtokea inawezekana kachukuliwa na Lucifer na sio Mungu. Amekufaje ghafla kama sio mtumishi wa Mungu. Kafariki kama mfanyabiashara hivi maana hao ndio vifo vyao kulipia makafara yao.

Haya sio maneno yangu jamani, nilikaa huko kwenye kijiwe cha kahawa mzee fulani ndio akawa anadadavua.
Jana Jumamosi kabla ya kufa kwenye kikao cha wadau wa Emmanuel TV, T.B. Joshua alisema hivi: "Kuna wakati kwa kila jambo. Wakati wa kuja kwenye maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya huduma."

Kwahiyo T.B. Joshua alijitabiria, amerudi nyumbani kwa Mungu Baba maana hapa duniani tunapita tu, wenyeji wetu uko mbinguni.
 
Kama itakuwa ni kweli basi ni habari ya kusikitisha sana,unless kama official site yake imekuwa hacked...
 
maliza JEURI yako hapa hapa, Ukifa huna ujanja, kwanza ukifa tu, hulali tena ktk jumba lako la kifahari tunakupeleka mochwari, kisha kaburini, hapo tu jeuri huna,
kinacho takiwa ishi na binaadamu wenzako kwa wema, acha kuonea watu, usidhani utazikwa na cheo chako, wangapi tumewazika walio kuwa viongozi wajuu na ulinzi kibao!!
Hii ni kweli kabisa mkuu. Hakuna msiba umenipa somo zito kama ule wa Magufuli. Jeuri zote mwisho pumzi inapokata.
 
Mhubiri wa Kimataifa kutoka Nchini #Nigeria, Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 57

Amefariki saa chache baada ya kumaliza Huduma katika Kanisa lake Jijini Lagos

Ni mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel.
Alibakiza siku 6 kufikisha miaka 58!
 
Jana Jumamosi kabla ya kufa kwenye kikao cha wadau wa Emmanuel TV T.B. Joshua alisema hivi: "Kuna wakati kwa kila jambo. Wakati wa kuja kwenye maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya huduma."

Kwahiyo T.B. Joshua alijitabiria, amerudi nyumbani kwa Mungu Baba maana hapa duniani tunapita tu, wenyeji wetu uko mbinguni.
Kwa fikra zangu hapo alikuwa anamaanisha kuwa wakati wa kurudi nyumbani baada ya huduma ni kurudi nyumbani kwake maana hapo ni kanisani ni eneo lake la kazi. So point hiyo sijaikubali mkuu hebu tafuta ushahidj mwingine kuwa alijitabiria kifo.
 
KUNA UFUFUO, MWILI UMEKUFA ROHO I HAI
1Wathesalonike 4:15-17 "Hapa ni kwamba walio hai mpaka kuja kwake Kristo, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala Mauti, na ujue kuwa waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza."

Yohana 14:1-3. "Yesu alienda kuandaa makao kwa ajili ya watu waliokufa na walio hai katika Kristo"

1Wakorintho 15:51-52 "Paulo anaongelea juu ya wafu kufuliwa na kubadilishwa, pamoja na wale watakao kuwa hai, "
Matendo 24:15 "Kutakuwa na ufufuo wafu wenye haki na wasio haki"
Matendo 2:34 "Biblia inathibitisha kuwa Daudi hayuko mbinguni"

Ayubu 14:12 "Ni hivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke, hata wakati wa mbingu kutokuweko tena."
Yesu Mwenye alipokufa pale msalabani hakuenda mbinguni hadi alipofufuka na kupaa. Yohana 20:17.
Ndugu yangu mpendwa somo litaendelea na cha msingi ujue kwanza wafu wamelala, pili hawajui lolote wala hawana msaada kwetu, tatu hawana uhusiano wowote na Mungu, hivyo usitishwe na roho za wafu hiyo ni mizimu tu ukimwamini Yesu Kristo huwezi sumbuliwa na pia usijisumbue kuwaombea marehemu au kuwaomba marehemu kwa maana wao huwa mavumbi na hawajui lolote!
Je Musa Na Elia Wapo wapi? Vipi kuhusu Abraham?
 
Back
Top Bottom