Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Wanangu wana jamvi,
Kifo cha tapeli mkubwa mwenye roho mtakakitu TB Joshua si habari mpya tena. Hata hivyo, kina funzo hasa kwa matapeli wanaomuuza Yesu wasijue kuna mwisho. Jamaa alijirundikia ukwasi asijue atakufa kijana hata kabla ya kuufaidi.
Sijui akina Gamanywa, Gwajima, Kakobe, Mzee wa Upako, Mwingila na wengine wengi wanajifunza nini? Je wachovu na wajinga wataendelea kuwatajirisha matapeli wakijidanganya kuwa sala na si kuchapa kazi vinaweza kuwakomboa?
Je wapumbavu wanaoamini manabii wa uongo watapata somo hapa? Naomba kuleta hoja tekenyeshi wanangu.