kwetu sisi tuliooa, kwanza tendo hilo ni takatifu, na hua tunalifanya kwa utakatifu. as to how many times, ndugu, inategemeana na uwezo wako na matamanio yako, ni kitu automatic, haiwezi kupangiwa ratiba. mume ukiwa na hamu kila siku, fanya, mkeo yupo hapo na mnalala bila nguo, mke hivyo hivyo ukiwa na hamu fanya. inapokuja mmoja ana hamu na mwingine hana labda anaumwa au amechoka, linaongeleka, haiwezi kuwa lazima ati kwasababu tupo kwenye ratiba ya siku hivyo hata kama unaumwa, umechoka, kichwa hakijakaa vizuri basi utimize ratiba no, hiyo itakuwa rape sasa. things just come automatically, hata mkifanya kila siku kama mpo vizuri na mnapatana, sio shida.
1 WAKORINTHO 7:3 -5 INASEMA: 3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
WAEBRANIA 13:4 INASEMA: Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
KWA KIFUPI, sex is a very very good think, na ni tendo takatifu kama mmeoana. ila kama hamjaoana ni dhambi, na itakupeleka motoni au matatizoni tu. Mungu aliiweka ukifanya utajisikia vizuri, stress itapungua na ina afya mwilini pia. ni muhimu kufanya kadiri unavyojaliwa. na ufanyapo, jua Mungu anakuona, anaposema malazi yawe safi, anakataza uchafu wenu wa siku hizi huo, kinyume na maumbile, wapo wanawake walishakuwa wanafanya hayo kabla ya ndoa, na wakiingia kwenye ndoa wanaendeleza, hayo sio malazi safi, kama umeokoka na unafanya hivyo jua unamuudhi Mungu. Warumi 1:26 na kuendelea inaeleza jinsi wanadamu walivyobadili matumizi ya asili na kugeukia matumizi yasiyo ya asili, na inaeleza kuwa ni chukizo kwa Mungu.