Tengeneza kiinua mgongo chako Usije ukatoa laana kwa wanao

Unaweza weka hela huko miaka 10 umekufa, miaka 15 benki hiyo ikatoweka vile vile.
Sijui utalia au kucheka
 
Unaweza weka hela huko miaka 10 umekufa, miaka 15 benki hiyo ikatoweka vile vile.
Sijui utalia au kucheka
Jifunze kwanza UTT ni nini?
Halafu ukifa unaacha watoto na mke/mme pia
 
Beberu Asante kwa uzi. WABONGO WENGI HATUNA culture ya kuweka akiba. UTT ni kiinua mgongo kwa lugha nyingine. Ni katika jitihada za serikali kuwasaidia watu wajisaidie. Umasikini uzeeni ni fedheha.
UTT pia wamejitahidi sana. Unaweza fungua account online bila kubangaika na makaratsi.
Naamini kuna mifuko mingi Zaidi ya uwekezaji. This is good for everyone.
Serikali ijitahidi sana itoe elimu Zaidi. Watu wawekeze.

Ni aibu ujana wako umekula bata kitambaa cheupe, siku ikifika hata million tano huna, inabidi nzengo iweke mkeka.

By the way faida UTT inatozwa kodi?
 
Hiyo utt ni mali ya nani?
Tumezoea kutiwa moyo mwanzoni baadaye zinaanza danadana
Ni hapa ndipo ukweli ulipo, kwamba sio kwamba watanzania hawawezi kushiriki hizi vitu tatizo imani wamekwishapigwa sana matukio tena ni ndani ya miaka miwili au mitatu ya uwekezaji.

Sasa imagine hii unawekeza ili uje kufaidika miaka 20 au 30 ijayo,mtu anawaza hiyo pesa yangu itakuwa salama kweli na serikali yenyewe ndio hii ya manyang'au ya CCM?
 
Somo zuri sana hili ila duh nikiwaza serikali ni ya CCM haya majambawazi yanayopenda kuharibu maisha ya watu yanaiba kila sehemu huko NSSF, sijui Bima ya afya huku hela zitapona kweli?
 
Utajiri at least unaanza kuonekana ukianza na miaka 20+ ,
Kwa miaka 10 lazima uanze na initial capital kubwa ndio utaona pesa ya maana ila sio hizi za kuweka 50,000 kila mwezi
Kama kiasi gani cha initial capital?
 
Mtoa mada unaleta ushauri mzuri sana, japo wengine wanaona sio.

Mimi binafsi, sasa nikiwa na umri wa miaka 71, nimeuishi utaratibu huo na ninafaidika sasa uzeeni.

Nidhamu kubwa ya kuŵeka fedha kidogo kidogo kila mwezi au kila mara katika taasisi za kifedha kama utt, hatifungani, nk inakuja kukujengea uhuru wa kifedha uzeeni.
 
Hiyo mifuko inacolapse na kuletaga vilio. Jifunze kuingiza pesa kwa kile unachokijua zaidi iwe kilimo, biashara, uzoefu wa kusafiri n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…