Tenzi za rohoni

Your browser is not able to play this audio.
 
Usijihesabie kufahamu kuliko wengine ndugu na kuona wengine hawajui kuomba, kusifu na kuabudu, kumbuka akili ya Mungu haichunguziki!! Mwache mtu aombe Kwa kadri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu maana pekee ndie anaweza kutusaidia kuomba! Kwa akili zetu hatuwezi tutaishia kujiona sisi ni bora kuliko wengine. Warumi 8:26-27, omba kadri unavyoongozwa ili mradi usimkufuru Roho wa Bwana.

Sent from my itel A662L using JamiiForums mobile app
 
Acha ulokole ndugu nani kajihesabia kujua tatizo lenu hampendi kuambiwa ukweli na kuchukua hatua

hapo juu nimetoa namna bora ya kushirikiana na Roho mtakaitifu na namna ya kumwimbia MUNGU
Na nimetoa mifano ya nyimbo zinaopaswa kuimbwa ndugu huwezi kumwimbia MUNGU kama huna connection na Roho Mtakatifu hivi unaimba usinipite mwokozi na unategemea roho mtakatifu akuhudumie?
hivi hujui kwenye Ulimwengu wa Roho lazima kitu uamini upo nacho ndipo unapata udhihilisho?
Mungu anakaa ndani yako yaani BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU wapo ndani yako halafu unaimba asikupite akili zako zinakua timamu kweli?
kumbuka imani ni kuchukua hatua ya kile unachokiamini gues what
unaamini yupo mbali au Mbinguni na Maandiko yanasema yupo ndani yako unategemea
udhihilisho gani?
angalieni muimbavyo MUNGU ni MFALME na mwimbieni kwa akili!
mpendwa usiponielewa naomba Roho Mtakatifu akufunulie namna bora ya kushirikiana na ufalme wa MUNGU
SHALOM!
 
Pole kwa kuondokewa na mzee wako, mimi hizo zote zikiimbwa machozi huja bila kuitwa yaani
 
Kaa nami

Mwamba wenye imara

Salama rohoni

Bwana u sehemu yangu

Kijito cha utakaso

Hizi tenzi zinanifanya nahisi kuwa karibu zaidi na Mungu pindi ninapokosa msaada wa kibinadamu [emoji120]
 
Tenzi za rohoni,zinampa mtu utulivu na amani.
 
Kwa ufupi hizi tenzi za Rohoni zina mguso wa Roho Mtakatifu...ndiyo maana ukizisikiliza unapata mguso wa kiroho.

Kuna nyimbo ukisiliza unahisi kama umefika heaven...kumbe uko hapa hapa. Hizi ni baadhi tu ya tenzi zinazonibariki sana.

1. Mlango wazi.
Mlango uko wa wema, mlango wazi Huo.
Yesu ameufungua na hakuna kufunga.

2. Bubujiko/There is a fountain
Damu imebubujika, ni ya Imanueli.
Wakioga wenye taka, husafishwa kweli.

3. Ninaye Rafiki.
Ninaye Rafiki naye alinipenda mbele
Kwa kamba za pendo lake nimefungwa milele.
Aukaza moyo wangu niache ugeuzi
Ninakaa ndani yake, yeye kwangu milele.

4. My Jesus I love thee
5. Rock of ages cleft for me
6. Nionapo amani kama shwari/It is well(Horatio Spafford story)
7. Abide with me/kaa nami.

The list is long....simply put, every note and every toned voice be to the glory and honor of God.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…