Dj_pacha the baddest
Member
- Jun 14, 2023
- 31
- 48
Halaf ukute huna hela tena 🤣🤣🤣😆🤣Hii uimbe ukiwa umesalitiwa na mke au mme unaweza kuhisi dunia yote umebaki mwenyewe 🔥🔥🔥🔥🔥
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halaf ukute huna hela tena 🤣🤣🤣😆🤣Hii uimbe ukiwa umesalitiwa na mke au mme unaweza kuhisi dunia yote umebaki mwenyewe 🔥🔥🔥🔥🔥
hii uipate ukiwa mwenyew ndani umetulia unaweza ukahisi ndo umeingia mbinguni 🙌 🙌Tufani inapovuma sana moyoni mwanguu
Huona pa kujificha mikononi pa MUNGU
Hunificha hunifichaa adui hatonipataa[emoji4][emoji4][emoji4]
Sent using Jamii Forums mobile app
Hali ya woga na mashaka ikinijia nikiuimba najiona nko salama.hii uipate ukiwa mwenyew ndani umetulia unaweza ukahisi ndo umeingia mbinguni [emoji119] [emoji119]
ukimaliza hiyo ifuate 'kale nilitembea' 🔥 🔥 👏
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 itabidi uimbe usinipite Mwokozi namba 10Halaf ukute huna hela tena 🤣🤣🤣😆🤣
Sahihi kabisaNyimbo za tenzi, zina upako sana, alafu cha ajabu ni worldwide zipo Mataifa almost yote. Tune na ujumbe/content ni hivyo hivyo ila kila Taifa wanatumia lugha yao. Waliotunga hizi nyimbo kwa vyovyote vile hawakuwa katika hali ya kawaida walivuviwa na ROHO MTAKATIFU, hivyo ukiimba kwa imani ukazama unajiconnect na ROHO MTAKATIFU.
1. Mbele ninaendelea
Napenda sana wanaposema siku ya Bwana. Mmoja wakiimba Efatha Ministry Askofu mwingira kuna sehemu anapomalizia anasema "Je utakuwepo kwenye karamu ile ya Mwana kondoo"98 huyo ndiye anashuka🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Hizi za chini ndio zangu dahh, Hiyo nasikia kuitwa wakati nahangaika na uzinzi na ujana ilikuwa inasema nami sana Moyoni Mwangu. Uliyewaita dah, hiyo ninlazima nitoe machozi nikiisikia na huwa najitahidi sana nisiisikilize mbele za watu.Mbele ninaendelea
Bwana uliyewaita
Nasikia kuitwa
Kimsingi, kanisa linalazimishwa kufuata ulimwengu. Sisi tunapoabudu, bado tumesimama kwenye ule uimbaji wa zamani.kuna wengine wameingiza amapiano katika kuimba tenzi. Tenzi zimekuwa zikiimbwa kwa mitindo ya ajabuajabu
Weee kama Mimi. Bwana Uliyewaita. Dah, ni wimbo wangu mzuri sana. Pia kuna Ni Sikukuu siku ile pia Mteteeni Yesu. Hizo ndio nyimbo zangu nizipendazo.Bila Tenzi Namba 67 "Bwana Uliyewaita"orodha yako haujakamilika. Naipenda sana hiyo tenzi.
Mkuu kama unayo itupie hapaKuna version ya kinyakyusa ya huu wimbo ni balaa 😀🔥🔥
Una audio yake ama nikuwekee hapaKijito cha utakaso
Ni salama rohoni mwangu
Kwa SDA wao wana nyimbo za kikrustu kuna wimbo no 158 U MWENDO GANI NYUMBANI? huwa unanipa nguvu sana
Mass choir hiyo kwa mwingira hatari sanaNapenda sana wanaposema siku ya Bwana. Mmoja wakiimba Efatha Ministry Askofu mwingira kuna sehemu anapomalizia anasema "Je utakuwepo kwenye karamu ile ya Mwana kondoo"
Hii ni ya kusemehea madeni unakuta unamdai mtu mpaka unajihisi utafika mahali unaweza mkosea Mungu ,basi unakumbuka jinsi Mungu alivyokusamehe dhambi zako bila kikwazo unajikuta unabubujika na hii nyimbo alafu unamwambia mdeni wako uende kwa amani Bwana atanilipaKwa Kalvari:
Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu msalaba,
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.
Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.
Kwa neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu,
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.
Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.
Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye mfalme wa pekee sasa,
Kwa furaha nitamwimbia,
Wa Kalvari.
Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.
Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishuswa toka juu,
Alitufanyia wokovu
Kwa Kalvari.
Rehema bure na neema,
Samaha nalo nilipewa,
Ndipo aliponifungua
Kwa Kalvari.
hawa waabudishaji wa kisasa ndio wanaharibu nyimbo asilia. Tenzi zinaimbwa tune za ajabu na wachungaji wao hawawakemeiKimsingi, kanisa linalazimishwa kufuata ulimwengu. Sisi tunapoabudu, bado tumesimama kwenye ule uimbaji wa zamani.
Flat chords nyingi, umarekani mwingi 😂😂😂, wanataka kuimba kama Kirk Franklinhawa waabudishaji wa kisasa ndio wanaharibu nyimbo asilia. Tenzi zinaimbwa tune za ajabu na wachungaji wao hawawakemei