Terry Bukuku: Mume wangu rudi nyumbani turudiane nimetambua kosa langu.

Terry Bukuku: Mume wangu rudi nyumbani turudiane nimetambua kosa langu.

Baba ivone wa watu kashamove on mwenyewe ona sasa wanataka wamrudishe kwenye dharau manyanyaso
Haha, sema tusilete utani, mtu amove on, kaacha watoto watano.Huyo arudi tu, wayaendeleze, hao wote.Mke angekua mchepukaji sawa, hayo ndo makosa hayasameheki.
 
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Terry Bukuku, kupitia video inayosambaa kwenye mtandao wa TikTok, ameomba msamaha kwa aliyekuwa mume wake, Juma maarufu kama Baba Ivone, huku akieleza kuwa anatamani warudiane na kuendelea kulea watoto wao watano.

Katika ujumbe wake, Terry amekiri kuwa kiburi, dharau na makosa yake ndivyo vilivyochangia kuvunjika kwa uhusiano wao, akisema awali aliamini angeweza kuishi maisha ya pekee lakini sasa amegundua kuwa ameshindwa kuzoea maisha ya kuwa single.

Ameeleza kuwa anamkumbuka sana Baba Ivone na kumuomba amsamehe ili waweze kurudiana, akisisitiza kuwa amejifunza kutokana na makosa yake ya nyuma.

"Mimi nipo hapa mbele yenu Namuomba Msamaha Juma (Baba Ivone) Mwenye watoto Watano, Mume wangu Popote ulipo Naomba unisamehe kweli kiburi changu kimeniponza

Nilidhani Nitaweza kuishi peke yangu kumbe siwezi nimechoka kukaa Single Naomba turudiane tulee watoto ninajua Mimi ndio nimekukosea wewe nilikuwa Nina kiburi na madharau

Na ulinambia utanikumbuka na kweli Baba Ivone nakukumbuka nakuomba nimejua bila wewe siwezi kuishi nakuomba Baba Ivone kiburi kimeniponza na sasa hivi sitaondoka hata unifanyie chochote nitakung'ang'ania" Amesema

Kauli hiyo imeibua hisia na mijadala mitandaoni kuhusu nafasi ya msamaha na nafasi ya pili katika mahusiano.
Baba Ivone piga kichwani bado anapumua
 
She thought she was too good for her husband and the streets will treat her like a queen. Unfortunately, the streets treated her like a hoe.
 
Back
Top Bottom