Terry Bukuku: Mume wangu rudi nyumbani turudiane nimetambua kosa langu.

Terry Bukuku: Mume wangu rudi nyumbani turudiane nimetambua kosa langu.

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Terry Bukuku, kupitia video inayosambaa kwenye mtandao wa TikTok, ameomba msamaha kwa aliyekuwa mume wake, Juma maarufu kama Baba Ivone, huku akieleza kuwa anatamani warudiane na kuendelea kulea watoto wao watano.

Katika ujumbe wake, Terry amekiri kuwa kiburi, dharau na makosa yake ndivyo vilivyochangia kuvunjika kwa uhusiano wao, akisema awali aliamini angeweza kuishi maisha ya pekee lakini sasa amegundua kuwa ameshindwa kuzoea maisha ya kuwa single.

Ameeleza kuwa anamkumbuka sana Baba Ivone na kumuomba amsamehe ili waweze kurudiana, akisisitiza kuwa amejifunza kutokana na makosa yake ya nyuma.

"Mimi nipo hapa mbele yenu Namuomba Msamaha Juma (Baba Ivone) Mwenye watoto Watano, Mume wangu Popote ulipo Naomba unisamehe kweli kiburi changu kimeniponza

Nilidhani Nitaweza kuishi peke yangu kumbe siwezi nimechoka kukaa Single Naomba turudiane tulee watoto ninajua Mimi ndio nimekukosea wewe nilikuwa Nina kiburi na madharau

Na ulinambia utanikumbuka na kweli Baba Ivone nakukumbuka nakuomba nimejua bila wewe siwezi kuishi nakuomba Baba Ivone kiburi kimeniponza na sasa hivi sitaondoka hata unifanyie chochote nitakung'ang'ania" Amesema

Kauli hiyo imeibua hisia na mijadala mitandaoni kuhusu nafasi ya msamaha na nafasi ya pili katika mahusiano.
 
Hapo kuna lijamaa limejikataa , baba ivone akakumbukwa kama mchezaji wa akiba
Kuna kitu nilikisoma sehemu nakubaliana nacho, kinachomfanya mtu awe na mtu fulani na kutotaka kumkosa ni kwa namna gani anamfanya ajisikie akiwa nae,wala sio mikasi,au pesa pekee

Kwahiyo baba Ivone ana kitu ambacho mama Ivone amekikosa kwengine ndio maana anamtaka baby boy wake
 
Hahaha kabisa
 
Hawa ndio wale akina
Anyonyile Mwakisimi
Antombile Mwakibolo
Anfilile Mwakikundu.......?
Kama na ndio hawa!!!!? Basi hawana maana
Walinitesa sana pale mikocheni
Mwamba hata usirudi kabisa,tafuta tu njia kuwasiadia watoto wako watano,japo mie sina hata mmoja na miaka yangu nusu karne kasoro
 
Hawafai hawa,na ukiwarudia tuu ndio kifo chako.
 
Feminists wazee wa polimilai halafu wanakuacha mataa "mwanamke wa shoka, mara Super Woman"

Wakamjaza maneno ya hamasa mwanamke wa watu naye pasipo kutumia akili akahamasika kama mashahidi wa Jamuhuri.

Mwishoni ameingia field kuyakabili maisha yaliyo rahisishwa kupitia midomo ya wajuaji.

Finally amekuja kugundua kuwa hamasa za mdomoni hazifanyi kazi eneo la field (real life)
 
Back
Top Bottom