Teruso, yaani aliyeokoka kuuawa kwa upanga wa miungu

Teruso, yaani aliyeokoka kuuawa kwa upanga wa miungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
TERUSO YAANI ALIYEOKOKA KUUAWA KWA UPANGA WA MIUNGU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuhani Katika Hekalu Jeusi.

Tena siku zile nikasema acha nifuate njia zangu mwenyewe. Nimechoka kuwa chini ya MUNGU. Nitatumia nguvu zangu mwenyewe. Akili zangu mwenyewe. Wala sitaki Tena kuongozwa na huyo Mungu. Wala sikujua nini nifanya lakini nilitaka kuwa Huru, kuishi vile nionavyo, nipendavyo na kufanya Yale yote yatakayo nifurahisha.

Tena siku zile nikamwambia huyo MUNGU kuwa ewe Mungu, ikiwa wewe ni Mwema, ikiwa wewe ni mwenye nguvu, ikiwa wewe ndiye muweza, Mwenye nafasi na mwenye kutoa nafasi. Niache Sasa niwe pekee yangu, Tena niishi pekee yangu. Nifikiri pekeangu, na niseme Yale yote yaliyomo akilini niyatakayo kuyasema.

Tena nikamwambia ikiwa wewe ndiye MUNGU wa miungu, hiyo ambayo ulisema isiabudiwe na watu na jamii za watu, isiabudiwe na viumbe na jamii za viumbe. Nakuomba Sasa kwa Wema wako,kwa nguvu zako, na uwezo wako unifanye niwe Huru, niwe pekeangu, Tena nisikutegemee kwa chochote.

Basi ndipo Huyo MUNGU akanambia katika fikra zangu, akisema, nitakupa Uhuru. Nawe utafanya kama nafsi yako itakavyo.

Basi nikaondoka zangu, kwa sababu nilikuwa nimeenda kukutana na yule MUNGU wangu kule Milimani nilipokuwa nakutana naye mara mbili kwa Mwaka. Sasa sikutaka nimuache kwa kumtoroka, kwa sababu licha ya kuwa alikuwa MUNGU kwangu lakini pia alikuwa Rafiki yangu Mkubwa.

Nami nikashuka kwenye ule Mlima. Nikiwa nalia. Midomo ikiwa inatetemeka. Uchungu wa kuagana na rafiki yangu kipenzi tangu utotoni mpaka nafikisha miaka ishirini na mbili. Sasa tumetengana, Sasa tumeachana.
Machozi ya Kwa kheri kwa Mungu wangu.

Nikachukua njia yangu. Nikaenda zangu katika mawazo yangu na Yale yote niliyoona yanafaa. Nikajifurahisha. Wala sikutaka kugeuka nyuma kuutazama uso wa MUNGU, wala sikutazama juu kuuona uso wa rafiki yangu. Nikaenda zangu.

Sasa nikawa katikati ya watu nikipita. Nikawa nikisema mbele za watu. Nao walikuwa wakinisikiliza kama mtu lakini hawakujua mtu aliyemkimbia Mungu wake, rafiki yake wa miaka mingi.

Nikasema, nitajitafutia marafiki wengine. Ambao nitajifurahisha nao katika Yale yote yatakayotupendeza.
Tena nikasema, nitatafuta Baba mwingine kwani Baba yangu alikuwa MUNGU. Huyo Baba mwingine ambaye nitamwona, nitamsikiliza na kumkimbilia.

Nikajiharibia njia yangu mwenyewe. Nikaichafua nafsi yangu mwenyewe kwa kufuata njia zisizo HAKI. Tena nikajiingiza katika ulaghai na uongo.

Yule MUNGU, ndiye Rafiki yangu alikuwa akinitembelea mara kwa mara akinisihi nimrudie.
Nikamkemea na kumwambia aniache.

Tena zaidi nikamwambia, Mimi Keterusa, ndiye Robert nafurahia maisha ya uhuru, kujiongoza mwenyewe, Tena nikamwambia kama Bado ningekuwa rafiki yake ningemwomba jambo. Lakini kwa vile yeye sio rafiki yangu na wala Mimi sio rafiki yangu. Yeye sio Mungu wangu na wala Mimi sio mtu wake. Siwezi kumwomba jambo lolote lile.

Huku nikijua anajua nataka kumwomba jambo gani. Akaniambia, unataka kuwa kiongozi wa miungu, utende uyapendayo kwa miungu, nayo ikusikilize wewe, na Kila utakachosema ifanye.

Nikamwambia ningetaka jambo hilo lakini siwezi kulitaka kwako Tena kwa sababu Mimi na wewe hatuna uhusiano Tena.

Basi miaka miwili ikapita, mambo yangu yakiwa yameharibika sana. Roho yangu ikiwa imeshuka kutoka juu nayo taa yake ikawa imefifia. Nafsi yangu ikawa inapapaara, ikawa pweke yenye upweke Mkuu.
Kumbe wale marafiki niliowachagua hawakuwa marafiki bali maadui. Walanigeukia.
Tena yule Baba niliyemfanya Baba kumbe hakuwa Baba kwani alitaka kuiteka roho yangu milele.

Mwaka wa tatu ikazuka Vita baina yangu na wale niliowachagua, nikapigana kufa na kupona. Uwezo mdogo ambao MUNGU alinipa ambao hakuuchukua ulinifanya nijione naiweza vita Ile.
Ulinisaidia lakini wale adui walikuwa wengi na walikuwa na mbinu maelfu.

Kumbe nyakati tulipokuwa marafiki na mmoja akiwa Baba niliyemchagua, Moja ya marafiki alikuwa akifanya hila mbaya sana ya kuziharibu akiba za nguvu zangu.
Mimi sikuwa najua kwa sababu nilijua ni marafiki tuu, niliwaamini. Na kwa vile sikuwatilia shaka ikawapa nafasi ya kuniharibu Polepole pasipo Mimi Mwenyewe Kujua.

Tena nakumbuka katika mwaka wa kwanza nilipomuacha Mungu, ndiye yule Rafiki yangu. Huo mwaka wa kwanza akaja Mungu, akiwa amebeba zawadi. Nikamuuliza hiyo ni nini akaniambia, hii ni zawadi nimekubebea Rafiki yangu.
Akanisihi niipokee Kisha hatakuja Tena Kunisumbua.

Basi hasira zikashuka baada ya kusikia kuwa kama nitaipokea zawadi Ile hatanisumbua Tena. Nikaipokea na kuifungua, natazama alikuwa ni mwanamke. Nikamwambia huyu ni nani? Akaniambia huyo ni rafiki bandia niliyekupa Mimi. Pengine itakuwa zawadi yangu ya mwisho kama utabaki na msimamo wako.

Nikamwambia nimfanyie nini huyu Mwanamke. Akaniambia subiri nitakuambia nini chakufanya Kisha akaondoka. Nikabaki na yule mwanamke tukiwa tunatazamana.

Nikamuuliza yule mwanamke unaitwa nani?
Akasema jina lake ni Miya. Kisha nami nikamwambia naitwa Keterusa. Ndipo nikamchukua Miya, ndiye huyo mwanamke niliyeletewa na MUNGU.
Tukaondoka na kurudi nyumbani.

Rafiki zangu wakaja, wakamkuta yule mwanamke, wakaniuliza huyu ni nani. Nikawaambia jina lake anaitwa MIYA. Wakatazamana.
Kisha wakaniambia, mbona yupo hapa!
Nikawaambia huyu yupo hapa kwa sababu pia ni rafiki yangu. Lakini kumbe wao hawakufurahia uwepo wa MIYA katika maisha yangu.

Baba naye akaniambia bila shaka Miya ni Mke wangu. Nikataka kukataa lakini Miya mwenyewe akajibu akasema, Baba Mimi ni kivuli cha roho ya Keterusa, taswira ya nafsi yake.

Basi alipojibu hivyo, Baba akasema basi sawa, tutaenda kwa miungu ili tufanyiwe tambiko na ibada ya miungu ili safari yetu iwe ya baraka na amani.
Mimi sikukataa, lakini MIYA akauliza lini tambiko hiyo itafanyika.
Baba akasema, kesho kwenye mwandamo wa mwezi. Kisha baada ya siku Saba baada ya mwezi kuandama, tutafanya kafara ndogo, Kisha tutamaliza na kafara kubwa siku ya kumi na nne mwezi ukishakuwa duara.

Lakini MIYA akapinga, akasema Bado ni haraka sana. Yeye hajaongea na wazazi wake. Mpaka aongee na wazazi wake ili ikiwezekana siku hiyo wawepo. Kwa sababu haitakuwa vizuri kwake kufanyiwa jambo hilo bila wazazi wake nao kuwepo.
Wazo hilo nikaliafiki lakini Baba pamoja na rafiki zangu wakaonyesha kulipinga lakini hawakuwa na jinsi. Hivyo tukapanga tambiko litafanyika siku ishirini na tisa kutokea kesho mwezi utakapoandama. Ili MIYA akawape wazazi wake taarifa wapate muda wa kujiandaa.

Wakaondoka Baba na rafiki zangu nikabaki na MIYA.
Kumbe MIYA Ile ilikuwa njama ya kukataa tusiende kwenye ibada za miungu. Tena jina la mungu yule alikuwa akiitwa ASHEZI mungu Mme, na LASHEZI alikuwa mungu Mke.

Basi MIYA akachukua Mimba hata kabla ya zile siku ishirini na tisa kuisha. Jambo lile likamkasirisha sana Baba na Rafiki zangu. Zaidi likamkasirisha ASHEZI. Mimba ikasukwa sukwa mpaka Ikatoka, ndiye ASHEZI aliyeitoa mimba ya MIYA.

Jambo lile likaniuma Sana kwani nilimuona MIYA akiwa hana furaha tangu mimba yake itolewe na ASHEZI. Amani na furaha ya pale nyumbani ikapotea. Kwa taratibu za Miungu ya ASHEZI na LASHEZI mwanamke mimba ikiharibika hatakiwi kufika kwenye madhabahu kwa kipindi cha miezi mitatu ya miandamo ya mwezi.

Basi Ile tambiko ikawa imehairishwa. Lakini Baba na Rafiki zangu pamoja na mungu ASHEZI na LASHEZI walijua Ile ilikuwa njama ya MIYA. Wakamkasirikia. Na walikuwa wakimsumbua sana lakini kwa vile Mimi nilikuwa na nguvu nilikuwa nawazuia wasimfanyie hiyana na ubaya uliopitiliza.

Ilipotimu miezi mitatu ili tarehe ya kupangwa kwa tambiko iwekwe kumbe MIYA alikuwa amebeba mimba nyingine.

Jambo hili liliwakasirisha sana. ASHEZI na LASHEZI walidhamiria wakati huu wamuue MIYA lakini kwa Siri bila kumhusisha Baba wala Rafiki zangu.

Huo ulikuwa mwaka wa tano tangu nimuache Mungu.

Katika siku hizo, Mungu akanijia katika ndoto mawazoni, akaniita, mara mbili, Keterusa. Nikaamka, nikamwambia mbona unanisumbua, na mbona haushiki ahadi na kiapo chako. Uliniambia zawadi Ile uliyonipa ambayo ni mwanamke aliyeitwa MIYA, kuwa ndio hatutaonana Tena.

Akanijibu, hakuja kwaajili yangu Bali kwaajili ya MIYA. Tazama Wanataka kumuua MIYA na mtoto aliyepo tumboni.
Hapo nikashtuka. Nikasema nani hao wanataka kumuua MIYA kipenzi changu, kwani tayari moyo wangu ulikuwa umeshazama kwaajili yake.

Akaniambia huyo Baba, na hao rafiki zako na hiyo miungu uliyoichagua ndiyo inataka Kumuua MIYA na Mtoto wako aliyetumboni.

Wakati huo mimba ilikuwa na miezi miwili hivi. Ndipo vita vikaanza baina yangu na Baba, rafiki zangu, na ASHEZI na LASHEZI Ile miungu ya kigeni.

Lakini kumbe walikuwa washanidhibiti vilivyo, kwani nguvu zote hasa zile za Akiba nilizokuwa nazitegemea na kudhani ninazo walikuwa washaziharibu.
Ndipo Sasa wakaniteka, nikaifunga roho yangu, Kisha wakachukua kitambaa wakafunga macho nafsi yangu isione. Hata yaliyokuwa yanaendelea sikuyaona.

Wakachukua mnyororo wa shaba na kuufunga Ulimi wangu usiweze kusema chochote. Huku wakinitishia kuukata.

Hofu ikanivaa, kushindwa kukawa mbele yangu. Naogopa kumuita MUNGU wangu,
MIYA akawa anataabika na kuteswa huku wakitaka kuiharibu Ile mimba Tena na kutaka kumuua kwa kumpa magonjwa.

Siku Moja MIYA akaja kwangu nikiwa nimefungwa roho yangu, nikiwa nimefungwa kitambaa kwenye macho yangu nisione, nikiwa nimefungwa na mnyororo wa shaba kwenye Ulimi nisiweze kusema neno lolote hasa kumhusu MUNGU.

MIYA akaniambia, hali hii itaendelea mpaka lini. Unataka nipoteze na huyu Tena.
Mimi sikuweza kumjibu kwa sababu Ulimi wangu ulikuwa umezuiwa usiseme.

Akaendelea kusema, Nataka mwanangu aishi.
Ndipo nikampa ishara aniletee karatasi na kalamu. Naye akafanya hivyo.

Nikaandika, Mimi nimegombana na MUNGU, yule Rafiki yangu kwa miaka ishirini na mbili, huu mwaka wa tano Sasa unaenda wa sita.
Hatanisikiliza hata nikimuita.
Tafadhali muite wewe kwa niaba yako na mtoto wetu Mwenyewe.

Mwambie Mimi ndiye nilivunja urafiki wetu lakini sio wewe na Mtoto.

Basi MIYA akaondoka.
Usiku ikawa vita kubwa sana nikiwa nimelala natazama nikaona nipo katika vita ya mapambano nikipambana na ASHEZI akiitaka roho ya mtoto, roho ya mtoto ikinililia na kuomba msaada kutoka kwangu.

Nikapigana sana nikawa nakaribia kushindwa natazama LASHEZI yule mungu Mke akawa amepanda farasi wa kijivu akiwa ameshika Panga lenye kung'aa makali huku na huku. Akimfuata kwa kasi mtoto ambaye alikuwa anakimbia huku analia, Mimi nikiendelea kupigana na ASHEZI.
Nikamwona LASHEZI akiwa amemkaribia mtoto Kisha akaunyoosha upanga wake na kumpiga mtoto lakini yule mtoto akaficha uso wake na Mkono wake wa kushoto, lile panga kabla halija fika katika uso wa mtoto ukatokea Mwanga mkali ukawaka kwa nguvu nyingi ule upanga ukampunyua mtoto kidogo kwenye shavu lake la kushoto n Mkono wake wa kushoto.

Nikazinduka, ilikuwa ni ndoto.
Lakini Ulimi ulikuwa umefunguliwa lakini roho na nafsi zilikuwa Bado.
Siku za mtoto kuzaliwa zikatimia, akazaliwa mtoto wa kiume akaitwa Teruso yaani aliyeokoka kuuawa kwa upanga wa miungu.

Ngoja nipumzike Sasa. Hii ya leo ni kama ndoto isichukuliwe serious

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom