Sitashangaa hili likitokea kwani Yanga wapo "serious" sana kwani wanajua biashara yote ya mpira kuanzia jezi, viingilio, wadhamini, n.k. ni kwanza lazima timu ifanye vizuri uwanjani na si vinginevyo. Kama timu haifanyi vizuri uwanjani usitegemee kuingiza mapato ya kutosha. Nilitegemea baada ya Simba kuona dili la Manzoki gumu basi wangetafuta mshambuliaji mwingine mwenye uwezo kati ya walio wengi waliotapakaa Afrika lakini walichofanya wanajua wenyewe.
Lakini yote kwa yote Simba toka Babra awe na nguvu pale Simba amekuwa mgumu wa kutoa pesa ya kutosha kusajili wachezaji wa maana matokeo yake sasa hivi Simba ni kama tu Arsenal ya mzee Wenger. Inatongoza wachezaji wazuri halafu wanaishia kusajiliwa na timu nyingine rejea mfano wa Adebayor, Aziz Ki, Sylla na hili la Manzoki kama litakuwa kweli basi litakuwa balaa kubwa na Msimbazi hapatatosha.