Tetesi: Rwanda yanunua madini kwa siri nchini Tanzania na kuyauza tena kwa kampuni ya Apple

Tetesi: Rwanda yanunua madini kwa siri nchini Tanzania na kuyauza tena kwa kampuni ya Apple

Mwenyewe niliuza chuma kutoka karagwe na tulikua tunauzia remera kigali, shinyanga na geita na kigoma hadi mpanda na sumbawanga wanyarwanda humiliki ardhi kubwa ya kilimo tena walinunua kihalali japo wako rwanda na kila mavuno wao hua na uhakika wa chakula na kuuza congo ya mashariki, mbona niliwahi kuandika hapa majuha yakapotezea note: mtutsi anayeishi tanzania ana haki na uraia wa rwanda pia na kwao hupiga kura kama mnyarwanda nashangaa serikali inapinga uraia pacha wakati watusi wana uraia wa tanzania na rwanda ukiwacheck viongozi wa bongo unaona hawa mazezeta kweli, maana mtu yuko runzewe, katoro, geita, ushirombo, kahama, mwanza, ngara, kakonko, kasulu, kibondo na ana uraia wa rwanda safi kabisa wao huku hua nawachek kama uhamiaji nawaona mazezeta tu
Jukumu la usalama ni letu sote toa hizo Intel info watu wafanye kazi
 
Hakuna tatizo isipokuwa tumezidiwa ujanja tu na Rwanda yeye katafuta soko la uhakika kutoka kwa apple
 
Jukumu la usalama ni letu sote toa hizo Intel info watu wafanye kazi
Kama hawayajui hayo na wanalipwahawafai kufanya hiyo kazi, baada ya kutoa intro waingie kazini waujue ukweli sio wakae ofisini
 
Wewe utakua mnyarwanda labda. Kinachodaiwa hapa madini yanatoka nje ya nchi kwa magendo. Kama wanunuzi wa Rwanda wanakuja kihalali kwenye masoko yetu kununua madini hakuna shida. Tatizo madini yanatoka kimagendo kama mpango wa serikali ya Rwanda. Tanzania serikali haipati ushuru wowote wala hela ya kigeni zozote. Kisha rwanda inauza madini hayo kama yametoka nchini kwao na kupata hela za kigeni wao. Hii ni sawa na wanavyofanya kwa congo. Tena kule kivu wanamiliki migodi kibabe kwa kuweka jeshi lao wakijidai kuna uasi wa M23 kisha wanapeleka rwanda madini kwa ndege ndogo zinazotua maeneo wanayamiliki kijeshi na kupeleka madini rwanda kisha kuyauza nje kama yametoka rwanda.
Ni uhuni na upuuzi wa kiwango cha juu, ni dharau kwa mataifa jirani.
 
Naona umeamua ama kupotosha au kuandika masuala ambayo huyafahamu uzuri kwa undani.

Habari za kijasusi zilizopo ni kwamba Apple wanunua madini yale ya T3s ambayo (kwa kufahamu au kutokufahamu) huibwa na kutoroshwa kutokea Kivu huko Goma na kuishia Kigali.

Na moja ya sababu kubwa ya Tshisekedi kuwa Paris wakati huu ni kujadili hilo maana M23 ndo wasadikiwa kuwa mkono wa kulia wa Rwanda.
Unafahamu uharamia wa makampuni ya kibepari? Wananunua madini mengine wasiohitaji na kuuza kwa washirika wao.
 
Back
Top Bottom