Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Naona umeamua ama kupotosha au kuandika masuala ambayo huyafahamu uzuri kwa undani.Kuna tetesi madini yamekuwa yakinunuliwa kwa kasi ktk mikoa ya Geita na Shinyanga na wafanyabiashara wasio wazalendo.
Wafanyabiashara hao hupewa mitaji na serikali ya Rwanda japo wao ni watanzania.
Wanachofanya ni kununua almasi na dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na kuiuza nchini Rwanda kimagendo kwa siri kubwa sana. Jengo la ununuzi lipo jijini Kigali na Rushwa hutumika pakubwa kuwazima mamlaka za mipakani.
Inadaiwa wafanyabiashara hawa hufanya biashara nyingine halali kati ya kanda ya ziwa na Rwanda huku lengo fiche ikiwa ni madini ya Tanzania.
Haikubainika ikiwa kampuni ya APPLE ambayo huyanunua madini hayo kutoka serikali ya Rwanda kama inayo habari kuwa madini hayo hutoka nchini Tanzania.
Source: Wachimbaji wadogo Geita na Shinyanga.
Habari za kijasusi zilizopo ni kwamba Apple wanunua madini yale ya T3s ambayo (kwa kufahamu au kutokufahamu) huibwa na kutoroshwa kutokea Kivu huko Goma na kuishia Kigali.
Na moja ya sababu kubwa ya Tshisekedi kuwa Paris wakati huu ni kujadili hilo maana M23 ndo wasadikiwa kuwa mkono wa kulia wa Rwanda.