Tetesi za Fabrice Ngoma kutekwa na Simba

Tetesi za Fabrice Ngoma kutekwa na Simba

1688481921335.png
 
Simba wamepata NGOMA.

YANGA watamtambukisha mchezaji wao saa nane usiku.

PUNGUZA kujaza Seva JF
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi UTO ni mazuzu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aliyewaita mashabiki wa simba ni mbumbumbu, aliwaza mbali sana.
 
Aliyewaita mashabiki wa simba ni mbumbumbu, aliwaza mbali sana. Yaani kwa namna wanavyosimulia hilo tukio, unaweza ukafikiri labda huyo Fabrice Ngoma atacheza peke yake uwanjani!
Na aliyewaita Uto Nyani aliwaza karibu? Kwanza mmemlipa hela zake? Kutukana amewatukana na hela mtampa, mtake msitake! Na dogo namba 6 iliyomuwa inasubiriwa kwa hamu ishachukuliwa na wajanja!
 
Kugombea wachezaji mambo ya kizamani ,kama mna maskauti wazuri mnaweza kupata wachezaji wa bei rahisi, wakaja kuwafanyia kazi ya bei kubwa, kama ilivyokuwa kwa Kante/ Marhez/ Vady na Leicester. Basi tu sometimes tunakiwa excited na hawa wachezaji ila uwanjani unaweza ukakuta hamna kitu.
 
Zama zakudandia mchezaji amabye hukuwa na mipango naye nao ni ushamba wa soka la Tz, sindio anakuja anakaa benchi mnaanza kumtukana kocha?, Sidhani Kama huu upuuzi bado upo kwenye mpira wa kisasa ambao unaendana sayansi
 
Duh kwel Simba noma ndege ikiwa angani mazungumzo yakafanyikia humo humo, agent alikua humo humo terms za mkataba zikaweka humo humo!




Kupata vichekesho kama hv bonyeza *666#
Wiki iliyopita walisema Yanga kazuiwa kusajili, huyo waliompora alitakiwa kusajiliwa na Yanga ipi?
 
Juzi si mlituambia Yanga kafungiwa kusajili? Tukaonyeshwa mpaka na TMS ikionyesha hivo sasa inakuaje Leo mnanyang'anyana mchezaji na timu ilofungiwa kusajili😂

Yaani mda mwingine mpaka najiuliza kushabikia mpira TZ lazima uwe chizi
 
Msemaji wa Yanga SC Ali Kamwe utaweka wapi Sura yako kwani huyu Mchezaji ulimtambia mno kwamba ndiyo atavaa Jezi #6 ya Yanga SC na hatimaye ameshasinya na Simba SC.

Unaambiwa wakati Watu wa Yanga SC wakimuwahi kumpokea JNIA Terminal III Leo Saa 11 Alfajiri kumbe Wenzao ( Watu ) wa Simba SC Kimafia walimtuma Mtu huko huko alikotoka na akasafiri nae kwa Ndege na Kukaa nae Siti Moja na Kumtolea Mkataba na 'Kuusinyia' huko huko Angani na Kumaliza na Ndege ilipotua tu Mipuuzi ya Jangwani wakiwemo Marafiki zangu Bhinda na Motisha wakijiandaa Kumpokea na Kumbebea Mabegi wakamkosa kwani Yule Mafia wa Simba SC alimpitishia Mlango mwingine kisha akakuta Gari limeshaandaliwa na 'Faster' likaondoka na sasa Mchezaji huyo anayetokea nchi yenye Machafuko kutokana na Marafiki Wakubwa Kusalitiana yuko Kajipumzisha katika Hoteli Moja Kubwa Jijini Dar es Salaam yenye Sifa ya Kubadili Jina lake kila baada ya miaka Mitano au Saba au Kumi.

Kisasi cha Mbuyi Twite kimeshalipwa.

Kudadadeki....!!
Namalizia KISA CHA MBUYU TWITE KIMELIPWA
 
Back
Top Bottom