Tetesi za Matokeo ya NECTA kidato cha nne 2012 [Kabla Hayajatoka]

Status
Not open for further replies.
BARAZA LA MITIHANI LAIKANA PAGE YA FACEBOOK INAYOTUMIA JINA LAKE
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi alisema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.

Uvumi huu umetokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti ya facebook yenye jina la Baraza na kuanza kuweka taarifa hizo zisizo sahihi. Napenda kuwajulisha wananchi kuwa Baraza letu halina mtandao kama huo hivyo taarifa hizo si sahihi.

Nchimbi alibainisha kuwa matokeo hayo si siri hivyo yakiwa tayari Katibu Mtendaji atayatangaza kupitia vyombo vya habari na baadaye yataanza kusambazwa kwa kutumia mtandao.

Aliwataka wananchi kuwa makini ili wasitapeliwe na wanaojifanya kuwa wanaweza kupata matokeo ya mwanafunzi kabla hayajatangazwa rasmi kwa vile suala hilo haliwezekani.
 
mi nsha zila haya matokeo jamani...! mana tunapewa matumaini kama wagonjwa wa ukimwi
kama vpi nasubiri ya 2013:glasses-nerdy:
 
Mwaka huu sijui st.Francis au Marian? Wadada wakiwezeshwa wanaweza
 
Habari wana JF,

kwa tetesi nilizopata matokeo yatakuwa displayed tar 08/02.

UPDATE:
Jan 08, 2013

By Manase Anthony.
Tetesi zako zimetokota,nikushauli tu,pamoja na uanazuoni wako uwezo wa kufikiri ulionao nimdogo unapaswa kupima uzito watetesi zako kwanza.unapotosha?
 
Aya sasa yako wapi?tetesi tu!mnafanya kua taarifa kamili kweli?nauliza yako wapi matokeo?acheni hizo kuweni na busara jamani!!.
 
Aksante sana kaka maana watu wananisumbua kwa sababu kati ya niliomaliza nao ni mimi tu ambaye nna cpt ,so raia wanipa mzigo ooo yametoka facebook! Thanks bro
 
Habari wana JF,

kwa tetesi nilizopata matokeo yatakuwa displayed tar 08/02.

UPDATE:
Jan 08, 2013

By Manase Anthony.
Tetesi zako zimetokota,nikushauli tu,pamoja na uanazuoni wako uwezo wa kufikiri ulionao nimdogo unapaswa kupima uzito watetesi zako kwanza.unapotosha?
 
Mods, Watu kama hawa wana tarnish image na reputation ya Jamii Forums. Siku zote JF imekuwa chanzo cha habari cha kuaminika. Kuruhusu watu kama hawa waendelee kuuhadaa umma wa wana JF utaishushia hadhi JF na kuonekana kama kijiwe kisicho na mwenyewe! Hili halikubaliki...Mtu anakaa chini na kutunga uwongo mkubwa namna hii halafu anaachwa tu? Tena kwenye Jukwaa la Elimu?

Wakuu Invisible, Paw na Mods wengineo tafadhali wote walioleta utapeli huu na kuleta usumbufu kwa mamilioni ya wazazi, watahiniwa, walezi na wadau wengine wa elimu wapigwe ban ya kueleweka!

Naomba kutoa hoja.
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
 
jaman hayo matokeo ni kwamba kuna pages zimepotea ndo wanatafuta au kuna tatizo gani kwa sababu yamesha tuchosha kusubiri kama yamemalizika mapema kusahihishwa kwann wasi yatoe sasa tanzania kila kitu rough,,,
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…