Tetesi za Siri ya vita ya Rwanda na Congo DRC na kwanini sasa sio jana?

Tetesi za Siri ya vita ya Rwanda na Congo DRC na kwanini sasa sio jana?

Asante kwa wake up call,
ngoja tufaye fumigation kuua mchwa
 
Kagame hana interest na TZ, Wala hataki kuchukua DRC yote, Ni kivu na Goma tu, Ila hasa Kivu, Kama akipewa hilo eneo hutasikia vurugu tena, Ila akitulia anaweza kuihitaji Karagwe,

Sioni uwezekano wa M23 kuachia mji wa Goma, jumuia za kimataifa zipo kimya, SADC NA EAC zinapigwa ovyo ovyo, TZ yamebakia maneno ya kanga, taabu imetukuta waafrica
 
Warwanda akili kubwa.
Wapo kwenye vyeo vya juu police, TPDF, TISS n.k
Mmoja kashitukiwa akiwa lieutenant colonel kalala mbele.
Vyombo vya ulinzi na usalama Bongo vinatukuzwa sana ila deeply hamna kitu
Dah.. aisee..
Na unaandika kwa amani kabisa..
 
Kwanza naomba mapovu yanaruhusiwa na hoja zina ruhusiwa ila mniache nabii nitoe yale nayaona...
Mziki ulianza Mozambique 🇲🇿 na sasa Congo DRC 🇨🇩 wanaucheza yes the dark days in Tanzania overseas intelligence....
Upo utani unasema nyani akimuona mwanamke basi kazi anayo ila akimuona mtoto wakiume hata kama ni mdogo basi nyani humkimbia yes twende na mimi....
Tanzania kwa miaka yote ni baba wa siasa za Africa 🌍 😑 ♥️ shime Mwalimu Nyerere tunakukumbuka Baba. Tanzania tumejaliwa na Taifa letu ninyumbani kwa wapigania uhuru wa Africa. Kete hii imetufanya kuwa na nguvu hata yakuweka watawala ktk nchi za Africa na huu uwezo umetuvimbisha bichwa haswaaa ila kwa wale mnasoma thread zangu mtakubaliana na mimi nimekuwa nikilia na idara zetu na kwenendo wa siasa zetu nakuona tunako enda basi kazi itakuwa ngumu.
Nakumbuka kuzitaadharisha idara za Taifa yakuwa mchwa ako kwa nyumba na paa likianguka amesha tafuna nyumba.

M23 wapo vitani na hii vita sio rahisi itakuwa ngumu kwa sababu ya conspiracy. Kagame kwa vyovyote huu ndio muda wake kumalizana na Tz wala sio nini wala nini hayati mch Mtikila aliwahi tuambia wakamalizana naye mapema kwa sasa sio siri Rwanda wanatujuwa vema Tz hata tujificheje wanajuwa siri zetu na huu ndio muda wakumalizana na sisi. Kuanguka kwa serikali ya Congo DRC nikishindo cha maumivu kwa serikali ya Tz. Natusibishane hili laweza tokea labda kama maamuzi magumu yatatokea yaani nyani aone mwanaume atarudi nyuma. Tangu Nyerere mpaka JK Rwanda hajapoa...
Rwanda anawaona Wabantu ndio kitisho cha kesho ya Tutsi na Tz ndio mlezi... SA ndio walewale na alie namba mbili ni uzao wa SA japo kazaliwa Tz ila history inasema wangoni ni wa SA unaweza kuona why Kagame hawez lala.
Pili Kagame ndio chairman EAC je unategemea nini kwa mfano?
Huu upupu ndio akili yako ilikoishia?
 
Kagame anafanya kuwaaminisha wanyarwanda kwamba Rwanda chini ya uongozi wake imekuwa na nguvu kubwa kijeshi kiasi cha kukabiliana na nchi zote za SADC, kaenda mbali zaidi hadi kuanza kuitunishia misuli South Africa.

Hii inampa mileage kisiasa na kuheshimika na kuogopwa, Jamaa anapenda kusujudiwa na anapenda kuogopwa, sasa ameona nchini kwake wananchi wanamlamba viatu kaona hapatoshi, ameanza kuleta udikteta wake kwa jirani zake.

Anapotoa kauli kama hizo kwamba yupo tayari kukabiliana na South Africa, wananchi wake nao wanakaa kwenye vijiwe wakiona Rwanda inaweza pambana na nchi yeyote Africa.

SANDF wana uwezo kupigana na Rwanda 10.
Nchi yenye military industrial complex kama SA si mchezo.
Japan alipoishambulia Pearl Harbor aliua askari 2300 wa USA, akajiona mwamba, kitendo kilichofanywa na US hadi leo imekuwa ni somo mashuleni wanafunzi wanasoma na kujibu mitihani.
South Africa ana hata na nuclear bomb. Ni nuclear power country!
 
NAto wamesanda kwa Putin kama SADC walivyosanda kwa PK.


Hapana Mkuu Kuna tofauti kubwa kati ya NATO na SADC, SADC hawajapigana na Rwanda na wala hawapigani na M23,Bali wanalinda amani,wakiamua kupigana Rwanda na M23 watashindwa mapema sana.
Sheria za kulinda amani ni ngumu sana.
Ila huko tunakoelekea Kuna uwezekano watu wakaamua kuipiga Rwanda yenyewe.
Kwa sababu ukitaka kumuua nyoka piga kichwa.
M23 ni kiwiliwili na Rwanda ni kichwa.
 
Hao Rwanda hakuna haja ya JWTZ kuingia vitani, watupe sisi jeshi la akiba (JKT mujibu wa sheria) tukamalize kazi.
 
Back
Top Bottom