Tetesi: Tetesi za usajili Ligi Kuu msimu wa 2026/27

Tetesi: Tetesi za usajili Ligi Kuu msimu wa 2026/27

Aman Josiah anaweza kuwa kocha msaidizi wa Simba endapo Matola ataondoka
 
FB_IMG_1780138410766.jpg
 
Mosses Shumah anatakiwa na Simba SC na Yanga
 
Bakari Msimu anatakiwa na Simba SC
Kwangu mimi huyo Msimu, William Edgar, Idd Nado na yule Rashid Chambo ndio mawinga ninaona wanafaa pale Simba. Wana kasi na nguvu sana aina ya mpira anaopenda Barker. Ila pale kwa Sopu naona ile ni dili ya wajanja pale Simba kwenye kamati ya usajili kama ilivyokuwa kwa Miraji Zambo.

Wazee wa dili walitafuta mpaka tiketi ya ndege kwa Zambo akajiunga "pre season" nje ya nchi kumbe chaguo la Fadlu lilikuwa Mligo. Sasa hivi wazee wa dili wameanza tena kwa Sopu huyu aliyechoka wakati Sopu alipokuwa wa moto walishindwa kumsajili. Na mbaya zaidi wana Karabaka aliye kwa mkopo ambaye kiwango kimepanda, wana Chasambi anayeozea benchi hapati nafasi na Bashir Kibailo aliyetoka timu "B" ambaye anaweza kucheza pembeni na katikati. Bado siioni nafasi ya Sopu pale Simba zaidi ya kuingozea tu Simba mzigo wa mshahara kwa mchezaji ambaye hatatumika na Simba bali ataishia kutolewa kwa mkopo.
 
Back
Top Bottom