Tetesi: Tetesi za usajili ligi kuu Tanzania bara 2024/2025

Tetesi: Tetesi za usajili ligi kuu Tanzania bara 2024/2025

Naona boss kakasirika.sana.
emoji23.png
naskia kuna mtu kaitwa dubai. Ni nani huyo mkuu ?
Chama huyo mkuu.
Mwamba namwamini kwa sasa, tetesi zake ni kweli
Huyu ni Mangungu mwenyewe.
 
Kuna uwezekano mkubwa leo,ikichelewa sana kesho atatambulishwa kocha mkuu( Fadlu Davids) kutoka Afrika kusini pamoja na wasaidizi wake watatu. Ni rasmi Sasa Matola na Mgunda hawatakuwa wasaidizi wake.
 
Rasmi sasa Charles Ahoua ametambulishwa
Ok mkuu hii ndio ipo sawa sasa. Naona safari hii Simba wamekuwa "serious" kiasi fulani ukilinganisha na miaka miwili/mitatu iliyopita ambapo Simba ilikuwa inajua tu kupointi vipaji ila ikifika kusajili wanaenda timu nyingine.

Lakini kamati ya usajili itaharibu kwa kitu kimoja tu nacho ni kuwa nimemsikia Ahmed Ally anapayuka kuwa Fred Funga Funga ndio msaidizi wa Mukwala. Kufeli ndio kutaanzia hapo kwani Mukwala akipata majeraha au kadi timu itakuwa inapoteza ushindi. Kumbuka kwenye mashindano makubwa nafasi za kufunga huwa chache sana sasa kwa Fred Funga funga anayefunga goli moja kwa kila nafasi zaidi ya nne itakuwa majanga.

Kama Simba wamemuacha Luis, Kramo basi wamalizie kabisa na Fred kwani pale mbele panahitajika watu wanaoweza kutumia nafasi kwa ufasaha. Kama hawajapata somo kwenye ligi iliyoisha kuwa magoli mengi ni muhimu basi hawatakaa waelewe ninachokizungumza hapa kuhusiana na kuwa wafungaji wakali angalau wawili wanaojua kufunga bila wasiwasi.
 
Kuna uwezekano mkubwa leo,ikichelewa sana kesho atatambulishwa kocha mkuu( Fadlu Davids) kutoka Afrika kusini pamoja na wasaidizi wake watatu. Ni rasmi Sasa Matola na Mgunda hawatakuwa wasaidizi wake.
Kuna mtu mmoja Simba ikimsainisha ...maua yako nitakupa
Japo mtiririko wako uko sahii

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom