Tetesi: Tetesi za usajili ligi kuu Tanzania bara 2024/2025

Huyu mwamba akija Yanga nitafurahi sana. Maana ni mwepesi, ana mbio, anapiga chenga na anatoa pasi za magoli.
Musonda ni complete player nashangaa wanaomlinganisha na mzize. Akiwa pembeni ni winga akiingia ndani anakuwa striker na target yake ni kubwa mno. Mchezaji mkubwa huonekana big matches
 
Nadhani mkanganyiko WA issue za udhamini na umiliki wa Vilabu ndo shida kubwa kwenye soka nchini. Utasikia mlezi wa Dodoma Jiji ni mjumbe wa kamati ya wadhamini wa Yanga mara mmiliki wa Singida mara Ihefu ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga. Kimsingi GSM ni mwekezaji Yanga hivyo hakupaswa kuwa mdhamini wa Coastal, Namungo, Prisons, Ihefu, Singida etc. Angalia matokeo ya Yanga na hizo timu kabla ya udhamini na baada ya udhamini. Si kwenye mpira tu mtu mmoja kumiliki viwanda viwili vitatu vya vya sukari au mitandao miwili ya simu mara benki moja kuimiliki nyingine kumetuletea changamoto kama Taifa. Vinaondoa ushindani na kuleta monopoly ya mmiliki kufanya anachotaka.
 
Kibu aje Yanga itakuwa safi sana pale mbele
 
Kuna tetesi Simba wametia nia kwa Aziz Ki
 

Hilo mnaloongea ni hisia na wala sio fact kwanini nasema hivyo?
Angalia timu ya Simba kwasasa imefungwa na Yanga nje ndani tena kwa idadi kubwa ya magoli je Simba ina udhamini wa GSM?

Kwanini tusiwaze kuwa timu zilizo dhaminiwa na GSM ndizo zimeonesha upinzani mkubwa kwa Yanga kuliko timu zingine ambazo hazidhaminiwi na GSM?

Tukiweka list za timu zilizofungwa magoli matano matano msimu huu je ngapi zilizo dhaminiwa na GSM zaidi ya Ihefu kwenye mechi ya marudiano ya ligi kuu?
Umeangalia mechi ya nusu fainali leo ya kombe la FA kati ya Ihefu na Yanga umeona mechi ilivyokuwa tough?

Nyie mnaongea hisia tu, ila ukweli ni kwamba hizo timu zilizo dhaminiwa na GSM na ambazo zinaonekana zina viongozi wenye ukaribu na Yanga ndizo ndio timu pekee zilizoipa Yanga upinzani. Prisons, Coastal, Ihefu, Dodoma jiji, Namungo, haikuwapa Yanga mechi nyepesi hata kidogo. Ila nje ya timu zisizo dhaminiwa na GSM tumeona Yanga akipata ushindi mkubwa na kushindwa kuipa Yanga upinzani
 
Tunaongelea fact siyo hisia bro. Kanuni za FFP na FIFA zinaruhusu kinachofanyika? Kwa nini udhamini wa GSM kwa ligi kuu ulikoma ghafla baada ya Barbara kusimamia kucha? Ushindani upi unaoongelea ? Angalia mechi za Yanga vs Coastal , Prisons na Namungo kabla na baada ya udhamini afu niletee matokeo
 

Kwanza sijakataa kuhusu hoja ya kikanuni, ila napokukatalia wewe ni kusema kuwa hao wapinzani hawatoi upinzani kwa Yanga kisa tu wanadhaminiwa na GSM hilo sio kweli.

Je Yanga ya kipindi cha nyuma ubora wake unalingana na Yanga hii ya sasa? Kama Yanga inaweza kupambana na akina Al Ahly, Belouizdad, Mamelodi, na Medeama na wakapata matokeo, itashindwa vipi kuwafunga timu za daraja la kati kama akina Coastal na Namungo? Zile timu zilizofungwa magoli matano matano ikiwemo Simba je zinadhaminiwa na GSM?

haya hoja yako ya mwisho unasema niangalie mechi za Yanga vs Coastal, Prisons na Namungo kabla na baada ya udhamini wa GSM. Ok sawa tuanze na timu ya Namungo.

Namungo ilipanda daraja kucheza ligi kuu msimu wa 2019/2020, je unajua kama Namungo walianza kudhaminiwa na GSM tokea 2020?

Ugumu na urahisi wa mechi ya Yanga dhidi ya Namungo haukuchochewa na udhamini wa GSM bali dhidi ya Yanga ya aina gani inayocheza?
Pamoja na hilo tokea Namungo ishiriki ligi kuu, hajawahi kumfunga Yanga zaidi ya kupata sare tu. Sasa unataka kusema nini hapo?
 
Tuendelee kwa upande wa Tanzania Prisons,
Nakuwekea matokeo ya Yanga vs Prisons tangu mwaka 2015 halafu ili ujishuhudie mwenyewe jinsi Prisons anavyonyanyasika kwa Yanga kabla ya hata GSM hajaidhamini hiyo Prisons. Tokea mwaka 2015 hadi sasa, Prisons kamfunga Yanga mara moja pekee tena ilikuwa 2018
 
Ushindani upi unaoongelea ? Angalia mechi za Yanga vs Coastal , Prisons na Namungo kabla na baada ya udhamini afu niletee matokeo

Tumalizie na matokeo ya timu ya Coastal union ambayo yenyewe tokea mwaka 2013 hadi sasa imeifunga Yanga mara mbili pekee.

Mwisho namalizia kwa kurudia nilichokisema juu kwamba kikanuni GSM anaweza kuwa anakosea kudhamini timu nyingi za ligi kuu, lakini kudhamini kwake hizo timu sio ndio kigezo cha Yanga kupata matokeo. Jana watu walishuhudia nusu fainali bora sana la kombe la FA kati ya Ihefu dhidi ya Yanga japo ina dhaminiwa na kampuni moja lakini Ihefu walikusudia kuiondoa Yanga mashindanoni, kwanini hilo tukio isiwaamshe kuhusu hali ya ushindani kwa hizo timu dhidi ya Yanga? Sijui hizo timu ndio zingekuwa zinapigwa goli tano tano na Yanga maneno yangezidi hapa.

Haya tuhitimishe kwa matokeo ya Coastal union ambayo imefanikiwa kumfunga mara mbili pekee tangu mwaka 2013

Source: sofascore & playmakerstats
 
Nadhani hoja kuu ni kanuni. Kama kanuni ni ya muhimu ugumu uko wapi kuifuata? Si TFF tu hata UEFA na FIFA kitu kinachofanyika Tanzania hakikubaliki. Naona msimu ujao itazuka tafrani kwa mtu mwingine kujitokeza kudhamini vilabu vingine jambo litakaloziibua mamlaka husika
 
Vipi kuhusu Prince Mpomelea Dube?
Nasikia Yanga washamsajili ni kweli?
 
Aende Chamazi Jangwani hatutaki wazee.
 
Onyango sikushauri,maana Onyango keshakwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…