Kamati kama hizi zimekwisha undwa mara kibao na matokeo yake bado ni hasara kwetu. Je, kuna uwezekano wa kuiweka mikataba iliyotangulia kuwa batili kutokana na mapungufu hayo?..
Haiwezekani isipokuwa wanatazama for the future agreements au sio?.
How many do we have at hand hivi sasa ambayo inasubiri wino - kuwekwa sahihi!..
Mimi na wewe nadhani hatujui hili.
wakati wa Mkapa tulikuwa na kamati,
JK alipoingia madarakani wametazama mapungufu hayo hayo na matokeo ndio hicho kipande cha keki asilimia 1.9..
Kwa hiyo, nikiyasoma vizuri maelezo yako kinachojitokeza wazi ni kwamba kamati hii haina mpango kabisa ktk maamuzi.
Mimi nilimwelewa JK kama ifuatavyo, kwamba nia ya ahadi yake ya
kutazama upya mikataba ya madini ilikuwa ni kipengele cha 15%, ambacho amekifanyia kazi, hili ndilo lililokuwa wazo lake pre-2005, na akawa akijua amelitimiza kwa kiasi na alikuwa akiendelea nalo! Na nadhani limefanywa na tume ya Lawrence Masha, ambayo aliahidi kuiunda na akatimiza pia, tofauti hii ilikuwa tume ndani ya serikali... tofauti na tume ya sasa,,, lakini tume ya sasa ina-replace tume ya Masha.
Katikati hapa ikaja issue ya Buzwagi, ikawa na issue mbili moja tuhuma za kusaini mkataba London, mbili mbona tunachopata kwenye madini kidogo?
1. Serikali ikajibu kwamba issue ya London hakuna utaratibu uliovunjwa, ikaishia hapo,
2. Issue ya mkataba wenyewe kwamba tunapata kidogo, serikali ikasema mbona kila kitu kilitoka kwenye Sheria ya 1998, kwa hiyo NO WRONG DOING, hivyo serikali haikuwa imeona umuhimu wa kuunda tume kwa sababu za Buzwagi.
Lakini Wananchi wakaendelea kuona tunapunjwa na makampuni yenye migodi, kelele zikaendelea na kelele hizi zikampa shida hata mkuu wa nchi, nadhani kwa busara zake akasema, well nadhani wenye mali (wananchi) huenda wana hoja, lakini hoja hii kwa sasa serikali haiaminiki kwa lolote itakalo sema kutoka na katume kao ka Dr. Lawrence Masha, huenda kuwaridhisha wenye mali inabidi.
1. Kuunda Tume nyingine ambayo composition yake iwe na hao wanaoona kwamba serikali inafanya ndivyo sivyo.
2. Kuwaridhisha wenye mali kwamba wanasikilizwa, wanaweza kui-task serikali yao...
Hivi ndivyo serikali ilichofanya.
Kwa maoni yangu serikali haikuwa tayari kuunda hii tume hii hata kidogo, ni mashinikizo yenu wananchi ndio yamefanya iundwe ili ku-clear tume...
Katika hili hapakuwa na sababu kwa hiyo ya kuangalia historia ya tume zilizopita, hii tume ya sasa ni kwa ajili ya:-
1. Kuangalia kama kuna opportunity ya kupata faida zaidi kwa madini yetu.
2. Kuwaridhisha wenye mali, mwanakijiji na mkandara kwamba mnasikilizwa.
Na kama haiwezi kuwa kamati ya kudumu kupitia mikataba yote kwani navyofahamu mimi kila mkataba wa madini lazima uwe na vipengele tofauti inategemea na kile kitakacho patikana kwani neno Madini linaunganisha vitu vingi, mfano leo hii tunapata asilimia ktk Almasi tukiwa na hisa ya Taifa wakati huo huo hatuna sehemu nyinginezo. Hivyo basi ni muhimu wawepo ktk kuutazama kila Mkataba kwa marefu yake na wakizingatia complication zilizopo.
What are expected deliverables, we better start afresh ili tusi-be-bogged down na mikata ambayo tulishasaini na kwamba hatuwezi badilisha lolote, let start afressh by knowing what do we really deserve?
Kamati hii iwe ya kudumu na pekee ndiyo ipewe madaraka ya kupitisha Mikataba baada ya kuiwakilisha Bungeni. Feedback zao zichukuliwe kama ni JICHO la Watanzania wote na muhimu tukiwa na wataalam wanaoaminika toka taasisi mbali mbali kwa mfano mapendekezo ya kampuni mwekeshaji yatolewe na STAMICO sio mwanasiasa.
Sawa tu, maoni Mazuri.
Ahsante kaka; tuendelee kulitetea taifa kwa unyenyekevu!