Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Huyu kijana ameonekana kupiga domo sana,baada ya uchunguzi wa kina ameonekana ana njaa,sasa amemegewa pande ili nae amungunye,mtaona sasa hatoki tena denda wala hatakuwa na uwezo wa kupiga makelele,tuna mbinu na mikakati ya kuwanyamazisha vijana wadogo wadogo.Ndio hivyo sasa ameingizwa kwenye ufisadi ule aliokuwa akiupigia makelele,jamani si mnayajua mambo ya kuunda unda tume,hivi tume ngapi zimeundwa kuhusiana na mambo mazito nitajieni moja tu iliyokuja na jawabu halafu likafanyiwa kazi....miezi mitatu !!!Mmesikia wapi anaeshitaki akahusishwa kwenye uchunguzi na washitakiwe wake.

..ukitaka kuongea tu,ruksa,maneno hayatozwi kodi!

..unakumbuka wale wafanyabiashara/watu wa madini wa morogoro waliopigwa risasi kule sinza? kamati au tume au whatever the @#$%!iloundwa!unakumbuka iliwasilisha taarifa halafu nini kikatokea?.....zombe et al, wako wapi?

..usiwape watu sababu!
 
Rev Kishoka:

I have read you loud and clear. Some people can be fooled for some time but not all the people all the time. Msimamo wangu kuhusu JK kuhusisha wapinzani kwenye hii kamati nilishautoa mara baada ya Kikwete kuzungumza kwenye mkutano mkuu wa chama chake. Na wapo walionipinga, nikautolea ufafanuzi zaidi mahali pengine, baadhi ya niliyoyasema yameanza kusemwa sasa baada ya Zitto kuteuliwa na wasifu wa wajumbe wengine kwenye kamati kuanza kujadiliwa. Ukipenda naweza kuweka hapa nini nilisema huko nyuma na nadhani chombo kimoja cha habari kilinukuu kidogo sehemu ndogo ya maoni yangu. Natofautiana na wanaopinga Zitto kushiriki kwenye kamati; ni vyema akashiriki ili kuthibitisha USANII wao akiwa ndani, cha msingi ni yeye kuendelea kuwa na msimamo. Binafsi naamini huu ni usanii mwingine tu, kwa nje ni sifa kuwa Rais amekuchukua hatua lakini kwa mlolongo wa matukio hiki ni kiini macho kingine. Ni kweli sisi kama chama tunapaswa kujadili. Nimevutiwa na uchambuzi wako kuhusu wajumbe walioteuliwe, na uchambuzi wa Mwafrika wa Kike, DUA na wengineo. Sina wasaa wa kuchukua michango yote na kuichambua kuiweka kama dossier moja kuhusu background ya wajumbe wote wa tume hii. Ningefurahi sana kama Mwafrika wa Kike akiniwekea muktasari wa hoja zote za msingi zilizotolewa kuhusiana na wajumbe wa Kamati na kutunitumia kwenye mnyika@yahoo.com ili tuifanyie kazi.

At the same time, ukirejea hotuba ya Rais Dodoma makundi mbalimbali aliyoahidi kuyashirikisha kwenye kamati mathalani wasomi(kwa maana ya kutoka academic institututions) na asasi za Kijamii(mathalani LEAT, LHRC nk) hazikushirikishwa. Hii ina maana ahadi yake hajaitimiza kwa ukamilifu wake.

Wakati huo huo kwenye hadidu rejea masuala ya haki za binadamu na mazingira katika maeneo yenye migodi hayajaguswa kwa ukamilifu wake.

Kuna haja pia ya kuhakikisha ripoti ya kamati hii inakuwa public, miezi mitatu si mingi sana. Ni vyema mjadala wa umma ukaendelea kwa kishindo.

Kamati ifanye kazi yake kwa uwazi, na ni vyema ikaanzia kwanza kwa kupitia kamati za nyuma kuhusu madini kama ile ya Mboma, ya Mang'enya, Kipokola, Masha nk- jambo hili nililisisitiza siku kadhaa nyuma nalirudia tena. It is a waste of resources kwamba ndani ya miaka isiyozidi sita tumeunda kamati nne katika suala hilo hilo.

Masuala ya msingi yanajulikana kwa kweli- ushiriki katika umiliki, uboreshaji wa mfumo wa kodi nk; kinachokosekana ni nia ya kisiasa. Na kinachochangia hali hii kwa kweli nadiriki kusema ni UFISADI! Lakini kila wakati tunakwepa chanzo cha msingi tunakimbilia kukabiliana na matokeo na tunakimbilia kufunika mijadala ya umma. Tunasahau kwamba kufukapo moshi ndipo moto utakapowaka

JJ

Asante Mnyika,

Natumaini kuwa CHADEMA kama chama mtakaa na kuhakikisha kuwa maslahi ya wananchi yanalindwa hapa kwa nguvu zote kama ambavyo mmekuwa mnafanya so far.

Kama mkizidiwa nguvu na spin master Mwakyembe na huyo mama wa IPTL - sijui nani vile! elewa kuwa hamtapata ize ride hapa na kutoka kwa wananchi vilevile. KUMBUKA YALIYOMPATA LAMWAI KWENYE ILE KAMATI SIJUI TUME YA KUCHUNGUZA NINI VILE miaka ile akiwa bado mpinzani!

Nitakutumia hoja zangu kama utahitaji maana naona Kikwete hataki kabisa hoja za wananchi ingawa anadai kuwa website kazi yake ndiyo hiyo - na baadhi ya mambo muhimu yoyote utakayohitaji.

Asante.
 
Nyangumi, Tume ya Rais haikuhitaji Wabunge kabisa, period. Ilihitaji wataalamu na wasomi kwani msingi wake ulikuwa ni katika sheria na taratibu. Siyo tume ya uchunguzi. Hivyo kungekuwa na wasomi wa sheria za Kimataifa, Mikataba ya Biashara, n.k


Mzee Mwanakijiji,
u got it wrong; tume haiendi kutunga au kurekebjisha sheria, tume inaenda kuangalia mapungufu ya sheria yetu ya madini, inaenda kuangalia what are the best practises globally,na kutoa mapendekezo on what be can done in order to maximize our interest as the resources owners,
it obvious that some, not neccessarily all of the recommendations from this commission, will be inputs kwa ile tume nyingine ya kurekebisha sheria, wao[tume ya kurekebisha sheria] ndio wataalamu wa sheria wataamua wachukue lipi na waache lipi, hao wataangalia muingiliano wa sheria ya madini na zingine nk., hawa ndio wanahitajika kuwa wanasheria per se! Tume tunayozungumzia ni ya kusema what are th..e owners expectations, what will be needed, it can recommend that we stop to provide exporation and mining licensing , say untill we are capable of doing that business.
Hili halimuhitaji Shivji.
Simply our requirements can well be defined by our representatives with little help of few experts not necessarily lawyers per se; these technorats will come later to streamline those expectations/ambitions/goals/objectives which are realitic and those which are not.
 
...the whole idea ya hii tume is very confusing!
 
...the whole idea ya hii tume is very confusing!


Main theme;,
ni kwa namna gani Tanzania itafaidika na madini yake?

Nini hakiko sawa sasa?is it policies, procedures, laws, regulations & control, bad contracts,people, or probably we are already there!!

Anyway, onces those weaknesses have been identified, what should/can then done?
 
Mzee Mwanakijiji,
u got it wrong; tume haiendi kutunga au kurekebjisha sheria, tume inaenda kuangalia mapungufu ya sheria yetu ya madini, inaenda kuangalia what are the best practises globally,na kutoa mapendekezo on what be can done in order to maximize our interest as the Asset owners,
it obvious that some not all of the recommendations from this commission will be inputs kwa ile tume nyingine ya kurekebisha sheria, wao[tume ya kurekebisha sheria] ndio wataalamu wa sheria wataamua wachukue lipi na waache lipi, hao wataangalia muingiliano wa sheria ya madini na zingine nk., hawa ndio wanahitajika kuwa wanasheria per se! Tume tunayozungumzia ni ya kusema what are th..e owners expectations, what will be needed, it can recommend that we stop to provide exporation and mining licensing , say untill we are capable of doing that business.
Hili halimuhitaji Shivji.
Simply our requirements can well be defined by our representatives with little help of few experts not necessarily lawyers per se; these technorats will come later to streamline those expectations/ambitions/goals/objectives which are realitic and those which are not.

Hayo niliyopigia msitari kwa kuanzia ndio yanachanganya hapa
 
kingine pia ni muingiliano wa tume zaidi ya moja hii, ile ya kupitia madini, na ile ya mazingira, na pccb, na ile itakayoundwa baadae kumchunguza Karamagi, na kazi ya kila siku ya polisi na vyombo vya usalama, na ile ya maadili, na ile kamati ya maadili, na kazi ya waziri mkuu, na sijui nini vile?, na:

hizikamatinatumenakazizakezisizotiliwamaananiinachanganya.co.ney
 
Kilitime,
Maelezo makini sana ulotoa mjomba, ila umeacha kitu kimoja muhimu sana.
Kamati kama hizi zimekwisha undwa mara kibao na matokeo yake bado ni hasara kwetu. Je, kuna uwezekano wa kuiweka mikataba iliyotangulia kuwa batili kutokana na mapungufu hayo?..Haiwezekani isipokuwa wanatazama for the future agreements au sio?. How many do we have at hand hivi sasa ambayo inasubiri wino - kuwekwa sahihi!..
wakati wa Mkapa tulikuwa na kamati, JK alipoingia madarakani wametazama mapungufu hayo hayo na matokeo ndio hicho kipande cha keki asilimia 1.9..
Kwa hiyo, nikiyasoma vizuri maelezo yako kinachojitokeza wazi ni kwamba kamati hii haina mpango kabisa ktk maamuzi. Na kama haiwezi kuwa kamati ya kudumu kupitia mikataba yote kwani navyofahamu mimi kila mkataba wa madini lazima uwe na vipengele tofauti inategemea na kile kitakacho patikana kwani neno Madini linaunganisha vitu vingi, mfano leo hii tunapata asilimia ktk Almasi tukiwa na hisa ya Taifa wakati huo huo hatuna sehemu nyinginezo. Hivyo basi ni muhimu wawepo ktk kuutazama kila Mkataba kwa marefu yake na wakizingatia complication zilizopo.
Kamati hii iwe ya kudumu na pekee ndiyo ipewe madaraka ya kupitisha Mikataba baada ya kuiwakilisha Bungeni. Feedback zao zichukuliwe kama ni JICHO la Watanzania wote na muhimu tukiwa na wataalam wanaoaminika toka taasisi mbali mbali kwa mfano mapendekezo ya kampuni mwekeshaji yatolewe na STAMICO sio mwanasiasa.
 
nitatoa maoni yangu baada ya tume kuwasilisha ripoti
 
-Pongezi za nini? wakati kachelewa sana kutimiza huo ulio wajibu wake?

-Si hilo tu, kashindwa kumuwajibisha kiranja mkuu EL kwa kuzuia/kuzima kamati ya bunge isiundwe yenye jukumu hasaaaa la kutunga hizo sheria!!

-Hii kamati ina tofauti gani na ambayo ingeundwa na bunge waliyo izuia?

Tatizo letu watanzania ni kitu kidogo tu eti pongeziii!! Tunaridhika na kusahau ufisadi wooote anao endelea kuukumbatia!


Pumbafffffffff!!!
 
Kamati kama hizi zimekwisha undwa mara kibao na matokeo yake bado ni hasara kwetu. Je, kuna uwezekano wa kuiweka mikataba iliyotangulia kuwa batili kutokana na mapungufu hayo?..
Haiwezekani isipokuwa wanatazama for the future agreements au sio?.

How many do we have at hand hivi sasa ambayo inasubiri wino - kuwekwa sahihi!..
Mimi na wewe nadhani hatujui hili.

wakati wa Mkapa tulikuwa na kamati,
JK alipoingia madarakani wametazama mapungufu hayo hayo na matokeo ndio hicho kipande cha keki asilimia 1.9..
Kwa hiyo, nikiyasoma vizuri maelezo yako kinachojitokeza wazi ni kwamba kamati hii haina mpango kabisa ktk maamuzi.
Mimi nilimwelewa JK kama ifuatavyo, kwamba nia ya ahadi yake ya kutazama upya mikataba ya madini ilikuwa ni kipengele cha 15%, ambacho amekifanyia kazi, hili ndilo lililokuwa wazo lake pre-2005, na akawa akijua amelitimiza kwa kiasi na alikuwa akiendelea nalo! Na nadhani limefanywa na tume ya Lawrence Masha, ambayo aliahidi kuiunda na akatimiza pia, tofauti hii ilikuwa tume ndani ya serikali... tofauti na tume ya sasa,,, lakini tume ya sasa ina-replace tume ya Masha.

Katikati hapa ikaja issue ya Buzwagi, ikawa na issue mbili moja tuhuma za kusaini mkataba London, mbili mbona tunachopata kwenye madini kidogo?
1. Serikali ikajibu kwamba issue ya London hakuna utaratibu uliovunjwa, ikaishia hapo,
2. Issue ya mkataba wenyewe kwamba tunapata kidogo, serikali ikasema mbona kila kitu kilitoka kwenye Sheria ya 1998, kwa hiyo NO WRONG DOING, hivyo serikali haikuwa imeona umuhimu wa kuunda tume kwa sababu za Buzwagi.

Lakini Wananchi wakaendelea kuona tunapunjwa na makampuni yenye migodi, kelele zikaendelea na kelele hizi zikampa shida hata mkuu wa nchi, nadhani kwa busara zake akasema, well nadhani wenye mali (wananchi) huenda wana hoja, lakini hoja hii kwa sasa serikali haiaminiki kwa lolote itakalo sema kutoka na katume kao ka Dr. Lawrence Masha, huenda kuwaridhisha wenye mali inabidi.
1. Kuunda Tume nyingine ambayo composition yake iwe na hao wanaoona kwamba serikali inafanya ndivyo sivyo.
2. Kuwaridhisha wenye mali kwamba wanasikilizwa, wanaweza kui-task serikali yao...
Hivi ndivyo serikali ilichofanya.

Kwa maoni yangu serikali haikuwa tayari kuunda hii tume hii hata kidogo, ni mashinikizo yenu wananchi ndio yamefanya iundwe ili ku-clear tume...

Katika hili hapakuwa na sababu kwa hiyo ya kuangalia historia ya tume zilizopita, hii tume ya sasa ni kwa ajili ya:-

1. Kuangalia kama kuna opportunity ya kupata faida zaidi kwa madini yetu.
2. Kuwaridhisha wenye mali, mwanakijiji na mkandara kwamba mnasikilizwa.


Na kama haiwezi kuwa kamati ya kudumu kupitia mikataba yote kwani navyofahamu mimi kila mkataba wa madini lazima uwe na vipengele tofauti inategemea na kile kitakacho patikana kwani neno Madini linaunganisha vitu vingi, mfano leo hii tunapata asilimia ktk Almasi tukiwa na hisa ya Taifa wakati huo huo hatuna sehemu nyinginezo. Hivyo basi ni muhimu wawepo ktk kuutazama kila Mkataba kwa marefu yake na wakizingatia complication zilizopo.
What are expected deliverables, we better start afresh ili tusi-be-bogged down na mikata ambayo tulishasaini na kwamba hatuwezi badilisha lolote, let start afressh by knowing what do we really deserve?

Kamati hii iwe ya kudumu na pekee ndiyo ipewe madaraka ya kupitisha Mikataba baada ya kuiwakilisha Bungeni. Feedback zao zichukuliwe kama ni JICHO la Watanzania wote na muhimu tukiwa na wataalam wanaoaminika toka taasisi mbali mbali kwa mfano mapendekezo ya kampuni mwekeshaji yatolewe na STAMICO sio mwanasiasa.
Sawa tu, maoni Mazuri.

Ahsante kaka; tuendelee kulitetea taifa kwa unyenyekevu!
 
Iddi Simba joins team to review mining contracts

2007-11-15 10:09:38
By Guardian Reporter


The just-formed presidential committee tasked with reviewing the mining contracts in which the Government has a stake has got a twelfth member - industrialist and former minister Iddi Simba.

This is according to a terse State House statement issued by Chief Secretary Philemon Luhanjo in Dar es Salaam yesterday, only a day after it was announced that President Jakaya Kikwete had delivered on his recent promise to pick a team of experts to study the matter and advise the Government accordingly.

``President Jakaya Kikwete has appointed Hon Iddi Simba one of the members of the committee charged with reviewing mining contracts under the chairmanship of (former Attorney General) Hon Mark Bomani,`` reads part of the statement.

Simba is a businessman-cum-politician who once served as Trade and Industries minister under retired President Benjamin Mkapa�s third-phase government.

He is held in high regard in both business and political circles in the country, particularly in connection with his championing of the need to empower indigenous Tanzanians.

The statement said the former legislator for Dar es Salaam�s Ilala constituency was expected to work alongside his 11 colleagues named late on Tuesday.

These include fiery Kigoma North legislator Zitto Kabwe from the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), suspended from the National Assembly a few months ago over charges of improper behaviour.

Zitto has been under suspension since the last budget meeting after calling for the formation of a parliamentary team to probe the controversial Buzwagi Mine contract.

His proposal provoked heated debate inside and outside the House, with some opposition leaders going around the country urging the people to demand that the Government respond to the MP�s arguments instead of making attempts to silence him.

A number of Government ministers soon made similar tours but this time specifically to undo the �damage� done by the opposition camp.

Among the other members of the presidential committee are legislators John Cheyo (Bariadi East - United Democratic Party), Dr Harrison Mwakyembe Kyela - CCM), and Ezekiel Maige (Msalala - CCM).

Also in the team are Peter Machunde from the Dar es Salaam Stock Exchange, David Tarimo from PriceWaterhouseCoopers, and Maria Kejo from the Justice and Constitutional Affairs ministry.

The others are Energy and Minerals ministry lawyer Salome Makange, Mugisha Kamugisha from the Finance ministry, and Edward Kihundwa from the Lands, Housing and Human Settlements Development ministry.

The committee is expected to review mining contracts and any other documents related to commercial mining as well as evaluate and sort out the taxation system applicable to the country�s mining sector.

It is also charged with assessing mining activities and sort out rights and responsibilities of investors on the one hand and the Government on the other.

The committee, which has three months within which to complete its work, is under instruction to meet with the Chamber of Mines and other key stakeholders before giving its recommendations.

SOURCE: Guardian
 
Lovely, maana Idd Simba huwa ni mzuri sana kwenye kuita spade a spade, na at this point and time hana anything to gain au to lose, kwa hiyo now Muungwana is talking!

Huyu Simba, ndiye aliyemung'oa Mbilinyi kwenye minofu ya samaki, safi sana kumuweka kwenye kamati!
 
Sasa huyu Mwakyembe atajigawaje???
It suprises me how the so called "system" works asubuhi Mh JK anamteua Mwakyembe kuwa kwenye kamati....jioni Mh Spika anamteua Mwakyembe kuwa kwenye kamayi nyingine....hakuna mawasiliano?????????????? I mean ya walioko kwenye hiyo "system"!
 
Lovely, maana Idd Simba huwa ni mzuri sana kwenye kuita spade a spade, na at this point and time hana anything to gain au to lose, kwa hiyo now Muungwana is talking!

Huyu Simba, ndiye aliyemung'oa Mbilinyi kwenye minofu ya samaki, safi sana kumuweka kwenye kamati!

Hapo si uongo mkuu.

Mbona hawa watu walisema Zitto alitakiwa kujielimisha kuhusu sheria za madini?Nakumbuka kuna thread aliyoleta Mugongo Mugongo ya tarehe 18 August hapa ikiwa ni juu ya kuchambuliwa hoja ya zitto kipengele baada ya kipengele.Kwenye kuichambua ile hoja sijui ni Karamagi au ni Mbunge aliseama Zitto ajielimishe kuhusu hii sheria ya madini.

Sasa hapa ina maana mheshimiwa JK ameweka wajumbe wa kamati ambao ni vilaza? Maanake kama yule waziri alikua sahihi basi Jk nae tuanze kumbadilishia upepo dhidi ya teuzi zake.

Maanake hawezi akaleta usanii for the sake of political credibility ambazo ni personal gains kwenye ishu serious ya kitaifa kama hii tukamuacha
 
Waungwana,

Nisaidieni, hivi kulamba dume maana yake nini? Hivi ni kiswahili sahihi mpaka hata gazeti la maana kama Majira watumie hilo neno?


JK umelamba dume


RAIS Jakaya Kikwete juzi aliteua Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini nchini, akijumuisha wabunge wa kambi ya Upinzani, Bw. Zitto Kabwe wa CHADEMA na Bw. John Cheyo wa UDP.

Uteuzi huo ni katika kutimiza ahadi yake alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, ambapo katika kamati hiyo ya kuangalia mikataba ya madini aliahidi kushirikisha watu wa kada mbalimbali wakiwamo wapinzani.

Pengine uteuzi wake huo uliamsha hisia tofauti kwa baadhi ya watu hasa kutokana na kujumuishwa kwa jina la Bw. Kabwe, Mbunge machachari aliyeibua sintofahamu bungeni kutokana na kuwasilisha hoja binafsi ambayo ilimsababishia adhabu ya kusimamishwa kazi.

Tunaamini Rais ametumia busara sana katika kufanya uteuzi huo, hususan wa kumjumuisha Bw. Kabwe, kutokana na kuwa mmoja wa watu ambao wanaonekana kuielewa vema sekta hiyo ya madini na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa Kamati na Taifa kwa ujumla.

Lakini si hivyo tu, hiyo inaonesha jinsi ambavyo Rais anaelewa kuwa si kila aliye katika kambi ya Upinzani basi hana manufaa kwa Taifa na kwamba si kila aliye ndani ya Chama Tawala basi ndiye kila kitu kwa ustawi wa Taifa hili.

Bila shaka Rais amezingatia, kwamba kuwa katika Upinzani hakumwondolei mtu utanzania wake na hivyo linapotokea tatizo katika nchi hapana budi kila mmoja kwa nafasi yake bila kutanguliza itikadi anastahili kushiriki kulimaliza ili mradi akijua tu kuwa ni kwa maslahi ya nchi.

Ni matumaini yetu kuwa Bw. Kabwe atakuwa ametambua heshima kubwa aliyopewa na Rais ya kumpa jukumu zito la kuondoa utusitusi ulioigubika sekta hii ya madini nchini kwa kushirikiana na wataalamu na wadau wengine na kwamba ataifanya kwa moyo mmoja.

Sisi tunamshauri Rais Kikwete, ili aweze kuivusha nchi hii, basi aendelee na utaratibu huo huo wa kubaini kama kuna mtu ana uwezo wa kuisaidia nchi hii, basi asisite kumpa majukumu bila kuangalia anatoka kambi gani kwa kuwa nchi hii ni yetu sote na ikizama tunazama nayo sote.

Tunaitakia kila la heri Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini, huku tukiwaomba wadau wote watoe ushirikiano mkubwa kwake, ili kufanikisha yale ambayo Rais anataka yafanikiwe na hatimaye tujiletee maendeleo kama Watanzania.
 
Mwakyembe aachie ngazi kamati moja na lissu aongeze
 
Back
Top Bottom