technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,706
- 52,355
Ni vile watu tumeipuza siasa na kwenda kwenye Mambo ya msingi baada ya kuona siasa ni Mambo ya kipumbavu!Miaka mingi nyuma, majina ya viongozi wengi yalikuwa maarufu kwa wananchi, siku hizi mimi kuwajua hata mawaziri tu ni shida, yaani mpaka afanye mambo ya kiki ndo nimjue, sijui kama ndo ilivyo kwa wengine!
Jaji Mfawidhi M.M. Siyani asisitiza mahakimu wafawidhi kusikiliza mashauri kwa kuzingatia weledi na kutenda haki ili wasiathiri Imani ya wananchi kwa Mhimili wa Mahakama.
Jaji Mfawidhi Mustapher Mohames Siyani alisema Mahakama haiwezi kujitenga na mchakato wa kidemokrasia wa nchi yetu,hivyo ushiriki wa muhimili uko katika hatua zote ikiwemo kabla ya kuanza kwa uchaguzi na hata baada ya matokeo kutangazwa.
Cliche..zamani ukikomenti na kutupia neno sukuma gang unapata likes kama zote..sasa hivi limewakinaiSukuma Gang linapukutishwa kwa kasi kubwa
So lazima lakin pia si ustaarab.Wawe wanaweka na sababu za kutenguliwa pia ingependeza ili wengne wajifunze
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwani Siyan si alijitoa?Mbowe anapangiwa Jaji mwingine!
Katiba ndio mchawi haya mambo ya kuteuwana gizani yamepitwa na wakatiWawe wanaweka na sababu za kutenguliwa pia ingependeza ili wengne wajifunze
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Siku hizi viongozi hawaendi kwa wananchi,muda mwingi wanawalaumu wataalamu na watendaji kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi.Miaka mingi nyuma, majina ya viongozi wengi yalikuwa maarufu kwa wananchi, siku hizi mimi kuwajua hata mawaziri tu ni shida, yaani mpaka afanye mambo ya kiki ndo nimjue, sijui kama ndo ilivyo kwa wengine!
Kama kuna ukweli hiviNi vile watu tumeipuza siasa na kwenda kwenye Mambo ya msingi baada ya kuona siasa ni Mambo ya kipumbavu!
Mi nilisikia ni chakula MpangoWatu wali doubt alipokuwa DC Ila saivi sijui watajua ni chakula Cha Nani vile
Huu uteuzi wa Siyani umekuja kimkakati au ni mpango uliokuwepo?
Hasa wakati huu ambao hukumu ya kesi ndogo ilikuwa inasubiriwa tar 19.10.2021, napata mashaka.
Nilimkubali sana alivyosikiliza kesi ndogo ya Mbowe, alikuwa kama refarii haswa, upande mmoja ukiweka objection anauliza upande wa pili wanaonaje, then wakijibu anarudi kwa upande wa waliotoa objection kama wanakubaliana na hoja ya upande wa pili, wakikataa, jaji anaangalia sheria inasemaje, then anaupa haki upande unaostahili kesi inaendelea kusikilizwa.
Sijui kama wataipangia kesi jaji mwingine, if yes, napata ukakasi na huu uteuzi kama sio wa kimkakati, kumuondoa huyu aliekuwa anaenda na sheria halafu wamrudishe kama yule wa mwanzo kuwafundisha jamhuri nini cha kufanya, fingers crossed.
Kheri yao wateuliwaji......Namuona dada sofia mjema kaongezewa ugali wake
Amepanda. Kutoka Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, hadi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, (Justice of Appeal).Hii ya Jaji Makungu imekaeje,amepanda cheo au kashushwa.au maandalizi ya kuwa jaji mkuu
Nahisi kuna kitu hapa hasa ukiangalia ile kesi ilivyokaa kisiasa.Nina wasiwasi kwamba huu ni mkakati maalum wa kuchelewesha kesi hiyo na kuzidi kumdhalilisha Mbowe na si ajabu hata kumfunga.