Eti Emmanuel kasomi Kaachwa Pale Mama Alipo Chama Mkeka.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakicheka na kuuliza mbona hatukuona kwenye mkeka wa mama?huku pia ukikutana na vijana utaona wana vichwa vya binadamu kumbe wamebeba mapapai. Wengine wamebeba vichwa vya matikiti maji japo ukimuangalia katulia utadhani ni kichwa cha binadamu. Ni wabishi kweli kweli na kujiona wao ni maalumu katika nchi hii, wamejaa ubaguzi dhidi ya raia wengine ndani ya nchi.
Watu hawa wanapatikana kwenye vyama vyetu vya siasa, wapo
NCCR Mageuzi, CHADEMA, CUF ACT Wazalendo na CCM. Wanapatikana
BAVICHA au UVCCM nk, wanapenda kulalamika na kuona kila jambo la manufaa linawafaa wao na si kwa wengine kwa kuwa siyo sehemu ya itikadi yao. Watu wa namna hii iwapo tutawaacha wakaendelea kukuza matabaka, mwisho wake tutaingia kwenye machafuko.
Ukipita kwenye mitandao ya kijamii, wapo baadhi ya watu wanaolalamika kuwa "
Mama kachana mkeka" nikiwa kwenye usafiri nawasikia vijana wakilalamika sana juu ya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya. Walilaumu kuwa "Mama kachana mkeka!". wakati natembea niliwasikia vijana wakilalamika kuwa "Mama kachana mkeka!" Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kusema ni bora wahamie upinzani kuliko kubaki CCM ambako hawapati fursa. Watu wa namna hii ndiyo wamebeba matikiti au mapapai, hawafai kabisa hata kidogo.
Hebu tupitie kidogo uteuzi huu wa Wakuu wa Wilaya, ili tujenge hoja vyema:
Mosi idadi yao, wapo jumla ya wakuu wa Wilaya 139. Wanaume wako 95 sawa na 68% wanawake wako 44 sawa na 32%, vijana wenye umri chini ya miaka 35 wako 28 sawa na 20% ya wakuu wote wa wilaya. Ukichukua idadi ya Watanzania ni zaidi ya milioni 60, idadi ya wanachama wa UVCCM ni zaidi ya milioni 4, nani achaguliwe na nani aachwe? Kwa hiyo wanaolalamika wapo CCM kwa maslahi binafsi na siyo itikadi ya chama?
Pili uzoefu wao, ukiichunguza vyema utabaini kila mmoja ana uzoefu katika kazi fulani, wapo wasanii 2, Walimu 3, Wanasheria 3, Wanahabari 4, Watumishi wa Umma 11, askari 13, waliotoka kwenye siasa za ndani ya chama 9, Wabunge wastaafu 11 na wakuu wa Wilaya wa zamani 83. Wanaolalamika mama kuchana mkeka na kuwaacha kama faida potea kwani waliyo teuliwa siyo watu?walitaka azingatie sifa ipi? Walimu wangapi wameachwa? Askari wangapi wameachwa? Matabibu na wauguzi wangapi wameachwa? Wapo watu wangapi wenye uzoefu wameachwa lakini hawalalamiki? Hii ni roho mbaya ambayo haipaswi kupewa nafasi kwa mstakabali wa afya ya nchi.
Tatu suala la elimu, Mama kazingatia sana usawa katika elimu, wenye PhD wenyewe wanaita uzamivu ni 8%, wenye shahada ya Umahiri wapo 19% wenye shahada ya kwanza wapo 68% stashahada wapo 2% na Sekondari wapo 3%. Kwa namna hii mama hajafanya upendeleo, kachukua makundi yote ya elimu ili kuleta usawa.labda kasiri la saba, Wanaolalamika mlitaka ateue kwa namna gani?
Ukiwasikiliza kwa makini vijana hao walikuwa wakihoji juu ya teuzi ya watu waliotoka upinzani. Wanahoji juu ya teuzi za: Mozes Machali, Joshoa Nassari, Faki Lulandala, Julius Mtatilo, Albert Msando, Vicent mashinji na Lijua Likali wengine walienda mbali mpaka wakahoji juu ya teuzi ya David Zacharia Kafulila
acha niwape ushauri hawa ndugu zangu.
Mosi, mnapaswa kujua wote walioteuliwa ni Watanzania, Hawa watu wametoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kwa ushindi wa CCM mwaka 2020. Wengine waliachana na ubunge kwenye vyama vyao vya upinzani wakajiunga ndani ya chama. Huu ni mchango mkubwa sana kwa chama, walihatarisha maisha yao pamoja na familia zao kwa mapenzi ya chama. Leo tunapiga kelele wasipewe nafasi, wengine walikuwa viongozi wakubwa ndani ya vyama vyao rejea Mashinji. Bado tunawaona hawafai, huu ni ubaguzi ambao kamwe haupaswi kuungwa mkono.
Pili ujengaji wa hoja na kuzisimamia, hao tunaowaona hawafai ndiyo wamesaidia kufichua mambo ya hovyo yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wetu ndani ya chama kipindi cha nyuma. Nani asiyejua mchango wa Kafulila kwa nchi yetu alipokuwa upinzani? Nani asiyejua mchango wa Machali na Lijua Likali wakiwa bungeni? Nani asiyejua mchango wa Nassari, Mtatilo, Msando na Lulandala? Nani asiyejua mchango wa Dkt Vicent Mashinji ndani ya CCM. Mbali ya uanachama wa CCM lakini wana uwezo wa kiutendaji kazi, tunapaswa kuwatia moyo badala ya kuwazodoa. Ukuu wa Wilaya ni ngazi kubwa ya kiuongozi, mama kazingatia mambo mengi katika teuzi hizo.
Tatu tupunguze kulalamika, badala yake tukosoe sehemu isiyo sahihi lakini tushauri pale penye makosa. Chama ni watu lakini wasiwe watu wenye kutaka kunufaika badala ya kuwafanyia kazi raia.
Nne tuondoe fikra za teuzi vichwani mwetu, tutafute njia nyingine za kuingiza vipato. Tushauri serikali kuimarisha mazingira mazuri ya upatikanaji wa ajira, tuishauri serikali utoaji wa haki sawa kwa Watanzania wote pasipo kuangalia ukanda, udini, uchama na mambo mengine ya hovyo.
Tano tupunguze kujikombakomba kwa viongozi, tuache kuwasiriba wenzetu kwa viongozi ili tuonekane wazuri. Tuwaambie kinaga ubaga viongozi wanapokwenda nje ya taratibu zilizopo pasipo kupepesa macho.
Sita vijana wa UVCCM mjifunze mazuri ya vijana wa Upinzani, miongoni mwa mambo niliyojifunza kutoka kwa vijana hawa. Wanauwezo wa hali ya juu kusimamia hoja zao, hawajikombi kombi kwenye ukweli wao husema bila kuogopa.
Saba siyo lazima uteuliwe wewe au Emmanuel kasomi. Anaweza akateuliwa mtu mwingine kulingana na mahitaji ya mteuaji. Kulazimisha kuteuliwa matokeo yake ndiyo tunapata viongozi wa hovyo, viongozi wanaoongeza migogoro kwa raia badala ya kutatua migogoro hiyo. Hakuna mkataba baina yako na mteuaji hivyo toa ushirikiano kwa walioteuliwa.
Nashauri tuachane na ubaguzi, mtu apewe majukumu kulingana na uwezo wake katika kutimiza majukumu. Tumuache mama wa watu hata kama kachana mkeka, mbona huko nyuma haya yalitokea mkawa kimya? Mbona hamkuhoji teuzi ya Daniel Makanga? Mbona hamkuhoji juu ya teuzi za Wasira na Guninita? Mbona hamkuhoji juu ya Masumbuko Lamwai, Akwilombe, Kiffu Guram Hussein, Kaburu na Salum Sabaha? Au kwa kuwa ni muda mrefu? Mbona hamkumwambia Mwamba wa chato juu ya Waitara, Silinde, Katambi, Mwambe na Polepole. Hamkumhoji mwanaume wa shoka juu ya teuzi alizokuwa akizifanya? Hebu tumwache mama wa watu achape kazi ila tumshauri akijikwaa. Hahaaaaaaa "Mama kachana mkeka"
Mniache mimi mwana JF mtukutu