Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Nakubaliana na yote uliyoandika kasoro pale unapomkosoa Rais Samia SSH kumteua Biswalo kuwa Jaji.Huyu Mganga hafai kuwa mtumishi wa umma anatakiwa kuwa gerezani kabisa.
Pima kati ya mawili lipi ni jema. Biswalo kubakia DPP ambaye maamuzi yake ya kimashtaka yeye hawi challenged na mamlaka nyingine yeyote, au kuwa Jaji wa Mahakama Kuu anaweza kuwa challenged na Mahakama ya Rufaa?
Kumtoa DPP ni suala la kikatiba/ kisheria kama ilivyo kumtoa CAG. Rais ana mamlaka ya kuwateua, lakini kuwatoa ofsini ni mchakato mrefu.
Je mnataka Rais avunjje Katiba Kama Mwendazake alivyofanya kwa kutoa Prof Assad aliyekuwa CAG?
Tumepata Rais msikivu na anayependa kufuata Katiba, asiyependa kuonea watu bado haturidhiki?
Hebu tujifunze kwa yaliyotupata baada ya kumponda JK tukapata lile Shetani la Chato