Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha ndugu zangu wanaJF.
Naungana na ndugu Charles Kitwanga kuhitimisha kwamba mama Samia ni Rais mzuri mwenye uwezo wa kuivusha nchi salama lakini amezungukwa na GENGE la watu (possibly SUKUMA GANG) wanaomshauri vibaya.
Tangu Rais Samia aanze uteuzi wa viongozi, kwa kuondoa timu aliyoirithi kutoka kwa hayati Magufuli, nimekuwa nikifuatilia teuzi zake nimegundua ziko biased kwa misingi ya udini na ujinsia. Mara nyingi kila anapofanya teuzi mpya, kuwahamisha wizara au kuwafuta kazi baadhi ya wasaidizi wake, anarudia tatizo lile lile.
Nadhani huu ni mwendelezo mbaya kutoka kwa genge la watu wanaomshauri. Mfano mzuri ni huu uteuzi aliofanya jana. Yaani uteuzi wake umejaa udini na ujinsia kila kona. Ifike mahali Rais Samia aache kusikiliza ushauri wa hili genge ili asijiingize kwenye tatizo la kuigawa nchi kidini bila sababu za msingi.
Nashauri anapofanya uteuzi ajaribu kubalance kwa sababu watanzania wote wanamtazama na bahati mbaya wengine hawajui kama anashauriwa vibaya. Wanadhani anafanya makusudi.
Nawasilisha.
RAIS SAMIA NA TEUZI ZA UDINI.
Toka Rais Samia apate 'ngekewa' ya kuongoza nchi hii ameonyesha upendeleo wa wazi wazi katika Teuzi zake kwa watu wa imani yake na kuwatenga WAKRISTO, hili halihitaji Rocket Science
ili kuweza kulibaini.
Upendeleo huu wa kuwabagua upande mmoja na kupendelea upande mwengine kisa tu watu wa imani yako unaleta/utaleta utengano wa kitaifa hili swala linabidi likemewe vikali na washauri wa Rais wamueleze wazi wazi misingi ya nchi hii bila kificho wala haya kwamba mama unapoelekea huku sipo.
Tazama teuzi za Mawaziri,Katibu Wakuu,RCs,DCs,MADAS na MADED,Majaji,Mahakimu,Wakuu wa Mashirika/Idara,nk.
Kila teuzi atakayotoa Samia wewe angalia wa imani ile wako wangap na imani hii wako wangapi,hapo ndipo utaona upendeleo uliokithiri.
Mtu mmoja akaenda mbali akasema ukiwa mpemba au unatoka visiwani tu mama lazima akuteue na hili nadhani liko bayana katika kila teuzi anayofanya
mfano Teuzi za leo,Ameteua wafuatao
1.Mbarouk Salim Mbarouk~Makamo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
2.Balozi Ramadhani Mapuri~Mjumbe Tume ya Taifa ya Uchaguzi
3.Dk Zakia Mohamed Abubakari ~Mjumbe Tume ya Taifa ya Uchaguzi
4.Prof.Idrissa Mshoro~Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa wakala wa Ndege za Serikali(TGFA).
5.Benjamin Mashauri Magai~Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
katika teuzi hizi zaid ya 97% ni imani yake na huku akiitelekeza jamii nyingine,Taifa lisilo na usawa katika uwakilishi ni bomu linalosubiri kulipuka.
Mwenye masiko na asikie,Na mwenye macho ni atazame!