Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Mamlaka zetu nyingi zimekuwa zikifanya kazi katika mfumo ule ule wa zamani tofauti na hali halisi ya sasa.
Kwenye masoko ya vyakula hali ni hatari mno maana wananchi wengi wanalishwa sumu bila kujua,na lengo la mfanyabiasha ni kupata pesa bila kujali anaenda kumuumiza mlaji.
Juzi kuna Mama mmoja rafiki yangu ambae ni mkulima wa mboga mboga,wakati akiwa shambani anachuma mboga nikamuambia aniuzie mboga kwa ajili ya kula siku hiyo lakini alichonijibu ni kuwa "rafiki yangu hizi mboga nimepiga dawa asubuhi Yaani sumu ya kuua wadudu siwezi kukuuzia hizi maana najua ni hatari" alichoniambia nisubiri baada ya siku tatu au nne dawa itakuwa Imeisha atanichumia.
Nikisikitikia sana kwa kuwa niliona kabisa watu wanaenda kupata maradhi tofauti tofauti kutokana na ulaji wa vyakula vyenye viambata vya sumu.
Hili pia niliwahi kuona kwa wakulima wa nyanya, biringanya nk. Anapiga dawa asubuhi akipata oda anachuma siku hiyo hiyo anauza.
Mamlaka ya chakula na lishe ingeingia sokoni kukagua hivi vyakula ingetuepusha na magonjwa yanayoweza kuepukika.
Mfanyabiasha wa sasa anaangalia pesa na sio afya ya mlaji