TFDA ni muda sasa wa kuingia na kukagua bidhaa katika masoko ya vyakula

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mamlaka zetu nyingi zimekuwa zikifanya kazi katika mfumo ule ule wa zamani tofauti na hali halisi ya sasa.

Kwenye masoko ya vyakula hali ni hatari mno maana wananchi wengi wanalishwa sumu bila kujua,na lengo la mfanyabiasha ni kupata pesa bila kujali anaenda kumuumiza mlaji.

Juzi kuna Mama mmoja rafiki yangu ambae ni mkulima wa mboga mboga,wakati akiwa shambani anachuma mboga nikamuambia aniuzie mboga kwa ajili ya kula siku hiyo lakini alichonijibu ni kuwa "rafiki yangu hizi mboga nimepiga dawa asubuhi Yaani sumu ya kuua wadudu siwezi kukuuzia hizi maana najua ni hatari" alichoniambia nisubiri baada ya siku tatu au nne dawa itakuwa Imeisha atanichumia.

Nikisikitikia sana kwa kuwa niliona kabisa watu wanaenda kupata maradhi tofauti tofauti kutokana na ulaji wa vyakula vyenye viambata vya sumu.

Hili pia niliwahi kuona kwa wakulima wa nyanya, biringanya nk. Anapiga dawa asubuhi akipata oda anachuma siku hiyo hiyo anauza.

Mamlaka ya chakula na lishe ingeingia sokoni kukagua hivi vyakula ingetuepusha na magonjwa yanayoweza kuepukika.

Mfanyabiasha wa sasa anaangalia pesa na sio afya ya mlaji
 
Hao wa kukagua nao ni watu pia, wana njaa ya pesa pia.

Wengine wanampa mfugo chanjo na maziwa anauza huenda yanatumiwa na watoto wachanga ila hawajali, wanaangalia pesa.

Tunanunua viroba vya unga unakuta wale wadudu wakubangua mahindi wamejaa juu kwenye unga, hao tfda nao pia wapo.

Kikubwa hata wewe muuzaji uwe na roho ya kibinadamu, kitu huwezi kula wewe kwanini umuuzie mwingine.

Pesa hazijai
 
Mkuu hili ni jukumu la TBS wao ndo wamepewa mamlaka ya usimamizi wa vyakula baada ya kulinyifoa hili kwa TFDA ya zamani. Just for your information TFDA ya zamani siku hizi inaitwa TMDA na kazi yake ni madawa na vifaa tiba tuu!
Chakula kipo TBS.
 
Hakuna mamlaka inayoitwa TFDA,
Ishavunjwa kuna TMDA,madawa na vifaa tiba wapo mabibo external njia ya makuburi ,hawahusiki na vyakula.
Hao wanaohusika nakupa home work ila wapo jengo la TBS ubungo
 
Kwanza siku hizi Hakuna TFDA Kuna TMDA ambao hawahusiki na vyakula tena.

Vile vile, haya mashirika Yana Makao Makuu mwisho kwenye KANDA hayana Watumishi ngazi za chini.

Na ndio maana, baada ya chakula na vipodozi kuondolewa TFDA na kupelekwa TBS, hao TBS wakaamua kufanya kazi na Watumishi wa Halmashauri.

Ndio maana, ukiwa Afisa Afya ( Bwana Afya/ Bibi Afya ) Halmashauri inabidi wewe huyo huyo uwe TBS, OSHA, TMDA, NEMC na PP.

Ina maana, kwa suala hili Afisa Afya na Afisa Kilimo ndio wahusika lakini probably ni wachache au wamezidiwa na hivyo wanafanya wanachoweza.

Sheria ya viwango ya mwaka 2019 👇👇👇
 
Attachments

  • Polish_20220710_124530134.png
    Polish_20220710_124530134.png
    39.4 KB · Views: 9
Hakuna mamlaka inayoitwa TFDA,
Ishavunjwa kuna TMDA,madawa na vifaa tiba wapo mabibo external njia ya makuburi ,hawahusiki na vyakula.
Hao wanaohusika nakupa home work ila wapo jengo la TBS ubungo
Asante sana kwa masahihisho hayo,tunaamini wataingia kazini sasa
 
Mkuu hili ni jukumu la TBS wao ndo wamepewa mamlaka ya usimamizi wa vyakula baada ya kulinyifoa hili kwa TFDA ya zamani. Just for your information TFDA ya zamani siku hizi inaitwa TMDA na kazi yake ni madawa na vifaa tiba tuu!
Chakula kipo TBS.
Kwanza siku hizi Hakuna TFDA Kuna TMDA ambao hawahusiki na vyakula tena.

Vile vile, haya mashirika Yana Makao Makuu mwisho kwenye KANDA hayana Watumishi ngazi za chini.

Na ndio maana, baada ya chakula na vipodozi kuondolewa TFDA na kupelekwa TBS, hao TBS wakaamua kufanya kazi na Watumishi wa Halmashauri.

Ndio maana, ukiwa Afisa Afya ( Bwana Afya/ Bibi Afya ) Halmashauri inabidi wewe huyo huyo uwe TBS, OSHA, TMDA, NEMC na PP.

Ina maana, kwa suala hili Afisa Afya na Afisa Kilimo ndio wahusika lakini probably ni wachache au wamezidiwa na hivyo wanafanya wanachoweza.

Sheria ya viwango ya mwaka 2019 👇👇👇
Asante, sikufuatilia kujua kama hizi mamlaka zimebadilishwa siku za usoni. Ni vizuri pia wakidili na vyakula vinavyotoka mashambani
 
Hao wa kukagua nao ni watu pia, wana njaa ya pesa pia.

Wengine wanampa mfugo chanjo na maziwa anauza huenda yanatumiwa na watoto wachanga ila hawajali, wanaangalia pesa.

Tunanunua viroba vya unga unakuta wale wadudu wakubangua mahindi wamejaa juu kwenye unga, hao tfda nao pia wapo.

Kikubwa hata wewe muuzaji uwe na roho ya kibinadamu, kitu huwezi kula wewe kwanini umuuzie mwingine.

Pesa hazijai
Wewe comment zako mimi hoi, genye kama zote... Sijui kwa nini
 
Back
Top Bottom