Ni kweli sheria ilibadilishwa na waliobadilisha ni UEFA wenyewe hivyo ni sahihi kuwa Liverpool alienda kushiriki CL kwa ticket ya bingwa mtetezi wa CL.
Na hilo tukio la bingwa wa UCL kushindwa kufuzu kwa ticket ya msimamo wa ligi kuu ndio lilitokea kwa mara ya kwanza tangu hayo mashindano yaanzishwe mwaka 1956, hapo kabla haikuwahi kutokea bingwa wa UCL kushindwa kufuzu kucheza CL kwa tiketi ya ligi kuu. Hivyo Liverpool ndio ilikuwa ni timu ya kwanza kubeba ubingwa wa UCL huku kwenye msimamo wa ligi kuu akiwa hana vigezo vya kushiriki UCL msimu unaofuata. Hivyo waliobadilisha ni wenyewe UEFA na ikabidilishwa ili kuipa favour timu yeyote ile itakayobeba ubingwa wa UCL kuutetea ubingwa wake.
Ingekuwa hicho mnawaza nyie ndio ipo hivyo, kwanini Liverpool ambaye anauzoefu wa UCL hakupewa favour msimu huu na shirikisho la soka la Uingereza kwa maslahi ya taifa lao na ili Newcastle ambayo haina uzoefu wasishiriki?