TFF hii inaiimarisha Yanga kwa uonevu

Kwahiyo simba sc wakiwasha moto sio psychological war?
Yanga wakimwaga dawa uwanjani ni psychological war?

Duh...NDIO MAANA MNAAMBIWA HAMNA AKILI.
Simba waliadhibiwa kwa kuwasha moto uwanjani sio kwasababu ya uchawi, bali kwasababu ya kutishia kusababisha ajali ya moto kwenye mkusanyiko mkubwa kama ule kiwanjani
 
Simba waliadhibiwa kwa kuwasha moto uwanjani sio kwasababu ya uchawi, bali kwasababu ya kutishia kusababisha ajali ya moto kwenye mkusanyiko mkubwa kama ule kiwanjani
ACHENI ULOZI
 
Hahaha. We jamaa umedata aisee. Kesho tembea kinyumenyume kutoka huko chanika hadi kariakoo kuuenzi huo utamaduni wako
 
Nimekwambia fanya hivyo kuenzi utamaduni wako unaoutetea, wewe unakimbilia kusema siyo uchawi halafu unatuma video isiyohusiana na mada. Una shida gani?
Nataka kukuonyesha kuwa milango yote ya uwanjani ni ya kutoka na kuingia uwanjani kwanini lazima nipitie hapo nisipopaamini kisaikolojia? hakuna uchawi kwenye mpira bali Kuna utamaduni unaochukua nafasi ya psychologist, asipofanya hivyo kwa kupita mlango usiotakiwa atafanya kitu kingine ambacho hukioni.
 
Unasema hauamini uchawi katika mpira halafu unauliza kwanini lazima upitie hapo usipopaamini kisaikolojia? Endelea kujichanganya na kujitia aibu
 
Unasema hauamini uchawi katika mpira halafu unauliza kwanini lazima upitie hapo usipopaamini kisaikolojia? Endelea kujichanganya na kujitia aibu
tofautisha kati ya imani na uchawi. Kinjekile aliwaaminisha askari wake wapigane vita ya majimaji kwa kutumia mganga wa kienyeji "mchawi" lakini walipigika sana pamoja na "uchawi", TFF ilivyoruhusu timu kusajili wachezaji wa kigeni 12 wenye ujuzi mkubwa ni sawa badala timu kuamini kichawi kama wachezaji wabovu wanaweza kushinda mechi kwa uchawi. Inamani kama hizo zitakufa zenyewe polepole kwa timu kuwa na bajeti kubwa ya kusajili wachezaji wazuri wanaokula vizuri, kutibiwa vizuri, wanaolipwa vizuri na kufundishwa na makocha wazuri badala ya TFF kuaminisha watu kuwa kuna uchawi unaostahili kutozwa faini ya 5ml.
 
Bado unaendelea kunyooshea vidole wengine badala ya wanaohusika na kuonyesha hivyo vitendo vya kishirikina. Hautatui tatizo kwa kulikimbia au kulionea aibu bali kwa kulikabili.
 
Hii adhabu ya 5 milioni na milioni 1, inaakisi matokeo ya mchezo wenyewe.
Kila goli lililofungwa ni milioni moja.
 
Sasa ushasema tunakomazwa kimataifa afu unalalamika nn sasa, hutaki Yanga SC tukomazwe?
 
Bado unaendelea kunyooshea vidole wengine badala ya wanaohusika na kuonyesha hivyo vitendo vya kishirikina. Hautatui tatizo kwa kulikimbia au kulionea aibu bali kwa kulikabili.
Kifupi Tanzania hakuna uchawi kwenye mpira, ndio maana timu zetu ni kichwa Cha mwendawazimu tangu enzi hizo mpaka leo. Huo uchawi unaopogiwa kelele na TFF uko wapi? kama upo umeusaidia nini mpira wetu? Waache watapetape TU ilimradi wasifanye vitu vya kudhulu wengine kama vile kuwasha moto na kusababisha ajali ya moto.
 
Mkiendelea na vitendo hivyo tutaendelea kuwanyooshea vidole hadi muone aibu muachane navyo.
 
Kuna sku mtanyamaza tu siku yaja
 
Mkiendelea na vitendo hivyo tutaendelea kuwanyooshea vidole hadi muone aibu muachane navyo.
Hata uwanyonge watu hawataacha imani zao (kubaka, viungo vya watu, kukeketa, kurithi wajane, kundika miili, kuchanja chale, kuvaa hirizi, pete za bahati, nk). Ni elimu pekee ndio inaweza kuwabadilisha watu imani zao. Timu ziko tayari kutozwa faini lakini watimize imani/mila zao zilizodumu kwenye jamii kwa karne na karne. Wewe mpuuzi mmoja huwezi kuwageuza watu waachane na mila zao kwa adhabu, utaondoka wewe na kuwaacha wao vilevile na tamaduni zao. Yaani TFF wanachofanya kwenye hili ni kitu kitaalamu tunakiita acculturation, ethnocentrism na stereotyping. Yaani wewe Karia umwambie mzee Mpili, Kilomoni, Aden Rage, Kaduguda au Mangungu asifanye tumba kwenye mechi, who are you? Watafanya watafanya watafanya tu hata ikibidi wakutoe kafara wewe. Mambo hayo yatapungua yenyewe kadri elimu kwa kizazi kipya itakapokolea polepole na kuanza kukumbatia sayansi na misingi ya football. Hata wazungu wana "uchawi" wao kwenye mambo yao mbalimbali. Mfano, pamoja na kuenea kwa demokrasia barani ulaya lakini Uingereza kuna ukoo mmoja tu wa kifalme unaotawala uingereza. Uko huu ni wachawi walioifanya Uingereza itawale dunia na inayowashindia vita. Acheni upuuzi wenu na ushamba wa rejareja.

Hakuna timu tanzania na Afrika isiyofahamu kuwa Karia ni Simba na hakuna timu isiyofahamu kuwa Simba inaroga sana kwenye mechi zake kuliko timu nyingine. Kwahiyo, TFF kutaka kulazimisha Yanga na timu nyingine zipite pale wanapotaka zipite ni kuisaidia Simba kushinda mechi, hiyo ndiyo tafsiri ya timu zote za nchi hii. Simba wamekamatwa live wakiroga kule Afrika Kusini kwenye uwanja wa watu, sasa hebu fikiria kama waliweza kuroga kwenye uwanja wa South Africa watashindwaje kuroga kwenye uwanja wa Tanzania? Acheni upuuzi wenu., chezeni mpira.
 
Yanga hili suala la kuingilia mlango usio rasmi inabidi wapigwe fine ya Mabilioni ndio watakoma, kila siku nyie khaa.
Hivi Champion League wataingia kwa mlango usio rasmi wakiwa ugenini?
 
Hivi Champion League wataingia kwa mlango usio rasmi wakiwa ugenini?
Akili hamna, hata mmasai haingii na sime yake kwenye ndege, havai shuka ya lubega akiwa Ulaya na Marekani, na huko champions league hakuna uchawi kama wa Simba hapa kwenye ligi yetu, hivyo timu haihitaji kuingia uwanjani kwa kupitia mlango mwingine na Wala mashindano ya champions hayana kanuni za kupitia mlango mwingine Wala uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…