TFF inadhalilisha wabia wake katika kuendesha mpira wa miguu nchini kutokana na chuki za watendaji wakuu wa TFF kwa Yanga. Waamuzi kuboronga mechi, kuahirishwa derby na kuchukua juu kwa juu fedha ya CRDB iliyokusudiwa kwenda Yanga kama bingwa wa mashindano ni ushahidi wa hili.
TFF imekosea sana tena sana kuzuia fedha za ubingwa kwakuwa TFF Ina njia nyingi nyingine za kudai madeni yake kutoka kwenye vilabu vyake.
Kwanini CRDB hailipi bingwa wa mashindano ya CRDB Moja kwa moja kwenye account ya Bingwa?
TFF Hawa hawana weledi, wanaendeshwa na upepo wa Simba na Yanga. Tabia hii sio rafiki kwa wadhamini wao.
Kihasibu mapato yote lazima yasome kwenye accounts za taasisi kisha ndio yatoke kwenda kufanya malipo, na hapo ndio reconciliation inaweza kufanyika kwa urahisi.