TFF kilichoshindikana kwa Tuisila Kisinda kiliwezekana kwa Perfect Chikwende (double standard)

TFF kilichoshindikana kwa Tuisila Kisinda kiliwezekana kwa Perfect Chikwende (double standard)

Wewe mpumbavu unajua ITC inaombwa na chama cha soka nchi husika,kwanini tff waliridhia kumuombea ITC kisinda kutoka berkane then leo wageuke,na ikiwa kambole hajapeleka malalamiko yoyote tff?
Mpumbavu mwenyewe makosa ya viongozi wenu kujifanya wajuaji mnatukana ovyo. Nendeni CAS kama mnaona mumeonewa. Bwege mtozeni wewe. Mnafikiri kutumia lugha chafu ndiyo mnapata suluhu?
 
Wewe mpumbavu unajua ITC inaombwa na chama cha soka nchi husika,kwanini tff waliridhia kumuombea ITC kisinda kutoka berkane then leo wageuke,na ikiwa kambole hajapeleka malalamiko yoyote tff?
Hata jimmy ukonde aliombewa itc akaishia kucheza cecafa,yacouba anayo itc inatumika avic town hata leo ukiomba itc 5 tff
wanakushughulikia tu
suala kwamba mmeleta mtu aangalie tv au kujaza choo hayawahusu
Ila ukitaka aingizwe kwenye system mwisho ni wachezaji 12 kwa foreigners
 
1. Nataka ieleweke kuwa hakuna hakuna kitu kimefanyika nje ya system siku hizi haiwezekani hilo kabisa.

2. System zote TMS, FIFA Connect zinapokea mchezaji aliyeombewa usajili, suala la Idadi ni matakwa ya nchi husika katika ligi yake.

3. Baada ya Kuomba ni suala la TFF kutoa APPROVE kulingana na hitaji lenyewe.

4. Yanga wameomba katika System kuhusu Kisinda kama ilivyo mtu mwingine yeyote anaweza kuomba na halina Idadi hata 100 unaweza kuomba.

5. Baada ya kuomba TFF hawawezi ku APPROVE Jina la Kisinda sababu tayari Yanga walishaomba kabla na kupewa APPROVE katika Majina 12 kulingana na kanuni zilivyo na kutoa Leseni hivyo Automatically haiwezekani kupata APPROVE ya 13.

6. YANGA Baada ya Kukosa APPROVE toka TFF katika TMS System ndio wakaandika Barua kwenda TFF kuomba ufafanuzi kuhusu suala hilo.

7. TFF wamejibu Barua ya Yanga ya kuombwa ufafanuzi tu ndio maana kuna barua.

8. Kuhusu ITC hili ni suala tofauti kabisa haiuhusiani na usajili, kuomba ITC unaweza kuomba kama Club kupitia TFF kwa wachezaji hata 50 ni kwa mujibu wa mikataba yako tu Mfano TP Mazembe au Mamelod ina Foreigners wengi sana wenye ITC ila hawapo katika usajili hapa Nchini Yanga msimu uliopita ilipata ITC ya mchezaji Toka Mozambique anaitwa Jimmy Ukonde na alicheza mechi za majaribio ila hawakumuombea Usajili pia sasa Yanga ina Yacouba ana ITC ila hayupo katika Usajili ni vitu Tofauti kabisa ITC na Usajili bali ili uweze kupata Usajili kwa mchezaji anaetoka nje lazima uwe na ITC ndio aweze kucheza.

Hivyo kuomba ITC ni jambo moja na kuomba usajili ni jambo lingine.

9. Katika Usajili wowote ule lazima uweke na Medical Examinations Report ndip unapata Leseni ina maana mwanzo Yanga walidanganya?

10. Yanga Kumtumia au kutomtumia mchezaji ni uamuzi wa kufuata Taratibu tu kama wangeweza kufanya Transfer ya mchezaji baada ya kuombwa na Timu ingine siku hiyo hiyo na baadae kuomba usajili wa Kisinda ina maana wangeweza kuwa na Logic kidogo ya kusikilizwa katika Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji wao Wameomba wakati tayari wanajua Hawawezi kuwa APPROVE.

TUFUATE TARATIBU
 
Mpumbavu mwenyewe makosa ya viongozi wenu kujifanya wajuaji mnatukana ovyo. Nendeni CAS kama mnaona mumeonewa. Bwege mtozeni wewe. Mnafikiri kutumia lugha chafu ndiyo mnapata suluhu?
We fala si ndio ulianza kuniquote kwa kuniita mpumbavu,unaonekana uko full stress
 
Wabongo mnajifanya wajuaji sana, unadhani Yanga ni wajinga kupeleka majina bila kuainisha wepi ni wa ligi ya wandani na wepi ni ligi ya nje.

Taarifa ya Kisinda ilitumwa kwa barua ya maelezo
Weka hapa hiyo barua ili utetezi uwe na nguvu. Kama barua hauna, basi weka hapa matamshi ya kiongozi yeyote wa Yanga aliyesema kwamba walikata jina la mchezaji fulani
 
Sio kweli kanuni za caf ziko wazi,unaweza kuoeleka hata majina 40 ya wacheza
Sasa bila kueleza nani atacheza ligi ya ndani tu na nani atacheza na ya CAF, TFF itajuaje? Uamuzi rahisi si ni kukata aliye chini?
 
Swali linakuja kwanini Kahata jina lake lilikatwa kwenye ligi ya ndani!? Au kwanini Chikwende hakusajiliwa kucheza mechi za kimataifa!?
Kwa hiyo Yanga wamekata jina la kambole? Kambole atacheza ligi ya ndani, TK kimataifa? Au TK atacheza ligi na kimataifa, kama atacheza ligi Ya ndani na kimataifa hamuoni ni mifano tofauti na issue ya kahata? Kwa hiyo kambole atabakia Yanga kama mfanyakaz au mchezaji hapo lazma kambole aende timu nyingine kuachia nafas. Tusiwe na ubishi usio na maana
 
Kwa hiyo Yanga wamekata jina la kambole? Kambole atacheza ligi ya ndani, TK kimataifa? Au TK atacheza ligi na kimataifa, kama atacheza ligi Ya ndani na kimataifa hamuoni ni mifano tofauti na issue ya kahata? Kwa hiyo kambole atabakia Yanga kama mfanyakaz au mchezaji hapo lazma kambole aende timu nyingine kuachia nafas. Tusiwe na ubishi usio na maana
Ni rahisi kumfundisha ng'ombe kukokotoa hesabu za milinganyo atakuelewa mapema kuliko kumfundisha mwanayanga hesabu ya 2+2 Maana jibu atakwambia ni 22.

Mliojipa Kazi ya kuwaelewesha hao jamaa endeleeni lakini mi najua mwishowe mtanyoosha mikono juu na kujisalimisha. Kazi kwenu.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Case yako uliyorefer sidhani kama bado utakuwa sahihi ukiitumia leo, wakati wa usajili wa Chikwende CAF walitoa nafasi timu zisajili tena hasa zile zilizokuwa champions league kutokana na tatizo la uviko ili ikitokea baadhi ya wachezaji wana maambukizi timu zisiathirike wawepo wengine wa kucheza

Sasa hiyo kanuni bado ipo pamoja na kupungua kwa maambukizi ya uviko kama bado ipo utakuwa sahihi mkuu
Kilaza huyo. ACHANA NAYE
 
Case yako uliyorefer sidhani kama bado utakuwa sahihi ukiitumia leo, wakati wa usajili wa Chikwende CAF walitoa nafasi timu zisajili tena hasa zile zilizokuwa champions league kutokana na tatizo la uviko ili ikitokea baadhi ya wachezaji wana maambukizi timu zisiathirike wawepo wengine wa kucheza

Sasa hiyo kanuni bado ipo pamoja na kupungua kwa maambukizi ya uviko kama bado ipo utakuwa sahihi mkuu
Kwani Uviko imekwisha mkuu?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mchezaji ambae amepata APPROVE ya TFF na kupewa Leseni anaweza kucheza Ligi ya Ndani Wakati Mchezaji ambae Ana Leseni ya CAF anacheza Ligi zote yaani Ya ndani na Caf kwa Maana ni Lazima kuwa na Leseni ya TFF katika Usajili wa CAF.

Na ukishakuwa na Leseni ya CAF na Dirisha la Usajili kubwa la CAF likawa limefungwa huwezi kutoa Jina lolote katika List zaidi ya kuongeza iwapo hujatimiza Idadi hitajishi ya usajili na haipaswi kuzidi wachezaji 7 tu. Na ieleweke Wazi Kwa Wachezaji wa Kigeni ili kupata Leseni ya TFF ni lazima CLUB kutozidisha Wachezaji zaidi 12.

Kipindi cha mpito cha usajili kinachokuwepo baada ya Dirisha kubwa la CAF kufungwa ni kwa ajili ya kuongeza tu sio vinginevyo ndio maana unaambiwa mchezaji atacheza hatua inayofuata hii ina kupa picha kuwa tayari usajili wa msingi ulishafanyika kabla.

Kwa Mantiki hiyohiyo huwezi kutoa au kufuta Leseni ya TFF pekeyake bila kufanya hivyo hivyo katika Leseni ya CAF, Sasa Kama muda wa kufanya hivyo kwa CAF umeshapita basi pia huwezi kuondoa kwa TFF itabaki kama ilivyo.

Ili kuweza kufanya mabadiliko inapaswa kusubiria Dirisha la CAF liwe wazi wakati mwingine na uweze kufanya Transfer au Kuvunja/kusitisha mkataba au makubaliano maalum yanayomshirikisha Mchezaji husika kwa maandishi.

Itambulike kuwa kuomba ITC ya mchezaji ni jukumu la Shirikisho kwa niaba ya Club na pia ITC ni moja ya Kigezo katika kupata Leseni ya TFF/CAF ila kuwa na ITC sio usajili unaweza kuwa/kupata ITC na usifanyiwe/kuombewa usajili na Club yako mifano ipo mingi Mfano ni Yacouba anayo ITC ila hajaombewa usajili na Club yake hivyo hana Leseni ya kucheza yeyote msimu huu bali bado ana mkataba na Club yake.

PLAY FAIR, BE POSITIVE
 
Weka hapa hiyo barua ili utetezi uwe na nguvu. Kama barua hauna, basi weka hapa matamshi ya kiongozi yeyote wa Yanga aliyesema kwamba walikata jina la mchezaji fulani
𝗞𝗔𝗠𝗔𝗧𝗜 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗘𝗥𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗔𝗠𝗨𝗔 𝗛𝗔𝗥𝗔𝗞𝗔 𝗛𝗔𝗧𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗦𝗜𝗡𝗗𝗔

Kaimu mtendaji mkuu wa Yanga Simon Patriotic amesema wamekamilisha usajili wa Winga Tuisila Kisinda kabla ya dirisha la usajili kufungwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF liliwasaidia kupata ITC yake ndani ya muda

Patrick amebainisha kuwa baada ya kukamilisha usajili wa Kisinda waliiandikia barua kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuomba kuomba kuliondoa jina la Lazarus Kambole katika orodha ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga kwaajili ya michuano ya ndani na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda

Yanga ilichukua hatua hiyo baada ya uchunguzi wa kitabibu kubaini kuwa Kambole amepata majeraha ambayo yanaweza kumuweka nje kwa muda mrefu

Patrick amesema kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inayo mamlaka ya kufuta leseni ya muda iliyotolewa kwa Kambole ili kupata leseni ya Kisinda hivyo wanasubiri maamuzi ya kamati hiyo ambayo ilitarajiwa kukutana jana
 
Wewe naye unapotosha, CAF wanaruhusu hadi wachezaji 40, ndio wasajiriwe ili kutumike kwenye mashindano yao, lakini kila shirikisho la nchi lina kanuni zake, za idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kusajiriwa , ndii maana kuna nchi wanaruhusu 5, na sisi hapa ni 12.madamu wasizidi 40, hata tukisema hakuna mchezaji wa kigeni anaruhusiwa hapa nchini, sio kosa.
Sasa mbona unaongea kile kile alicho sema jamaa
 
Caf inaruhusu wachezaji 40 lkn hao wachezaji ni lazima wawe na leseni ya shirikisho husika. Sasa hapa kwetu tff hawatoi leseni kwa wachezaji wakigeni zaidi ya 12 kwa tim moja. Maana yake ni kwamba simba inaruhusiwa na caf kupeleka wachezaji 40 bila kujali mataifa yao lkn kwanza ni lazima wasajiliwe na wapewe leseni ya tff ndipo wapewe leseni ya caf. Kama simba itakuwa na wachezaji 13 wa kigeni na 27 wa ndani jumla 40 ina maana kwa kanuni za tff mchezaji mmoja wa kigeni kati ya hao 13 hatopewa leseni na tff na hivyo hatopata leseni ya caf! Kwa jumla ya wataopata leseni za tff ni 39 na ndio watakaopata leseni za caf mmoja atakosa ambaye ni wa kigeni. Na atakosa licha ya ukweli kwamba timu haijazidi kiwango cha wachezaji wanaoruhusiwa na caf (40)

Issue ilivyo kwa yanga. Inasemeka yanga walitoa maelekezo kwa tff wakate jina la kambole waweke jina la kisinda. Tatizo ni kwamba tff walikuwa washatunza usajili wa kambole kwa hiyo kambole ndio mwenye leseni ya tff na ndie atayepata leseni ya caf. Kisinda mlichelewa
Dohhh mambo yanafanyika ki digital now amna tena mamno ya mibarua ilikuwa ni kitendo cha ku click button tu kwenye server kambole out kisinda in na kazi ingeishia apo apo simple tu ..sema kwakuwa wana ajenda zao binafsi na yanga ndio mahana
 
Back
Top Bottom