TFF Kuchunguzwa na FIFA Migogoro ya Kiuongozi

TFF Kuchunguzwa na FIFA Migogoro ya Kiuongozi

Wale jamaa zetu ikija TFF iliyo nyooka sijui wataishi vp maana timu yao bila maelekezo ya marefa hawatoboi
 
Huenda ikasaidia watu wakajitambua na wakaanza kuhoji mambo ya maana ya mustakabali wa nchi kwani sasa hivi CCM imewekeza kwenye Simba na Yanga kuwapumbaza watanzania wabakie kubishania ushabiki wa mpira huku wenyewe watawala wakiendelea kujipakulia minyama ya keki ya Taifa wao na familia zao.
Mkitoka huko mtahamia kwenye bongo fleva mtasema watanzania wanawafuatilia sana wakina Diamond na Ali kiba kuliko kujadili siasa.
 
Mkitoka huko mtahamia kwenye bongo fleva mtasema watanzania wanawafuatilia sana wakina Diamond na Ali kiba kuliko kujadili siasa.
Umepewa kandarasi ya kunifuatilia nini? Naona unanipalatia palatia kama changudoa aliyekosa danga. Karibu
 
Umepewa kandarasi ya kunifuatilia nini? Naona unanipalatia palatia kama changudoa aliyekosa danga. Karibu
Unaweza kutaja idadi ya comments zako nilizo reply jana na leo ili tuone kwa kiwango gani nakufuatilia mkuu?
 
[Jina lako]
[Anwani yako kamili]
[Simu: +255 XXX XXX XXX]
[Barua Pepe: [email protected]]
Tarehe: [Weka tarehe ya leo]

Kwa:
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA)
Fédération Internationale de Football Association (FIFA)
FIFA-Strasse 20,
P.O. Box 8044 Zurich,
Switzerland.

YAH: MAOMBI YA UCHUNGUZI DHIDI YA TFF KUHUSU MINGILIANO YA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA MASUALA YA MPIRA

Mheshimiwa Rais wa FIFA,

Napenda kuchukua fursa hii kukuandikia kwa heshima kubwa, nikiwa kama raia wa Tanzania na mpenzi wa soka, kwa lengo la kuomba Shirikisho lako tukufu lifanye uchunguzi huru na wa kina dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuhusu kile kinachoonekana kama mingiliano ya moja kwa moja ya serikali ya Tanzania katika masuala ya ndani ya soka.

Kwa mujibu wa kanuni na katiba ya FIFA, mashirikisho ya soka yanatakiwa kuwa huru bila kuingiliwa na mamlaka ya serikali. Hata hivyo, hali nchini Tanzania hivi karibuni imeonyesha tofauti kubwa na miongozo hii.

Mfano halisi ni mgogoro uliotokea kwenye mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya klabu ya Yanga SC na Simba SC, ambao uliibua mvutano mkubwa wa kiuendeshaji, na hatimaye, uongozi wa vilabu hivyo uliitwa ikulu (ofisi ya rais) kwa ajili ya kusuluhishwa, badala ya suala hilo kushughulikiwa na vyombo vya ndani vya mpira kama TFF au kamati husika.

Aidha, mgogoro wa usajili wa mchezaji Feisal Salum "Fei Toto" ambaye alihamia klabu nyingine huku kukiwa na utata wa kimkataba, pia ulimalizwa kupitia uingiliaji wa moja kwa moja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala ya kufuata taratibu za kitaaluma na kitaasisi zinazopaswa kuendeshwa na TFF au FIFA kupitia Kamati ya Usuluhishi wa Migogoro ya Usajili.

Matukio haya yanaashiria wazi kuwa uhuru wa TFF katika kuendesha soka nchini Tanzania umeathiriwa, na vyombo vya serikali vinaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika maamuzi ambayo kimsingi yanapaswa kuwa ya kitaalamu, huru na yanayozingatia katiba ya FIFA.

Kwa misingi hiyo, naomba FIFA ifuatilie na kuchunguza hali hii kwa ukaribu, ili kulinda uhuru wa shirikisho letu la mpira na kuhakikisha soka linaendeshwa kwa kufuata misingi ya haki, sheria, na miongozo ya kimataifa.

Tuna matumaini makubwa kuwa FIFA haitasita kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuwa kuna ukiukwaji wa misingi ya utawala bora wa michezo.

Nashukuru kwa muda wako na kwa uongozi wako wa haki kwa maendeleo ya soka duniani.

Wako kwa dhati,
[Jina lako kamili]
[Mashabiki/Mpenzi wa Soka Tanzania]
 
Ikiwapendeza FIFA wafunge kabisa mambo ya mpira TANZANIA kwa miaka 10 hivi
Acha upuuzi wewe; unataka tufungiwe mpira halafu tushabaikie nini. Wote tuwe machawa wa mitano tena?
 
Wafungiwe tu ili kwanza akili itulie sehemu Moja Uyanga na Usimba ututoke
 
Back
Top Bottom