TFF Kuchunguzwa na FIFA Migogoro ya Kiuongozi

Wafunge tu, unajua SERIKALI, TFF, SIMBA& YANGA wamesababisha hasara mara ngapi kwa sisi mashabiki wa mpira?
 
Mababu 24)7 unawaza Simba Yanga? Huu hatari iliyopo mbeleni kama hii habari itakua na ukweli?
 
Ikiwapendeza FIFA wafunge kabisa mambo ya mpira TANZANIA kwa miaka 10 hivi
Ili tuwe tunaongelea kuhusu CCM ama mjadala ya kiuchumi

Swali fikirishi je kama huo muda ambao watanzania wanautumia kubishana kuhusu yanga na Simba kama ukatumika kubishana kuhusu maendeleo binafsi na Kwa jamii zetu hapo vipi
 
Itakuwaje kama itagundulika kuwa chanzo cha migogoro ndani ya TFF ni serikali tutakwepa kufungiwa?
Ingawaje interference ipo lakini sioni serious institutional interference bali kilichopo interference inayotokana na ushabiki wa viongozi! Aina hii ya inteference inakuwa haina ushahidi wa kuadhibu nchi lakini inaweza kuwa na athari kubwa kwa Viongozi wa TFF wenyewe! Kama taarifa hii ni ya kweli basi walio kwenye risk ni akina Karia, na wanaweza hata akufungiwa kujihusisha na soka!

Ile ya SSH majuzi watu tunaikuza tu unless kuwe na ushahidi kwamba SSH alilazimisha TFF kubadili ratiba! Kinyume chake, itaonekana tu Kiongozi wa Nchi alichofanya ni kusuluhisha mgogoro uliokuwa unatishia mechi #184 kutochezwa kabisa lakini sio kwamba ALITOA AMRI kwa TFF kwamba Mechi isogezwe mbele!
 
Kwa uelewa wangu Rais alifanya kitu sahihi japo alichelewa kidogo lakini kuchelewa huko ndiyo usahihi wenyewe kwasababu mtifuano utaonekana kwenye picha mjongeo za wadau na Viongozi wa mpira wakiwemo wasemaji wa yanga na simba na mtifuano wa TFF na yanga kuhusu malipo ya CRDB confederation cup bira kusahau taarifa kwa umma za Simba, yanga na TFF

Rais alifanya kitu kinaitwa 'arbitration,' yaani usuluhishi, (upatanishi) ambao ulizaa matunda mimi binafsi nampongeza kwa hilo

Hakuingilia mchezo alihamasisha mchezo uchezwa na Ndiyo maana TFF wametangaza mchezo tarehe 25-06-2025

Hitimisho

Vilabu vya Simba SC na Yanga SC kazi yao ni kucheza mpira bodi ya ligi msimu huu wamejichanganya wazi wazi kushindwa kuzisimamia kanuni za mpira kikamilifu kwasababu wanazo zijua wenyewe .

Tanzania premier league board failed to effectively manage foot regulations, for the reasons best know by themselves
 
Upo sahihi kwa 100%, kwa sababu nami ndivyo uelewa wangu upo hivyo!
 
Kama hii habari ni ya kweli basi Simba mnaenda kumchoma mshikaji wenu wa TFF. Hii si habari nzuri kwa viongozi wa mpira bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…