kwanza nichukue fusa hii nikiwa mdau wa ball kupitia jukwaa hili la michezo la jamii forum kuzipongeza timu kutoka championship na kupanda ligi kuu.
KENGOLD FC NA PAMBA FC, Hakika timu hizi zinastahili pongezi maana siyo kazi nyepesi kutoka championship mpaka kupanda ligi kuu
Na pia nichukue fursa hii kuwashauri (kuwasihi) ndugu KENGOLD FC NA PAMBA FC kuwa ligi kuu ya NBCPL haitaki mbwenbwe za huko mlikotoka bali ligi kuu inahitaji NIDHAMU, UONGOZI BORA, USAJILI MZURI NA BENCHI MAKINI, ligi kuu haitaki mambo ya kuchinja paka, kuchimba chimba uwanja bali ni usajili mzuri na kuwapa morali wachezaji.
Turudi kwenye kichwa cha habari kama kinavyojieleza hapo juu ligi yetu imekua inakipengele cha play off, timu nne za mwanzo katika ligi ya championship timu mbili hupita moja kwa moja lakini mbili zilizobaki hucheza play off bingwa anakwenda kucheza na timu moja wapo ya ligi kuu iliyocheza play off na mwenzie nje ndani na kushinda
HOJA YANGU; timu za ligi kuu zinakua tayali zinauzoefu msuli wa usajili pamoja msuli wa fedha tofauti na championship wanakua ni wa kuunga unga sasa ukiwakutanisha kwenye playoff kwa asilimia kubwa timu inayotoka championship lazima itapigwa tu na timu kutoka ligi kuu itarudi tena wa championship atarudi alikotoka
MAONI YANGU; TFF na Bodi ya ligi inapaswa waliangalie hii sheria hii wa championship wamalizane wao kwa wao a wa ligi kuu pia wamalizane wao kwa wao kuliko wa championship kukutana na wa ligi kuu hhiyo ni ngumu na kwa upande mwingine ni uonevu tu