TFF na Bodi ya ligi inapaswa kubadili sheria ya timu ya ligi kuu kucheza play off na timu ya championship

Sasa kama unapigwa na kibonde wa ligi kuu unapanda kwenda kufanya nini? ibaki hivyo hivyo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mob

misimu karibu miwili au mitatu timu inacheza play off ni Dhahiri hii timu inabebwa kwa kua ni wakongwe na ndiyo maana slogani yao kubwa watanzania wawaombee eti wana hali mbaya
 
hivi umenielewa nilichokiandika hapo juu

Nimekuelewa mkuu, niliomba data lakini ukanirudishia jukumu hilo na mimi nimetekeleza. Katika timu 8 za ligi kuu zilizocheza playoffs katika misimu 4, ni timu 3 tu zilizoweza kubaki na 5 zilishindwa na timu za championship.

Tena mwenyewe umekumbuka jinsi Mbeya City walivyofanyiwa uhuni, sasa kwa uzoefu wao wa ligi kuu si ungewasaidia kushinda uhuni wa Mashujaa?
 
Kwani shida ni nini? TFF inaweza kusema kupanda wawili na kushuka wawili basi. Wameweka playoff kumpa nafasi mwingine naye ajaribu bahati. Bundesliga wanacheza playoff, unataka kusema nao ni wajinga.
 
Wangefanya kama waingereza wanavyofanya, kinaumana nyie kwa nyie na wa kushuka anakuwa kishashuka. Huku kwetu sasa mtu alitakiwa kushuka anachezeshwa play off na mwenzie akishinda anabaki Ligi Kuu na aliyefungwa anacheza tena play off na mshindi toka play off ya championship-ujinga mtupu.
 
Germany,France na Belgium wanatumia kanuni hii kwenye ligi zao.
Ni vyema kutafuta maarifa kabla ya kuandika chochote hapa jukwaani.
 
Kweli mkuu
 
Germany,France na Belgium wanatumia kanuni hii kwenye ligi zao.
Ni vyema kutafuta maarifa kabla ya kuandika chochote hapa jukwaani.
UINGEREZA WANATUMIA IPI LIGI YA UINGEREZA NI BORA SANA HAPA DUNIANI KWANI WAO WAJINGA?!

FIKIRI MARA MBILI KABLA YA KUANDIKA HUO UPUUZI WAKO.
 
Una hoja nzuri sana. Sasa unachukua nafasi; unaipeleka wapi?? Kumbuka haichukuliki hiyo. Sema .......NATAKA NITUMIE NAFASI HII ......
 
Hakuna timu ya Championship iliyowahi toboa kwenye play off kwa miaka hiyo 3
 
Kila kitu kina faida na Hasara...

Faida
  • Kuongeza amsha amsha katika mashindano ya championship timu zinakuwa na kitu cha ku-play for mpaka game ya mwisho bila ya hivyo mbili zikishajulikana watu wataanza kuchukua mlungula mapema na kuuza mechi

Hasara
  • Sioni hasara kama wewe umetoka championship na unashindwa kuwafunga vibonde wa premier league maybe you do not afford to be there..., bola vibonde katika vibonde kuliko vibonde zaidi ya vibonde...
Thus all for play-off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…