TFF na Bodi ya Ligi wapo kimkakati zaidi katika upangaji wa ratiba

Huu uzi hausiani na mapungufu ya waamuzi. Bali ni uzi unahusu chombo kinachosimamia ligi na kinachosimamia mpira wa miguu Tanzania kwa kuifanya timu moja iwege nyuma kwa idadi ya mechi na huku aliyejuu yake waendeleege tu kucheza mechi.
Na mimi naweka malalamiko yangu hapa ili wahusika wafanyie kazi
Hii nayo ni offside
 
Karia anajulikana ni mnazi wa simba na coastal union
Tujue wasifu wa makamu waje , katibu na ceo .
 
We ni thimba kolowizard og. Maana hata iweje kolo ni mbishi grade one! Ananyolewa na Ambangula ila bado yumo tu anashupaza tu shingo! Ambangula kaharibu kabisa mfumo wa kufikiri wa makolo! Hasira za makolo Sasa zipo kwenye mataulo ya makipa wa timu pinzani!

Sasa msumari wa mwisho na mazishi ya huu ujinga wa kuibeba thimba kwa viporo ni mechi yetu ya derby, tutawakanda na kufikisha lile gepu tunalopenda la points kumi!

Angalau sasa kidogo afadhali marefa wamepunguza kuibeba kolowizard maana ilikuwa inachefua kucheki mechi za Simba wanaopewa penati kama pipi
 
Ukiwa unajua mpira utaona ukichoandika ni ujinga.

Hivi kati ya Jamuhuri na Manungu kipi kiwanja kibovu?

Simba imecheza Manungu na kupata alama 3 kwenye kiwanja kibovu kwanini sababu ya kupoteza mechi iwe ni uwanja?

Nakukumbusha kwamba mechi ya juzi tumecheza na JKT kwenye uwanja wao mpya ambao sio mzuri na bado tulipata matokeo

Katika mechi ambazo Simba amecheza mkoani asilimia 90 zote ameshinda.

Pointi alizodondisha nyingi zote kazipotezea nyumbani

Sare na Namungo ilikuwa ni Uhuru pale tayari tumepoteza pointi 2

Sare na KMC tena kwenye uwanja wa Chamazi unaoutaja taja.

Ungekuwa umeangalia mechi usingetaja sababu ya uwanja.

Makosa personal ya wachezaji hayawezi kufanya sababu iwe ni uwanja.

Nafasi ngapi tulitengeneza za kufunga lakini poor marking za forward yetu ndio iliyokuja kutuhukumu.

Plus Manura anakosaje lawama kwenye yale magoli? Au ulitaka lawama iende kwa uwanja?

Jifunze kuujua mpira na sometimes kukubali kushindwa ni moja ya fairness ya kumheshimu mpinzani.
 
Azam amecheza michezo 20 wewe umecheza michezo 19

Unaelewa maana yake?

Maana yake Azam angekuwa ni mtu wakutafuta huruma angeanza kulia kuwa wewe unapendelewa.

Unakumbuka ule muda ambao Azam alikuwa anaongoza ligi kutokana na kucheza michezo mingi?

Lini uliwahi kujitokeza hadharani kukemea TFF kwa kitendo cha kuiachia Yanga na Simba viporo?

Gape la mechi ambalo lipo kati yako na mimi ni mechi moja tu na hiyo ilitokana na AFL kuingilia ratiba ndio maana unaona gape hilo.

Sasa niambie wewe gape lako na Azam kwenye utofauti wa mechi moja limetokana na nini?

Hoja ni kwamba kuna ugumu gani unaofanya Yanga ishindwe kushinda hiyo mechi kisa tu Simba ina kiporo?


Kwasababu hata wakati juzi mnacheza na Ihefu bado ratiba ilikuwa ni ileile ya Simba kuwa na kiporo, na bado mkashinda na hakukuwa na kelele za Simba kwanini ana kiporo.

Leo umeona unacheza na Azam ambao ni wagumu umeanza kulia lia kutafuta sababu, ni uoga tu.
 
Hujaelewa na hutaelewa kwasababu uko kishabiki zaidi.
Kwa nini koporo cha Yanga vs JKT na Simba vs Mtibwa kisimalizwe kwanza Machi 17 na 18 mtawalia?
Je hapo pana sababu ya kuvitunza viporo vya namna hiyo?
Unaelewa JKT na Mtibwa wakicheza hizo mechi watakuwa wamecheza mzunguko wangapi?

Unaelewa sababu yako ya kutafuta fairness kwa Yanga inaenda kuzikandamiza timu zingine kwa sababu zile zile ulizokuwa unazilalalmikia wewe?
 
This is well known . Time table ya league 23/24 ipo designed to favor SIMBA in all aspect . Sijui lini this non sense will stop [emoji706] . Allow AZAM or coastal to be favorable . Not the big 2
Akili za viazi mbatata hizi!
 
Kumbe mlifungwa kwa makosa ya personal, kwanini hapo juu ulilalamikia fixture mgumu ndio iliyochangia kwa timu ya Simba kupoteza mechi. Tusimame na fixture au tusimame na makosa personal?
 
Mwaka jana wakati mko shirikisho viporo vilidandiana hampigi kelele,mkiona simba wana viporo mnaanza kupiga kelele kama manesi wa zamu
 
U
Upo kishabiki sana, kwahiyo hapa kinacholalamikiwa hakimjumuishi na uonevu anaofanyiwa Azam? Kwanini Azam unamtoa wakati ni mmoja wa waathirika katika hili ambapo mimi nipo kumuongelea pia? Kwanini umekaa kiusimba na uyanga pekee badala ya kukaa kiunamichezo?
Unazungumzia AFL je imeisha lini au bado inaendelea? Kwanini baada ya kuisha mechi za AFCON kwanini Simba na Yanga wacheze idadi sawa ya mechi ilihali mmoja kamzidi mwenzie michezo?
Kwanini baada ya kuisha michezo ya klabu bingwa ipangwe ratiba kwa kurudia kosa hilo hilo la kuwapa idadi sawa ya mechi Simba na Yanga wakati Simba ndiye aliyekuwa nyuma kwa mechi moja.
 
Kumbe mlifungwa kwa makosa ya personal, kwanini hapo juu ulilalamikia fixture mgumu ndio iliyochangia kwa timu ya Simba kupoteza mechi. Tusimame na fixture au tusimame na makosa personal?
Mechi ngumu kwa sababu mechi za Simba zilifululiza na bado hapo ilitakiwa kuwe na kiporo ili kupunzisha wachezaji
 
Mbona hiyo ratiba unayoongelea ilikuwa ni sawa kwa Yanga mzee,
Wote wanapumzika siku sawa sawa. Simba tarehe 6 yanga tarehe 8 baada ya hapo tarehe 9 Simba na tarehe 11 Yanga. Wote wamekuwa wakipumzika siku mbili ya tatu mechi. Au point yako ni ipi hapo?
 
Wewe unaongelea Yanga siyo Azam ndo maana mada haina jina la Azam, hata Simba angekuwa mbele mchezo mmoja bado ungelalamika tu maana ni nature ya utopolo
 
Mechi ngumu kwa sababu mechi za Simba zilifululiza na bado hapo ilitakiwa kuwe na kiporo ili kupunzisha wachezaji
Wote wamefululiza.
Ratiba ya Simba ilikuwa tarehe 6, 9, 12,15
Huku Yanga ilikuwa ni tarehe 8,11,14,17 sasa kuna tofauti gani hapo katika kufululiza mechi kwa Yanga?
Hoja ya msingi mnaikwepa, kwanini Azam acheze na Yanga tarehe 17 wakati kwanza ligi inasimama kwenda mapumziko na kalenda ya FIFA?
2) kwanini wakati Simba atakuwa anaendelezewa mzigo wa viporo?
 
Wewe unaongelea Yanga siyo Azam ndo maana mada haina jina la Azam, hata Simba angekuwa mbele mchezo mmoja bado ungelalamika tu maana ni nature ya utopolo
Je umeona mada ina jina la Yanga?
 
Unaelewa JKT na Mtibwa wakicheza hizo mechi watakuwa wamecheza mzunguko wangapi?

Unaelewa sababu yako ya kutafuta fairness kwa Yanga inaenda kuzikandamiza timu zingine kwa sababu zile zile ulizokuwa unazilalalmikia wewe?

Hivyo ni viporo haijalishi watakuwa na mzunguko wa ngapi lakini lazima viporo vichezwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…