TFF na Wizara ya Michezo mdhibitini Hajji Manara ndiye kichocheo cha chuki uhasama wa Simba na Yanga

TFF na Wizara ya Michezo mdhibitini Hajji Manara ndiye kichocheo cha chuki uhasama wa Simba na Yanga

yes ni mwanaume anatafuta ugali kwa familia yake, wewe je tukuulize umeshawahi kumpa hata mia yako
Huu ni utetezi rahisi ,nimesema ni kazi yale inayompa ugali
Na sisi wenyewe pia tuna kazi zinazotupa ugali vile vile
 
Enzi ya Jerry Muro mlikua mnaona kutania wenzenu burudaani kabisa!
Acheni kujiliza kama watoto wa kike, pambaneni uwanjani heshima yenu irudi!
 
Wadau wa michezo toka enzi na enzi tunataniana na si kuvuka mipaka ya kuanza kutafutana matawi na kuanza kubomoleana vizimba vya matawi. Toka muda mrefu nimemfuatilia msemaji wa Simba kwa kauli zake yeye anaita za kukera ndizo chokochoko ambazo washabiki wa Simba nao wanazibeba kisha wanazungumza mbele ya mashabiki wa Yanga huku wakijua wanae zungumza nae ana hasira kiasi gani na wapembeni nae ana hasira kiasi gani ipo siku moto utawaka chukueni tahadhari hiyo ingawa yeye kwa kufanya hivyo anaingiza pesa ila anajenga chuki na si utani ule wa Simba na Yanga wa enzi na enzi werevu tumeliona hilo.
Mumesahau kauli za kichochezi alizokuwa anatoa Jerry Muro, alikuwa anatukera zaidi Haji anavyowakera ila tulivumilia. Tulieni mkamuliwe jipu lenu mpone fresh
JamiiForums-286118396.jpg
FB_IMG_1596970740939.jpg
 
Back
Top Bottom