TFF wanazidi kujipambanua kwamba Simba ni Kijana wao mpendwa

Songwe hauko Mbeya, ila ni kweli hauko mbali na Mbeya Mjini

Tazama ramani mzee...nikipata muda nitakuwekea ramani inayoonesha mpaka wa Mbeya na Songwe upande huo wa Mbalizi
 
Ukieleweshwa elewesheka basi Mkuu, ni mkoa unaojitegemea huo. Utakuaje tena mkoa wa Songwe uko ndani ya Mkoa wa Mbeya?
View attachment 2898376

Kumbe unamquote mtu hata pasipo kufuatilia mtiririko wa mjadala wa awali...

Soma vizuri utaelewa kinachotajwa kuwa Mbeya na si Songwe ni uwanja wa ndege wa Songwe...
 
Reactions: Tui
Yanga imecheza leo, Kesho inapanda ndege inakwenda Mbeya kumbuka watashukia Songwe na safari ya basi mpaka mbeya wakati huo Kesho
Acha malalamiko ya kitoto, kwani umeambiwa Songwe Airport ipo Tunduma? Yaan kilometa 20 tu unataka kuigeuza nongwa utadhani wanatokea Tunduma au Nakonde, au ulitaka watue hotelini moja kwa moja?
Simba anacheza na Azam Mwanza then anacheza na Geita utd pasipo na Shaka Tff watawabana Geita utd wachezee Mwanza so Simba hatosafiri na kupata faida ya kupunguza uchovu haya yote yanamtengenezea mazingira Simba..
Umeangalia
Kama walitumika sana, hilo si ni jukumu la Yanga kuwapumzisha?
Kama hilo halitoshi ukiangalia mazingira ya marefa bado wanaibeba SImba kuna tukio gemu na Mashujaa kule Kigoma Kibu D alichezewa rafu refa akatenga tuta leo the same same event kachezewa Yao refa kapeta.
ukiona refa hakubebi unatakiwa kuhesabu kuwa wapinzani wenu wapo 13 uwanjani. Sasa hilo nalo ni la kuwalaumu TFF?
Hakika matukio ni mengi ntajaza server ya JF tu ila Tff watambue kwa tabia hii ya kuipendelea Simba ni ngumu sana kuja kupata timu nzuri ya taifa tutaendelea kudemadema tu
Kama ni ngumu yanini sasa kulalamika?
 
Mayowe yameshaanza
 
MPIRA WA BONGO NDIVYO ULIVYO.

SISI HATUTAKUJA KUENDELEA HATA SEKTA MOJA.

N:B UKIZIDISHA SANA USHABIKI WA SIMBA NA YANGA AKILI ZINAANZA KUPUNGUA.
 
Reactions: Tui
Unapotaka kukosoa ufanye utafiti kwanza..acha kuchanganywa na majina ya mikoa..uwanja unaitwa Songwe ila uko mkoa wa Mbeya.
 
Reactions: Tui
Songwe Airport ipo mkoa wa Mbeya, siyo Songwe.
Unapotaka kukosoa ufanye utafiti kwanza..acha kuchanganywa na majina ya mikoa..uwanja unaitwa Songwe ila uko mkoa wa Mbeya.
Aisee nilikua sijui hili, ndio nimejua leo. Mko sahihi kabisa.

Imetumwa : May 12th, 2018

Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya imependekeza kwa pamoja kubadilishwa kwa jina la Uwanja wa Ndege wa Songwe kuitwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mbeya (MIA)

Mapendekezo hayo yalitolewa na wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika jana Ukumbi wa Mkapa na kusema kuwa kumekuwa na mkanganyiko wa mahali ambapo uwanja huo upo.

Akiongea katika Kikao hicho Mwenyekiti wa kamati Mhe. Amos Makalla alisema kuwa kuwepo kwa Mkoa na Wilaya mpya iliyobeba jina la Songwe kumeleta changamoto ya utambuzi sahihi wa maeneo na miundombinu inayotumia jina hilo.

Mhe. Makalla alisema changamoto hiyo imeleta mkanganyiko mkubwa hususani kwa wageni mbalimbali wakiwemo watalii, wasafiri, wawekezaji na hata Watendaji wa Serikali kujua eneo halisi la uwanja huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya Bw Mwalingo Kisemba alisema kuwa lengo la kubadili jina ni kufanikisha kwa urahisi mikakati ya mkoa ya uwekezaji, biashara na utalii ili kuwarahisishia wawekezaji namna ya kuutambua mkoa na miundombinu yake.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya Bw. Bosco Mwanginde alisema kuwa mkanganyiko huo wa jina la uwanja umepelekea wawekezaji kudhani kuwa miundombinu hiyo ipo Mkoa wa Songwe badala ya Mkoa wa Mbeya na kuupunguzia mkoa sifa ya kuwepo kwa miundombinu rafiki kwa ajili ya uwekezaji.

Ujenzi wa uwanja wa Songwe ulizinduliwa rasmi mwaka 2001 na kuanza kutumika mwaka 2012. Jina la Uwanja wa Songwe lilitokana eneo ambalo uwanja huo upo na uwepo wa mto Songwe eneo hilo.
 
Yes, hauko peke yako. Wengi ilikuwa ikiwachanganya hii na wengi bado inawachanganya.
 
Mkuu songwe airport Ipo mkoani mbeya,ni dk10 tu kwa daladala kutoka airport mpaka city centre
 
Yanga ikiwa inafanya vizuri TFF inapumua ila mambo yakianza kuonekana tofauti............
 
Jana kulikuwa na clear penalties 4
1 Yao yao
2Beki wa biashara alinawa
3Max
4Kibabange
Zote refa alimeza filimbi!
 
Kuwa Yanga ni mmoja wa mnufaika hilo halina ubishi na hiyo imetengenezwa namna ili ionekane Yanga nae yumo ila mlengwa mkuu yaani mnufaika namba moja ni Simba.
Swala la mashindano mengi ni shindano moja tu ndio iliyoongezeka ambayo ilikuwa ni AFL ambapo mlicheza mechi mbili tu mkaaga mashindano. Au mlicheza hadi fainali?
Ukitaka kuona TFF wapo kimkakati zaidi na wapo kwaajili ya kuitengenezea mazingira simba kwa kutengeza matokeo; angalia ratiba walivyopanga, yaani Simba ndiye mwenye kiporo zaidi ya wote lakini kwenye fixture wameifanya Yanga ndio itangulie kucheza kabla ya Simba. Kichekesho zaidi ni kwamba Yanga ndiye atakayeaanza kucheza mechi ya raundi ya 15 na mechi ya raundi ya pili kabla ya hata ya Simba. Wameweka ratiba ya kiporo cha Simba tarehe ya mbele ambapo Yanga atakuwa bado katangulia mechi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…