TFF yatoa maamuzi sakata la Ramadhani Singano 'Messi' na timu yake Simba

Mkuu katika mkutano wa TFF ulioamua hili suala, wajumbe waliokuwapo ni;

1. Collin Frisch - Simba SC
2. Ramadhan Singano
3. Kisoki - Mwenyekiti Sputanza
4. Celestine - Katibu TFF

Sasa hapa Hans Pope anaingiaje Mkuu?
Mkuu!
Hans Pope na Haji Manara wanahusika kwa sababu ni wao ndio waliohakikisha kwenye maongezi yao na wanahabari kwamba Simba ina mkataba halali wa miaka 3 wa Singano, kwamba watamchukulia hatua za kisheria Singano kwa kuikosea heshima Simba, kwamba Singano anapotoshwa na waliowaita mawakala uchwara, n.k. Waliropoka hayo bila ya kutafakari kwamba wao na uongozi wao sio walioingia mkataba - wowote kati ya miwili iliyokuwa ikibishaniwa - na Singano. Si hasha Collin aliingia kwenye mkutano huo akiwa amejaa kujiamini kulikotokana na kauli hizo nzito za Pope na Manara. Laiti wawili hao wangetumia kwanza busara kutaka kumsikiliza Singano na madai yake kabla ya kuropoka walivyoropoka, 'aibu' ya jana isingempata Collin, Simba wala TFF iliyolazimika kwa mara nyengine kuamua kisisasa swala la kisheria.
 
Me nafikiri tufike mahali ijulikane wazi, hata kama mikataba yote miwili ina makosa lakini uliopo au ulipokelewa kule TFF na kugongwa muhuri ni upi kati ya hiyo miwili? au yote haipo kule TFF? Kama yote haipo kule TFF, je uliopo unaisha mwaka gani?.

Tukiyajua hayo ndo Simba wakae na Messi wamalize kiundugu.
Vinginevyo bado kuna utata mkubwa kwa kuwa jamii inataka kujua nani mshindi kama mjadala wa mwanzo ulivyojielekeza, hivyo kuna haja ya kupata majibu.

Kuna upande wa Simba, Messi na upande wa Waandishi wa habari ambao wengi pia wapo kwa Messi kwa sababu kwao kama waandishi story kubwa ni Simba kufoji mkataba ndiyo itakayouza kuliko Messi kufoji mkataba, kwahiyo lazima watakuwa upande wa Messi kwa maslahi ya kazi zao.
 
Mkuu katika mkutano wa TFF ulioamua hili suala, wajumbe waliokuwapo ni;

1. Collin Frisch - Simba SC
2. Ramadhan Singano
3. Kisoki - Mwenyekiti Sputanza
4. Celestine - Katibu TFF

Sasa hapa Hans Pope anaingiaje Mkuu?
Sasa huyu Singano ameshindwa hata kumtafuta mwanasheria kwa msaada zaidi.
 

Japo kuna mikanganyiko ya kimkataba.. ila ukimuangalia Messi moyo wake haupo kabisa Simba Sc.. busara inabidi itumike kwa kumuacha aende zake.
 
Sasa huyu Singano ameshindwa hata kumtafuta mwanasheria kwa msaada zaidi.

nadhani hapo mwanasheria wake alikua ni huyo kisoki ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wacheza mpira.
 
Mi naona simba wamuache aende tu

Kumuacha aende inaweza kuwa sahihi, lakini lazima tujue kwanza sakata hili linaishaje. Tusiwape ujiko kirahisi tu kina Shaffih Dauda. Hapa kama SSC tumesanda ieleweke TU au kama wamesanda wao ieleweke pia.
 

Nyie ndio mnaendekeza ujuha kwenye taifa letu. Kama TFF wana mkataba halali wa Simba dhidi ya Singano, kwa nini basi walazimishe majadiliano ya mkataba mpya? Hapo kuna mambo mawili tu :

1. Ama Singano amechezea Simba pasipo kuwa na mkataba halali kisheria (mkataba wake una mapungufu yanayoufanya uwe batili)

2. Ama Simba wameghushi mkataba wa Singano. Hakuna zaidi ya hapo

Kudhani kuwa Singano kagushi mkataba wake haiwezekani. Pia TFF wamedhihirisha uhuni wao katika hili. Hapa palikuwa na maamuzi ya aina moja tu : nani kagushi mkataba ambalo ni kosa kisheria. Kwamba Singano ana photocopy si hoja. Msimamizi wa mkataba maadam yupo. TFF wanaficha uovu, jambo ambalo jumuiya ya soka haipaswi kulifumbia macho. Hapo lazima upande mmoja uwajibike, hakuna mjadala. Mikataba mawili tofauti iliyosainiwa na mtu yule yule ni serious offence. Bahati mbaya common sense is not that common!!
 
Jana nilipata wasaa wa kuangalia taarifa ya habari azam tv nikajiridhisha tena kwenye mshikemshike viwanjani,,,,kuna jambo huwa silielew...hivi simba wanavyodai kwenye mazungumzo ya jana hapakuwa na mshindi kwenye uchakachuzi wa mkataba wa mchezaji (messi) wanamaana gani kama hakuna mshindi inakuwaje TFF waambie simba wakae chini wajadili mkataba mpya...kitu ambacho ni kinyume na madai ya simba kwamba mkataba unaisha 2016 kwa mantiki hii basi MESSI alikuwa sahihi kusema muda wa mkataba wake umeisha...nilicheka sana MANARA (msemaji wa simba) alivyokuwa anakomalia kuwa hakuna mshindi simba watakaa na messi wajadili mkataba mpya, wakati mwanzo kila uchao kwenye media akidai watamkomesha MESSI! yakowapi MANARA ? Kwa staili hii tutaendelea kuuwa vipAji na mchezo wa soka na kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu TFF naona mmefunika kombe mwanaharamu apite, niliyegemea adhabu iwepo hapa hasa kwa simba kwa kugushi mkataba wa kijana...SIMBA HAMNA SHUKRANI
 
Kumuacha aende inaweza kuwa sahihi, lakini lazima tujue kwanza sakata hili linaishaje. Tusiwape ujiko kirahisi tu kina Shaffih Dauda. Hapa kama SSC tumesanda ieleweke TU au kama wamesanda wao ieleweke pia.

ili iweje?
 
simba ana shukurani sana ..na uzuri wao wakila wakashiba wala hawasumbui wanyama wadogo kama swala..tatizo kuna mnyama mkorofi anaitwa libolo....aaahh ni shida huyu mnyama
 
DOGO MESSI naye hajitambui kwanini akubali hakuna mshindi, wakati kuna upande umegushi mkataba ,
 
TFF ndo mchawi wetu katika hili swala, yan hii timu ya malinzi itatuulia soka letu, sijapata mantiki ya kusema wakae waongee wakati shida yetu ni kujua mkataba wa nani ni sahihi
 
DOGO MESSI naye hajitambui kwanini akubali hakuna mshindi, wakati kuna upande umegushi mkataba ,

'Messi' ni mshindi: Yeye anadai hana mkataba na Simba kwa vile umeisha baada ya kuitumikia miaka miwili, Simba wanadai 'Messi' bado ana mkataba nao uliobakiza mwaka mmoja. Kwa kuwa TFF imeamua wakae wajadili mkataba mpya ni dhahiri kuwa 'Messi' hana mkataba tena na Simba na mkataba ulioko Simba ni batili.

My Stand:
Hadi sasa 'Messi' ni mchezaji huru, anaweza kuongea na timu yoyote na kujiunga nayo kwa utashi wake, sio lazima aongee na Simba pekee.
 
Tatizo ni tff wanashindwa kuwa na mwanasheria mmoja wa kuajiriwa ili awe anatoa ushauri ya mikataba iwe ya ndani au nje ya nchi pindi mchezaji anapopata dili huko..na mikataba inakua kwa wakili,mchezaji copy na tff. Kwa atakae kaidi kufanya kazi bila kumuona wakili wa tff yatakayotokea asilaum..
 
hata hivyo ungemsikia chotara wa kigirik kwenye efm sport hadecoter mh hans pope mesi anakazi kamkomalia kama kamzaa.
nikisikia simba wakatamka kuwa kuanzia sasa hatumuhitaji singano nitajua watakuwa wastarabu lakini hans pope kasema wanataka mahakamani ya hadhi ya wachezaji ili wawahonge wapate ushindi ili mesi aendelee kukata rufaa fifa ili aendelee kutocheza mpira na hapo itakuwa TANZANIA FITINA FEDARATION
 
Yaani huyo mshenzi Pope amenikera amekomaa na mtoto watu, eti ooh tushampa mkataba mwngne, sasa km bado wana mkataba nae wamempa mwngine wa nn
 
Kuondoa uhuni na kujenga nidhamu katika soka

Hakuna haja ya vita zisizo na msingi

Acheni dogo akacheze mpira

Simba tumekosea...Huwezi kumlipa messi sh laki 4 na bado unamlazimisha mwaka mwingine tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…