mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
Mkuu!Mkuu katika mkutano wa TFF ulioamua hili suala, wajumbe waliokuwapo ni;
1. Collin Frisch - Simba SC
2. Ramadhan Singano
3. Kisoki - Mwenyekiti Sputanza
4. Celestine - Katibu TFF
Sasa hapa Hans Pope anaingiaje Mkuu?
Hans Pope na Haji Manara wanahusika kwa sababu ni wao ndio waliohakikisha kwenye maongezi yao na wanahabari kwamba Simba ina mkataba halali wa miaka 3 wa Singano, kwamba watamchukulia hatua za kisheria Singano kwa kuikosea heshima Simba, kwamba Singano anapotoshwa na waliowaita mawakala uchwara, n.k. Waliropoka hayo bila ya kutafakari kwamba wao na uongozi wao sio walioingia mkataba - wowote kati ya miwili iliyokuwa ikibishaniwa - na Singano. Si hasha Collin aliingia kwenye mkutano huo akiwa amejaa kujiamini kulikotokana na kauli hizo nzito za Pope na Manara. Laiti wawili hao wangetumia kwanza busara kutaka kumsikiliza Singano na madai yake kabla ya kuropoka walivyoropoka, 'aibu' ya jana isingempata Collin, Simba wala TFF iliyolazimika kwa mara nyengine kuamua kisisasa swala la kisheria.