TFF yatoa maamuzi sakata la Ramadhani Singano 'Messi' na timu yake Simba

mm namshauri mesi simba usiwasogelee hata kuwanusa hawa tanzania fitina fedaration naamini watakufanyia fitina tu ni bora kuanzia sasa tafuta timu ufanye mazoezi
 
Samahani Mkuu, naomba uniruhusu nitofautiane na wewe kidogo:
1. Kama uhuru wa Messi unategemea mkataba ulioko TFF, kwa nini TFF isisimame kwenye mkataba huo? Jawabu pekee inayokidhi haja ni kwa sababu TFF ilibaini kasoro zinazoufanya mkataba huo usiweze kusimamiwa, yaani ni batili.
2. Kama TFF imeona hivyo, unadhani vyombo vya sheria visingeona? Pengine visingeona, iwapo mkataba wenyewe haukuwa na kasoro yoyote ila TFF tu ndio iliamua hivyo kwa sababu zao. Lakini kama TFF imefanya hivyo, Collins angekuwa mjinga kiasi gani kuridhia 'uonevu' huo?
3. Hata kwenye swala la Ngassa, mkataba wa Ngassa na Simba ulikuwa batili kwa sababu uliingiwa wakati Ngassa bado ana mkataba wa zaidi ya miezi 6 na Azam. Kitendo cha TFF kuingilia suluhu ya mkataba huo batili ilikuwa ni kuhukumu kisiasa swala la kisheria, kama walivyofanya jana kwa mkataba wa Messi.
 
Japo kuna mikanganyiko ya kimkataba.. ila ukimuangalia Messi moyo wake haupo kabisa Simba Sc.. busara inabidi itumike kwa kumuacha aende zake.
Mkanganyiko wa kimkataba sawa. Lakini HP na HM walipaswa kujiridhisha wao kwanza juu ya undani wa Messi kun'gan'gania kwamba ana mkataba wa miaka miwili tu. Angalau wangejiuliza kwa nini mkimya Messi amegeuka kupaaza sauti ghafla. Wangekumbuka ule usemi/wimbo 'bubu hutaka kusema anapozidiwa na mambo'. Hii ya Messi kutokuwa na moyo tena na Simba imechangiwa sana na kauli za kudhalilisha za HP na HM dhidi yake, bila ya wao kuangalia kwanza undani wa swala hili na/au kukaa naye kwanza mezani.
 
Hakuna haja ya vita zisizo na msingi

Acheni dogo akacheze mpira

Simba tumekosea...Huwezi kumlipa messi sh laki 4 na bado unamlazimisha mwaka mwingine tena
Mkuu,
Leo nimefurahi sana kusoma comment yako. Unajua kwanin nimefurahi!!!
Ni kukuona mkuu unatoa maoni yako mazuri na ya kujenga kwa maendeleo ya soka letu bila kujali ushabiki.
Nani angeridhika kuwaona wenzake wakifanikiwa katika soka na yeye akiendelea kuishi maisha ya kubahatisha!?
Hassan kessy kwa mwezi analipwa milioni 2 na laki 2,
Mkude analipwa milioni 2 na laki 5 kwa mwez.
Iweje yeye afurahie kulipwa vilaki 4!!
 
Ushauri wa bure kwa singano asisikilize hao waandishi na watangazaji uchwara (ambao siku hizi eti ni mawakala wa wachezaji) wasiojua sheria wao kwa maamuzi ya jana wanakimbilia ooh messi yupo huru. Hata wakati wa ngasa walisema hivyo hivyo wakaweka na picha za ngasa kwenye blog zao kashika mamilioni anaenda kuwalipa simba lakini kilichotokea baadae kila mtu anajua na wao ndio walikuwa wa kwanza kumcheka ngasa wakati anakula nusu mshahara. Kwa kifupi messi anachotakiwa kufanya awe jasiri awafuate viongozi wa simba awaambie live mahusiano ya kikazi kati yao na yeye yamekuwa si mazuri hivyo hakuna uaminifu tena kati yao kwa hiyo wamwache huru akatafute maisha sehemu nyingine naamini viongozi wa simba watakua waungwana watamwacha huru. Hakuna asiyejua kati yetu nini hutokea pale mwajiri na mwajiriwa wanapotokea kukosa kuaminiana.
 
Nmegundua kuwa Viongozi wa simba ndo chanzo cha timu kuwq hovyo wamekaa kiujanja ujanja tu
 
We jamaa una akili sana,kwa maana hiyo simba ndio wamefoji mkataba
 

sputanza nao wamenunuliwa ?
 

Hakuna uvivu wa kufikiri hapa, wewe sema unazo facts zaidi yetu sisi wengine kuhusu ili saga. Labda nikuulize kwa nini huyo Messi hana mkataba original? Kwa kawaida inapashwa ziwe original 3 kwa case kazi hizi. Kila party yaani Simba na Messi wanakuwa na original copy na TFF wanapeleka original copy vile vile. Na je aliyepeleka huo mkataba TFF ni mchezaji au ni Simba? Kama ni Simba waliupeleka, basi wanayo nafasi kubwa kwamba walipeleka huo ambao upo forged. Kuondoa huo utata ili suala lingekwenda polisi ili wahusishe wataalamu wa miandiko ili kubaini nani mwenye mkataba halali kati ya Simba na Messi. Huu mtindo wa forgery inabidi utafutiwe dawa.

Tiba
 

ili la simba kufoji mkataba sio la mara ya kwanza
 
... na mkataba ulioko Simba ni batili.
Tatizo watu mna vichwa vigumu. Ishu sio mkataba uliopo Simba au kwa Messi, ishu ni mkataba uliopo TFF. Kama mkataba wa Messi ndio ungekuwepo TFF, angeshakuwa huru zamani sana na Yanga wangeshampa milioni 70
 
Huyo ndio Malinzi bwana..na huyo ndio muwakilishi wetu kwenye kumchagua Blatter..akili za kima kabisa hizi

kwanini FBI, wasijifanye wamekosea njia waibukie na huku TFF?!! haponi mtu, na huyu malinzi ni hamna kitu kabisa, eti katibu mkuu wake anajiita KOFI ANANI, eti mtaalamu wa kutatua migogoro!! na siku hizi wameleta kipengere kwenye sheria, eti common sense ndio inatumika zaidi, ukiwauliza ni kanuni gani imetumika kutatua mzozo huo, ni commonsense(funika kombe mwanahalamu apite) !!! na ndio maana ulikuwa ukimgusa tu Blatter, unaonekana huutakii mema mpira wa Afrika!! kumbe ni huko kufaidika na pesa wanazoletewa bila kuwa audited!! ndio hayo yakina jack Warner!! nahadi pesa za wahanga wa mafuriko ya haiti amepiga!! ki fupi hii fifa ya Blatter lilikuwa chaka la wahuni kupiga pesa, ukihoji kidogo, ohho fifa hairuhusu kwenda mahakamani!! wanazidi kupiga tu, Asante sana USA(Polisi wa dunia)
 
Tatizo watu mna vichwa vigumu. Ishu sio mkataba uliopo Simba au kwa Messi, ishu ni mkataba uliopo TFF. Kama mkataba wa Messi ndio ungekuwepo TFF, angeshakuwa huru zamani sana na Yanga wangeshampa milioni 70

Kama ilivyokuwa kwa Kelvin Yondan
 
Tatizo watu mna vichwa vigumu. Ishu sio mkataba uliopo Simba au kwa Messi, ishu ni mkataba uliopo TFF. Kama mkataba wa Messi ndio ungekuwepo TFF, angeshakuwa huru zamani sana na Yanga wangeshampa milioni 70

Na kama mkataba ulioko TFF ungekuwa halali, kusingekuwa na haja ya majadiliano ya mkataba mpya. Tumia logic ndogo tu hapo
 
ndio maana walisema wazingatie mkataba mama wengine hawajaelewa mkataba mama ni upi mkataba mama ni ule ulioko tff tatizo yanga mpaka sasa hawajui kwanini wanafungwa na simba kila wakikutana badala yake wanafikiri wakichukua mchezaji simba ndio wanaweza kupata ushindi messi amepata jina kupitia simba hivyo yanga waache kiherehere simba wanaweza kumruhusu na bado asifanye chochote kwani mpira wa simba na yanga ni tofauti
 
Miongoni mwa comment mbovu hii kuwahi kutokea humu jamvini hii mojawapo.
 
Kwani TFF hawana mwana sheria? TFF kama walipenda kusuluhisha ilikuwa busara kwao Kwanza kumbaini mkosaji na makosa yake, pamoja na adhabu kulingana na sheria, na kanuni. Wote; mkosaji na aliyekosewa wakikubaali na kutambua makosa na kuyakiri, hapo sasa busara ya TFF itumike kuwapatanisha. Kwa maoni yangu.
 
#Jamali_Malinzi yukwapi!? Si kipindi kile alikuwa anakuja kujibu jibu hapa, sa hivi maji ya shingo kapotea zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…