TFF yaunda Kamati inayoongozwa na Paul Makonda ya kusaidia Taifa Stars ishinde kufuzu AFCON! Je, kazi yake ni nini hasa?

TFF yaunda Kamati inayoongozwa na Paul Makonda ya kusaidia Taifa Stars ishinde kufuzu AFCON! Je, kazi yake ni nini hasa?

Tati

Kwa maoni yangu hii kamati imekaa "kisiasa" zaidi watu kama Zitto kabwe wako wapi? au "Msomali" anaogopa kelele za Lumumba, Bashite hakustahili kuwepo kwa kuwa si mtu wa mpira bali ni mtu wa kurukia rukia kila jambo lenye mvuto kwa watu..Anyway hili ndio tatizo la kutengeneza kamati kabla ya kujua nini lengo na kazi ya kamati hiyo....
Kamati imeundwa ili kuwapaisha watu fulani. Katika watu wote kiongozi awe Bashite? Huu utani mbaya sana.
 
Kwa akili Hizi Za Tff mpira hautakaa Usonge mbele, acha tufungwe tu maana waganda wamejiandaa kwenda, eti kamati ya ushindi, hivi walishatafakari na kujiuliza kwamba ili Taifa Stars Ishinde inahitaji Kamati?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ligi kuu timu ina viporo nane si vichekesho wazalendo tunateseka sana na Taifa letu hili
Hovyo kabisa
 
TFF wanajaribu kufanya kitu ili Timu ifuzu, Kuliko kukaa bila kujaribu ni bora wamejaribu haijalishi kwenye kamati ameteuliwa nani kinachotakiwa ni kuonyesha Uthubutu. Kamati haichezi ila ina hamasisha na kujaribu kufanyakitu nje ya uwanja. Tanzani haijaanza kuunda kamati leo, zilisha kuwepo kabla mwisho wasiku wachezaji na benchi la ufundi ndio wapambanaji sisi ni kutoa hamasa. Tatizio tulilonalo kila mmoja kujifanya mjuaji tunaingiza na siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu kushiriki michuano ya AFCON 2019, Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) limetangaza majina 14 yatakayokuwa kwenye kamati iliyopewa jina la Saidia Taifa Stars ishinde.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu ni Mhandisi. Hers Said.

Wajumbe wengine ni pamoja na Mohamed Dewj 'Mo' Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Patrick Kahemele na Abdallah Bin Kleb na Mohamed Nassor.

Wengine ni pamoja na Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Faraji Asas, Jery Muro na Haji Manara.

Stars watakuwa na kibarua mwezi Marchi kucheza na timu ya Taifa ya Uganda ili kufuzu hatua hiyo ya AFCON na dua zao zikiwa kwa Lesotho kupoteza mbele ya Cape Verde

Kwenye kundi L ambalo Stars ipo Uganda wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku Stars na Lestho zikiwa na pointi tano na Cape Verde wana pointi nne

View attachment 1027290

My take:
Vyombo vyetu vya habari na waandishi wabobezi wa michezo ni kwangu pakavu, wao wangetuamsha kwa kufanya awareness raising campaign.

Tukatae ubabaishaji wa aina hii michezoni maana wanaonufaika ni wachache

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wangemteua Ismail Aden Rage yule ndio anazijua fitna za soka kulikoni hiki kikundi cha wanasiasa!
 
Back
Top Bottom