zipompa
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 11,432
- 24,596
Niko na wewe, zikiwa chache ziwe 10 kuanzia maombi ya leo usiku hili sita liacha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niko na wewe, zikiwa chache ziwe 10 kuanzia maombi ya leo usiku hili sita liacha
Kamati imeundwa ili kuwapaisha watu fulani. Katika watu wote kiongozi awe Bashite? Huu utani mbaya sana.Tati
Kwa maoni yangu hii kamati imekaa "kisiasa" zaidi watu kama Zitto kabwe wako wapi? au "Msomali" anaogopa kelele za Lumumba, Bashite hakustahili kuwepo kwa kuwa si mtu wa mpira bali ni mtu wa kurukia rukia kila jambo lenye mvuto kwa watu..Anyway hili ndio tatizo la kutengeneza kamati kabla ya kujua nini lengo na kazi ya kamati hiyo....
Kwa akili Hizi Za Tff mpira hautakaa Usonge mbele, acha tufungwe tu maana waganda wamejiandaa kwenda, eti kamati ya ushindi, hivi walishatafakari na kujiuliza kwamba ili Taifa Stars Ishinde inahitaji Kamati?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nitashangaa Mo kushiriki kwenye kamati kama hii. Huenda ni njia nyingine ya kumdhalilisha.
Na mimi nasema tufungwe!Bora tufungwe tu
Tangu tukio la utekaji, DAB akienda uwanjani Mo haendi, No akienda uwanjani DAB haendi.Mechi ya watani nlimuona DAB yu Karibu na Mwakye! Na hakuvaaa ile T-shirt yake!
Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wangemteua Ismail Aden Rage yule ndio anazijua fitna za soka kulikoni hiki kikundi cha wanasiasa!Kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu kushiriki michuano ya AFCON 2019, Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) limetangaza majina 14 yatakayokuwa kwenye kamati iliyopewa jina la Saidia Taifa Stars ishinde.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu ni Mhandisi. Hers Said.
Wajumbe wengine ni pamoja na Mohamed Dewj 'Mo' Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Patrick Kahemele na Abdallah Bin Kleb na Mohamed Nassor.
Wengine ni pamoja na Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Faraji Asas, Jery Muro na Haji Manara.
Stars watakuwa na kibarua mwezi Marchi kucheza na timu ya Taifa ya Uganda ili kufuzu hatua hiyo ya AFCON na dua zao zikiwa kwa Lesotho kupoteza mbele ya Cape Verde
Kwenye kundi L ambalo Stars ipo Uganda wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku Stars na Lestho zikiwa na pointi tano na Cape Verde wana pointi nne
View attachment 1027290
My take:
Vyombo vyetu vya habari na waandishi wabobezi wa michezo ni kwangu pakavu, wao wangetuamsha kwa kufanya awareness raising campaign.
Tukatae ubabaishaji wa aina hii michezoni maana wanaonufaika ni wachache
Sent using Jamii Forums mobile app