Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Nimekutana na hii barua kutoka kwa Kaka yangu Cliford Ndimbo kuwa imevifungia viwanja vya Jamhuri, Kirumba, pamoja na Liti kwa kukosa vigezo vya ubora wa kuchezesha michezo ya ligi kuu.
Ni suala zuri na bora kutoa taarifa kwa umma kuwa kuna viwanja ambavyo vimekosa vigezo muhimu kikanuni ila taarifa yetu imekaa kimkakati, sidhani kama kuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye hafahamu kuwa viwanja hivi vipo chini ya chama cha CCM na sio timu ambazo zinacheza kwenye viwanja hivyo.
Mfano mzuri, Kiwanja cha Kirumba ambacho kimekuwa kikitumiwa na timu ya Pamba Jiji ni mali ya CCM mkoa wa Mwanza. Vivyo hivyo viwanja vya Jamhuri pamoja na Liti.
Kitu cha ajabu ni kuwa kwenye taarifa ya Ndimbo na kamati yake hawajasema wala kuweka wazi kuwa viwanja hivi ni miundombinu ya CCM, yaani CCM KIRUMBA, CCM LITI pamoja na uwanja wa Jamhuri. Na ni suala la uwazi kuwa timu hizi hazichezi michezo yake bure bila gharama, wanalipa pesa kwa wamiliki wa miundombinu hii.
Taarifa mwishoni inasema kuwa TFF inazihimiza timu kutunza na kuboresha hali za viwanja hivyo. Najiuliza kwa sauti ya kinyonge sana je, timu ya Pamba Jiji ina uwezo upi au mamlaka gani ya kwenda kurekebisha miundombinu ya uwanja wa CCM Kirumba?