Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
UFAFANUZI KUHUSU UTARATIBU WA UGAWAJI WA MASHAMBA KATIKA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO
Agosti 27,2026 - Dodoma, Tanzania
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umefuatilia taarifa na madai yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii na miongoni mwa baadhi ya wananchi kuhusu uwepo wa uuzaji wa mashamba katika Shamba la Miti la TFS West Kilimanjaro, lililopo Kata ya Endumeti, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro.
Hoja ya awali ~ Shamba la Miti TFS - West Kilimanjaro lichunguzwe, maeneo ya misitu yanauzwa 'cash', kuna mazingira ya uhujumu uchumi
TFS inapenda kufafanua kuwa maeneo yanayotajwa katika taarifa hiyo hutolewa bure bila malipo yeyote kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na shamba hilo kama sehemu ya ujirani mwema kwa ajili ya kulima mazao ya muda mfupi baada ya miti kuvunwa ikisubiriwa msimu mwingine wa upandaji.
Utaratibu huu ambao husimamiwa pia na serikali za vijiji husika hufahamika kitalaam kama 'Taungya'. Utaratibu huu unalenga kuwapa wananchi fursa za kiuchumi kupitia kilimo ambapo wengi wamenufaika nao kwa miaka mingi.
TFS inapenda kuwakumbusha wananchi wote wanaopewa mashamba hayo kuzingatia masharti yaliyowekwa wakati wote na kuwaomba wasirubuniwe kuuza au kuuziwa mashamba hayo kwani kinyume cha taratibu na nia njema ya serikali. Wakala hautasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mwananchi au mtumishi yeyote wa shamba atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo.
Imetolewa na;
SACC Johary Kachwamba,
MENEJA UHUSIANO-TFS