Thamani ya maneno POLE na SAMAHANI katika Mahusiano

Pamoja na kuwapenda nini nini... Akili hio na uzoefu unaonesha.. kuna vitu ukikiri kwa Mwanamke ndio umepoteza kabisa kabisa. Wanaume tunazo njia laki nane... mwanaume anaweza kuwa amefanya kosa na ni kweli ni kosa akalikuchambulia ukakuta wewe mwanamke unampigia magoti na umbembeleze vibaya mno akusamehe... masikini ... trust me cc watu8

Kwani nyie hamuonagi mnavyomchukia mwanaume mwenye tabia tabia za kike kike (simaanishi gays apa) ....
Bible pia iliagiza mtupende. Sasa unashindwaje kumuomba msamaha mtu unayempenda, endapo umemkosea
 
mme huomba msamaha wa dhati pale unapomshika red hended kachit basii. Kwingne huku unapigwa danadana tu.
 
Nakumbuka usia wa babu yangu.
"Mjukuu wangu daima kumbuka, ukitaka kuishi vyema na mwanamke daima kuwa mtu usietabirika"

Mara nyingi nikikosea navuta pumzi kidogo kisha baadae namuomba msamaha wa ubavu wangu pamoja na mahaba kibao.
Ila mara nyingine naharibu hali ya hewa halafu nakuwa nunda hadi anashangaa.
Basi mwenyewe utasikia anasema, "mume wangu ni mpole ila we usiombe ukute siku bange zake zipo kichwani"

Somo ni kuwa;
Ili kujenga mahusiano mema na wandani wetu wanaume tunatakiwa kuwatendea wema na kuwasiliana nao kwa upole ili kujenga mapenzi baina yetu, ila hatutakiwi kufikia mahali ikawa ni fomula.
Wanawake hupenda pia kuziona haiba na tabia fulani za kiume kwa waume zao zilizo katika mila na desturi za jamii zao. Mfano utukutu na ubabe fulani hivi ambao haujapitiliza.
Ukiwa laini sana hawajisikii raha, na ukiwa mbabe sana unawapotezea amani.

Amani kwenu

Na kwako pia
 
Bible pia iliagiza mtupende. Sasa unashindwaje kumuomba msamaha mtu unayempenda, endapo umemkosea

Bi mkubwa nahisi hujayaelewa vyema hayo niliyoyaandika nami pasi hiyana nitakufafanulia...

Mleta mada katuletea kisa cha Hawa na Adamu, katueleza zaidi namna Adamu alivyoshindwa kuomba msamaha kwa Mungu kwa niaba ya mkewe...

Utakubaliana na mimi kuwa katika kisa hicho hapo juu hakuna mahali ambapo Hawa alimkosea Adamu isipokuwa wote wawili walimkosea Mungu...

Kwa mantiki hiyo basi, aliyepaswa kuombwa msamaha ni Mungu na wala sio Hawa. Kitendo cha Adamu kushindwa kuomba msamaha kwa Mungu na kusukuma zigo lote kwa Hawa ndicho kilichozua tafakuri kwa mleta mada na kuiwakilisha hapa kwetu...

Sasa je sisi wanaume wa leo tunajifunza nini hapo?

Kimsingi kuna mafunzo mengi kutokana na kisa cha Adamu na Hawa, isipokuwa kwa wanaume kuna funzo moja kubwa...

Funzo hili ni namna ya kuishi nanyi kwa akili, na hivyo ndivyo Biblia ilivyotuagiza

(1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.)

Hilo ulilolibainisha la kusameheana nafikiri ni mjadala mwingine kabisa(labda kama sijaielewa hii mada), kwa sasa tujadili hili la kusukumiana mizigo badala ya kuwajibika kwa niaba.
 
Kuomba msamaha inategemea na kosa na mda mwengine ni lazima ufanye ivo ili kuonesha upendo. Neno "samahani" na "asante" lina maana kubwa sana kwa wanandoa wote, linapotumika huonyesha kujali kwa anaeambiwa "honey am sorry"
 
Wanaume wengi hawaombi msamaha ila wanakubali kumaliza kimyakimya

Mimi msamaha siombi, ila suluhu ni kwenye kitanda, akijifanya kanuna imekula kwake coz it's the only opportunity that I can truly say "I'm sorry" out of that ni fix tu!
 
duh hii imekaa njema lakini inabidi uangalie unaomba msamaha kwa lipi sio kila kitu beib naomba msamaha. mhhhh utapandishwa juu ya mti ukiwa umevaa moka na suti.
 
Pamoja na kuwapenda nini nini... Akili hio na uzoefu unaonesha.. kuna vitu ukikiri kwa Mwanamke ndio umepoteza kabisa kabisa. Wanaume tunazo njia laki nane... mwanaume anaweza kuwa amefanya kosa na ni kweli ni kosa akalikuchambulia ukakuta wewe mwanamke unampigia magoti na umbembeleze vibaya mno akusamehe... masikini ... trust me cc watu8

Kwani nyie hamuonagi mnavyomchukia mwanaume mwenye tabia tabia za kike kike (simaanishi gays apa) ....

kuishi na wanaume ni tabu, na kishi bila nyie haiwezekani
 
Bi mkubwa nahisi hujayaelewa vyema hayo niliyoyaandika nami pasi hiyana nitakufafanulia...

Mleta mada katuletea kisa cha Hawa na Adamu, katueleza zaidi namna Adamu alivyoshindwa kuomba msamaha kwa Mungu kwa niaba ya mkewe...

Utakubaliana na mimi kuwa katika kisa hicho hapo juu hakuna mahali ambapo Hawa alimkosea Adamu isipokuwa wote wawili walimkosea Mungu...

Kwa mantiki hiyo basi, aliyepaswa kuombwa msamaha ni Mungu na wala sio Hawa. Kitendo cha Adamu kushindwa kuomba msamaha kwa Mungu na kusukuma zigo lote kwa Hawa ndicho kilichozua tafakuri kwa mleta mada na kuiwakilisha hapa kwetu...

Sasa je sisi wanaume wa leo tunajifunza nini hapo?

Kimsingi kuna mafunzo mengi kutokana na kisa cha Adamu na Hawa, isipokuwa kwa wanaume kuna funzo moja kubwa...

Funzo hili ni namna ya kuishi nanyi kwa akili, na hivyo ndivyo Biblia ilivyotuagiza

(1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.)

Hilo ulilolibainisha la kusameheana nafikiri ni mjadala mwingine kabisa(labda kama sijaielewa hii mada), kwa sasa tujadili hili la kusukumiana mizigo badala ya kuwajibika kwa niaba.

mmh! wanaume nyie, nafikiri mleta mada hakukosea, mna explanation kwa kila kitu, hamkubali kushindwa. hilo la wanaume kutupenda, so soon nitalianzishia thread
 
mimi huomba msamaha haraka kwani, naamini silaha ya ndoa njema ni haya maneno matatu:-
1.POLE
2. SAMAHANI
3.ASANTE
Haya maneno ukiyatumia vizuri walah ndoa yako haitakuja kuyumba milele. maneno hayo yatumike kwa wote.
kuna wengine, hata ahsante hawasemi, inabidi kuwafundisha kusema thank you. sometimes huwa najiuliza ni malezi au ndio nature ya mfumo dume ipo kazini
 
Nakumbuka usia wa babu yangu.
"Mjukuu wangu daima kumbuka, ukitaka kuishi vyema na mwanamke daima kuwa mtu usietabirika"

Mara nyingi nikikosea navuta pumzi kidogo kisha baadae namuomba msamaha wa ubavu wangu pamoja na mahaba kibao.
Ila mara nyingine naharibu hali ya hewa halafu nakuwa nunda hadi anashangaa.
Basi mwenyewe utasikia anasema, "mume wangu ni mpole ila we usiombe ukute siku bange zake zipo kichwani"

Somo ni kuwa;
Ili kujenga mahusiano mema na wandani wetu wanaume tunatakiwa kuwatendea wema na kuwasiliana nao kwa upole ili kujenga mapenzi baina yetu, ila hatutakiwi kufikia mahali ikawa ni fomula.
Wanawake hupenda pia kuziona haiba na tabia fulani za kiume kwa waume zao zilizo katika mila na desturi za jamii zao. Mfano utukutu na ubabe fulani hivi ambao haujapitiliza.
Ukiwa laini sana hawajisikii raha, na ukiwa mbabe sana unawapotezea amani.

Amani kwenu

Na hili ndio JAWABU!!
 
yani ndugu yangu naona sasa wewe ndo walewale
wenye mfumo dume wanaopenda kunyenyekewa na
kulambwa miguu ikidhania kuwa wao huwaga wakosei

hebu jirekebishe ndugu kwani kama ukimkosea mkeo
yabidi umwombe msamaha kwani ni wewe ni sababu

Nitaomba msamaha iwapo umenifuma navunja amri ya sita tu na wala si vinginevyo.
 
Jnrs
akisoma tu hapojuu lazma akusamehe
 
huu ndio uanaume mkuu... Kila mwanaume na afahamu hili.

Nilitaka kuhighlight kitu nikajikuta nahighlight yote.. Niaacha. Safi sana kiongozi

kama kweli mkeo anaishi na wewe na kukulinganisha na wavuta bangi kuna tatizo
 
mmh! wanaume nyie, nafikiri mleta mada hakukosea, mna explanation kwa kila kitu, hamkubali kushindwa. hilo la wanaume kutupenda, so soon nitalianzishia thread

Hahaha!!! hapana bi dada wala hatuna maana hiyo...

Nitafurahi kuona hiyo thread yako na utakuwa umefanya vyema
 
kuna wengine, hata ahsante hawasemi, inabidi kuwafundisha kusema thank you. sometimes huwa najiuliza ni malezi au ndio nature ya mfumo dume ipo kazini
unajua dada venine kwa uzoefu wangu kunamakabira siyoyataja wao kuomba na kushukuru ni kujidharirisha kwa mwanamke, wao ndio wana haki,nahakika usipo yatii hayo ndoa yako ipo mashakani daima
 
Back
Top Bottom