Thamani ya Yanga ni Tsh. Bilioni 100, Simba ni Tsh. Bilioni 20

Thamani ya Yanga ni Tsh. Bilioni 100, Simba ni Tsh. Bilioni 20

Nimekutolea mifano ya kihistoria kuhusu uuzaji wa hisa ambayo inabatilisha hesabu yako. Mifano ile ndio inaweza kuwa termed kama mantiki na sio hizi speculations zako

Kwa hiyo, hoja yako ya “ceteris paribus” haifanyi kazi hapa.

Hisa si maharage ya kupimwa kwa mizani ya asilimia. Zinahitaji uchambuzi wa mazingira, historia, na thamani ya kimkakati. Kama huwezi kuonesha valuation rasmi ya Simba, basi hiyo hesabu ya 49% = 20B → 51% = 21B ni ya kufikirika.
Pointless.
 
Hivi wewe upo timamu kweli? ni lazima kuwe na channel maalumu ndio yaitwe maudhui? Zile footage za Yanga wakiwa mazoezini, Yanga day, activities zote zinazo rushwa na Azam media zinarushwa kwa mkataba gani?
Kwa kweli hoja yako ni ya kushangaza na inaonesha kiwango cha juu cha ujinga wa wazi katika kupambanua muktadha wa mkataba.

Unaposema “footage za Yanga Day na mazoezi zinarushwa na Azam Media” kama ushahidi wa utekelezaji wa mkataba wa Yanga TV, unajichanganya vibaya sana.

Kwanza tuweke sawa muktadha wa Mkataba ulivyo:
Mkataba wa Azam media na Yanga wa mwaka 2021 ulieleza kuwa
Yanga TV itakuwa channel maalum kwenye kisimbuzi cha Azam, ikirusha maudhui ya klabu pekee—mazoezi, vipindi vya mashabiki, maandalizi ya mechi n.k.
Mpaka leo hii tunavyobishana:
  • Hakuna channel ya Yanga TV inayotambulika kwenye kisimbuzi cha Azam.
  • Hakuna namba ya channel wala ratiba ya maudhui ya Yanga pekee.
  • Hakuna ushahidi wa maudhui ya kipekee yanayorushwa kwa mujibu wa mkataba huo.
Kwa hiyo, footage unazozitaja si sehemu ya utekelezaji wa mkataba wa Yanga TV, bali ni sehemu ya matangazo ya kawaida ya ligi.

1. Swali ni Je, unataka kusema kabla ya mkataba wa Yanga TV, Azam walikuwa wanarusha footage za Yanga bure bila mkataba wala malipo?
Ikiwa footage hizo zilikuwepo kabla ya mkataba, basi mkataba haukuleta kitu kipya.

2. Je, footage za mazoezi za klabu zingine hazioneshwi kwenye Azam TV?
Kama zinaoneshwa, kwa nini unataka kuhalalisha footage za Yanga kama za kipekee kupitia mkataba ambao unapingana na utekelezaji wa makubaliano ya kimkataba yaliyoainisha kuwepo kwa Yanga Tv?
 
Pointless.
Ulikaririshwa wapi kuwa 49% zilizouzwa 20B maana yake value ya 51% ni 21B?

Hii ni hesabu ya wapi Sheikh wangu? Unaweza kutufafanulia hizi namba umezipataje?
 
Ulikaririshwa wapi kuwa 49% zilizouzwa 20B maana yake value ya 51% ni 21B?

Hii ni hesabu ya wapi Sheikh wangu? Unaweza kutufafanulia hizi namba umezipataje?
Leo ukiambiwa 1 share ya CRDB (ambayo labda ni 1/3billion in ownership) inauzwa kwa shs 1500.
Je, shares 3, siku hiyohiyo zitauzwa shs ngapi? Na zitakuwa sawa na umiliki wa kiasi gani?
Hebu jibu kwanza hilo.
 
Kabla hatujafika huko, nataka kwanza huo mfano wako wa CRDB uwe una reflect muktadha wa mchakato wa hisa uliotumika Simba.

Simba haijawahi kuorodhesha hisa zake sokoni, wala kuweka valuation ya wazi ya kampuni. Kwa hiyo, kabla hatujaenda mbali

Thibitisha kwanza​

  • Ni lini Simba waliweka valuation rasmi ya kampuni?
  • Ni taasisi gani ya kifedha ilifanya tathmini ya thamani ya klabu?
  • Ni wapi hisa za Simba ziliwekwa sokoni kwa bei ya wazi kama CRDB?

Bila majibu ya maswali haya, huo mfano wako wa CRDB hauwezi kutumika kama kigezo cha kuhalalisha bei ya hisa za Simba, kwa sababu muktadha ni tofauti kabisa.
 
Usichoelewa ni kwamba ukishaweka IPO (Initial Public Offer) na kuuza kwa mara ya kwanza kabisa, hiyo bei ni market value (Bei unayothani soko litainunua) siyo Book value (yaani thamani ya mali minus thamani ya madeni/liabilities).
Sasa kwa kuwa simba hawajawahi kuorodhesha hisa zao, yaani kutoa IPO Dar stock exchange, basi hizo 20B zilizotolewa na Dewji ili kununua 49% ni book value, siyo market value, kama ni market value according to Dewji, basi hiyo siyo offical market value.
Book value inaweza pia kutumika kujua thamani ya kampuni kwa sababu book value ni assets -liabilities.
Ndiyo maana nikakwambia kama 20B ni 49% basi 41B ni 100% based on book value.
 
Ila unapendaga sana ligi za kitoto
Katika yooote hayo niliyoyaandika tangu page ya kwanza, ulichoweza kun"gamua ni ligi ya kitoto?

Hujaona ubishani wenye hoja zenye mantiki kwa wanaodai thamani ya Yanga ina worth bilioni 100?

Hujaona challenge niliyoitoa kwa wanaosema thamani ya bilioni 100 ni kutokana na Jengo la Yanga ambalo lipo Jangwani eneo lenye changamoto za kijiografia kwenye kukumbwa na mafuriko?

Hujaona hoja hiyo kuwa sio ligi ya kitoto bali ni hoja ya kuonesha namna thamani ya eneo hilo inavyoweza kuathiriwa kaulingana na hali ya kijiografia ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara?

Hujaona kabisa mantiki ya hoja zangu kupitia mifano ya Club ambayo ni benchmark (Al Ahly) kwenye uwanda wa soka la Afrika, yenye mafanikio makubwa kuliko Club nyingine, yenye uwekezaji mkubwa wa kimikataba kuliko Club nyingine, yenye fanbase kubwa, yenye kumiliki asset nyingi na zenye thamani.

Halafu Club hiyo kuzidiwa thamani na Yanga kwa hoja ya asset ambazo ni Jangwani na hekari 7 za Kigamboni, huoni hoja hii kuwa na mashiko badala yake unaona anayejibu hivi kupinga madai ya Yanga kuwa na thamani ya bilioni 100 analeta ligi za kitoto

Hujaona mantiki ya hoja zangu kwanini swala la Yanga Tv ni scam? Au pengine wewe unaweza ukawa na majibu yenye uthibitisho kutuoneshea ni Channel namba ngapi kwenye kisimbuzi cha Azam kuna Yanga TV?

Au kwakua na wewe ni miongoni mwa mashabiki wa Yanga hivyo inakufanya by default unaingia kwenye mkumbo wa kukubali kila kitu ambacho Club yako inafanya au kudai imefanya?
 
Nikushauri kitu, punguza kukaa vijiweni yaani channel umeona ni big deal sana? Azam wameweza kufungua channel ya vichekesho washindwe Yanga TV?
Kijiweni siwezi kuacha kukaa, huko ndio maskani yangu.

Yes lazima nione kama big deal kwasababu Yanga ni taasisi otherwise utakuwa unafanya makosa kuniambia nisikae kijiweni halafu timu yako inaendeshwa kwa falsafa za kijiweni.

Taasisi haiwezi kufanya blundering na kutotoa sababu za msingi kuelezea kwa mashabiki zake kwanini hilo dili halijawezekana.

Taasisi kukaa kimya ni kutuma meseji kwa mashabiki wake kuwa imewadharau na nyie hamna mandate ya kimaamuzi wala hamna guts za kuwaajibisha viongozi wenu that's why wanakuwa huru kuingia madili hewa.

Ni simple tu, Azam wamefungua channel ya vichekesho kwasbabu lilikuwa ni dili la ukweli haikuwa blunder kama Yanga TV. Hili nalo linahitaji argument?
 
Usichoelewa ni kwamba ukishaweka IPO (Initial Public Offer) na kuuza kwa mara ya kwanza kabisa, hiyo bei ni market value (Bei unayothani soko litainunua) siyo Book value (yaani thamani ya mali minus thamani ya madeni/liabilities).
Sasa kwa kuwa simba hawajawahi kuorodhesha hisa zao, yaani kutoa IPO Dar stock exchange, basi hizo 20B zilizotolewa na Dewji ili kununua 49% ni book value, siyo market value, kama ni market value according to Dewji, basi hiyo siyo offical market value.
Book value inaweza pia kutumika kujua thamani ya kampuni kwa sababu book value ni assets -liabilities.
Ndiyo maana nikakwambia kama 20B ni 49% basi 41B ni 100% based on book value.
Kuna maelezo naweza kukubaliana na wewe, na kuna maelezo nitapingana na wewe kwasababu hayana ukweli au uhalisia.

Ukweli uliopo kwenye hoja yako.

Ni ukweli kuwa IPO huweka market value ya awali, na ni ukweli kuwa Simba haikutoa IPO, Na ni ukweli kuwa Book value ni assets - Liabilities

Hoja zisizo na ukweli hapa

Kudhani kwamba kwasababu hakuna IPO basi 20B ni book value.
Kutokuwepo kwa IPO haimaanishi moja kwa moja kuwa thamani ya hisa iliyolipwa ni book value. Inawezekana kabisa ilikuwa ni negotiated value kulingana na matarajio ya biashara, mikakati ya klabu, ukaribu wa familia yake kuisapoti timu, mapenzi yake kwa timu nk . Kwa hiyo, kusema ni book value tu bila ushahidi wa vitabu vya hesabu ni speculation.
 
Okay ili kupunguza ubishi usio na maana, tuseme ni negotiated value.
But it's a "value" right?
Sasa imagine hiyo value ni sawa na 109B today, so what is the fuss?
 
Kijiweni siwezi kuacha kukaa, huko ndio maskani yangu.

Yes lazima nione kama big deal kwasababu Yanga ni taasisi otherwise utakuwa unafanya makosa kuniambia nisikae kijiweni halafu timu yako inaendeshwa kwa falsafa za kijiweni.

Taasisi haiwezi kufanya blundering na kutotoa sababu za msingi kuelezea kwa mashabiki zake kwanini hilo dili halijawezekana.

Taasisi kukaa kimya ni kutuma meseji kwa mashabiki wake kuwa imewadharau na nyie hamna mandate ya kimaamuzi wala hamna guts za kuwaajibisha viongozi wenu that's why wanakuwa huru kuingia madili hewa.

Ni simple tu, Azam wamefungua channel ya vichekesho kwasbabu lilikuwa ni dili la ukweli haikuwa blunder kama Yanga TV. Hili nalo linahitaji argument?
👍
 
Back
Top Bottom