Thamani ya Yanga ni Tsh. Bilioni 100, Simba ni Tsh. Bilioni 20

We ni mfano hai wa kile kinachoitwa “ujinga unaojivunia”

Aina ya ujinga ambao si tu hauna aibu, bali unajitangaza kwa kelele kama vile ni ushindi wa Nobel.

Na kwa bahati mbaya, nyuzi kama zako huwenda ndizo zilikuwa zikitawala timeline ya JamiiForums TCRA walipoamua kufungua ukurasa mmoja, wakakutana na bandiko lako, wakaulizana: “Hivi kweli hawa ni great thinkers?” Kisha wakaifungia jukwaa lote kwa kosa la mtu mmoja asiyejua tofauti ya club value na squad value.
Kama una biashara ambayo cycle yake kwa mwaka ni million 20 kwa mwaka,ukitaka kumu uzia mtu utauza sh ngapi?
 
Kuwa specific, biashara ni jambo lenye wigo mpana usisite kuweka maelezo ya kutosha ili ueleweke.

Mzunguko wa mapato (revenue cycle) sio kipimo cha moja kwa moja cha kuonesha thamani ya biashara. Thamani ya biashara huamuliwa kwa kuzingatia mambo mengi.

Kuna changamoto zinazoweza kuua thamani ya biashara. Mfano ni biashara yenye migogoro ya umiliki wanafamilia wanazungukana kuuza mali za urithi au biashara ina kesi mahakamani, wanunuzi huingia hofu kununua biashara hiyo.

Ni sawa na changamoto ya kijografia iliyopo hapo Jangwani ina influence kubwa ya kuwakimbiza wanunuzi au wawekezaji eneo hilo.

Ebu tuijadili kwa undani kidogo hiyo biashara kwa ku outline makadirio ya mapato na gharama zilizotumika.

Tuseme biashara ina mzunguko wa mapato ya Tsh milioni 20 kwa mwaka. Hii ni sawa na:
  • Milioni 1.67 kwa mwezi
  • Takriban Tsh 55,000 kwa siku
Sasa tuangalie upande wa uwekezaji:
Tuseme biashara hiyo imeanzishwa kwa mtaji wa Tsh milioni 60 (gharama za vifaa, kodi, leseni, bidhaa, wafanyakazi, n.k.).

Tujadili Faida halisi inayopatikana
Tuseme faida halisi baada ya gharama zote ni milioni 2 kwa mwaka (sio mzunguko wa mapato, bali faida halisi). Hii ni:
  • Milioni 0.17 kwa mwezi
  • Tsh 5,500 kwa siku
Kwa maana hiyo hapo kutakuwa na changamoto kadhaa
1. Kwa faida ya milioni 2 kwa mwaka itachukua miaka 30 kurudisha mtaji wa milioni 60
2. Gharama za uendeshaji zinaweza kupanda (umeme, kodi, mishahara nk)
Biashara inaweza kukumbwa na majanga kama mafuriko ikiwa haikufanywi kwenye eneo lenye miundombinu mizuri au changamoto ya kushuka thamani kwa bidhaa.

Kwa hiyo thamani ya biashara ni dhana pana inayohitaji uchambuzi wa kina wa faida, mali, madeni, hatari na tathmini ya fursa ya ukuaji.
 
Huyo ana ubongo wa bata 🦆 hawezi kuelewa
Eti tuna hekari 7 hiyo ni asset. We unazijua aseti?

Viongozi wenu wamewaaminisha kuwa huyo wa juu mmemzidi kwenye thamani na nyie mlivyo mapimbi mmejaa

1757374251042.png
 
Sasa una ujuaje uongo kama haujui ukweli
Kujua uongo hakuhitaji kujua ukweli wote, bali kunahitaji uwezo wa kugundua mgongano kati ya madai na uhalisia.(Contradiction between assertions and reality)

Uongo mara nyingi hujifichua kwa kupingana na mantiki, takwimu, au mazingira halisi.

Hii ndiyo sababu hata bila kujua thamani sahihi ya klabu ya Yanga, mtu anaweza kusema kwa uhakika kuwa madai ya bilioni 100 ni ya kupotosha.
 
Hiyo Club value inapimwa kwa vigezo gani?

Value ya Club ni asset au kitu gani? Halafu tuje kujadili, Je ni kweli asset za Yanga zina thamani sana kuizidi Al Ahly na Mamelody

Tupe evaluation iliyofanyia hadi kufikia conclusion ya bilion 100
Mkuu umesoma Fedha

Kuna kitu kinaitwa Present Value,Market Value , Real Value,Future Value

Mfano Umenunua Gari milioni 40 leo,Hii ni Current Value lakini leo hii unaweza uliza bei la gari hilo hilo unataka kuliuza ukaambiwa Market Value au Bei ya soko ni milioni 30 kumbuka hiyo ni siku moja umelitoa Yard na umeuliza bei mita kadhaa nje ya Yard

Yanga wanaongelea kama watataka kuuza share ,Narudia kama watataka kuuza share wanaongele Future yaani Future Value

Future Value ya yanga watakapoanza kuuza shares ni 100 bilulions lakini ukitaka kupata thamani leo wakiwa hawajaanza kuuza share unafanya Discounting

Discounting ni nini? Ni kitendo cha kuirudisha thamani ya kitu kwa bei ya sasa yaani Je nikikupa milion 20 leo kwa ajili ya nyumba yako ,miaka mitano ijayo itakuwa na thamani gani hiyo milion 20

Sasa Bilion 100 za ya yanga kimehesabu kuna mambo ya kuzingatia

1.Uimara wa shilingi yetu( Strengh of our currency)

2.Mfumuko wa bei (Inflation)

3.Discounting rate au rate of return ,Hii inapatikana kwenye masoko ya hisa na masoko ya Bonds zipo
 
Kuwa specific, biashara ni jambo lenye wigo mpana usisite kuweka maelezo ya kutosha ili ueleweke.

Mzunguko wa mapato (revenue cycle) sio kipimo cha moja kwa moja cha kuonesha thamani ya biashara. Thamani ya biashara huamuliwa kwa kuzingatia mambo mengi.

Kuna changamoto zinazoweza kuua thamani ya biashara. Mfano ni biashara yenye migogoro ya umiliki wanafamilia wanazungukana kuuza mali za urithi au biashara ina kesi mahakamani, wanunuzi huingia hofu kununua biashara hiyo.

Ni sawa na changamoto ya kijografia iliyopo hapo Jangwani ina influence kubwa ya kuwakimbiza wanunuzi au wawekezaji eneo hilo.

Ebu tuijadili kwa undani kidogo hiyo biashara kwa ku outline makadirio ya mapato na gharama zilizotumika.

Tuseme biashara ina mzunguko wa mapato ya Tsh milioni 20 kwa mwaka. Hii ni sawa na:
  • Milioni 1.67 kwa mwezi
  • Takriban Tsh 55,000 kwa siku
Sasa tuangalie upande wa uwekezaji:
Tuseme biashara hiyo imeanzishwa kwa mtaji wa Tsh milioni 60 (gharama za vifaa, kodi, leseni, bidhaa, wafanyakazi, n.k.).

Tujadili Faida halisi inayopatikana
Tuseme faida halisi baada ya gharama zote ni milioni 2 kwa mwaka (sio mzunguko wa mapato, bali faida halisi). Hii ni:
  • Milioni 0.17 kwa mwezi
  • Tsh 5,500 kwa siku
Kwa maana hiyo hapo kutakuwa na changamoto kadhaa
1. Kwa faida ya milioni 2 kwa mwaka itachukua miaka 30 kurudisha mtaji wa milioni 60
2. Gharama za uendeshaji zinaweza kupanda (umeme, kodi, mishahara nk)
Biashara inaweza kukumbwa na majanga kama mafuriko ikiwa haikufanywi kwenye eneo lenye miundombinu mizuri au changamoto ya kushuka thamani kwa bidhaa.

Kwa hiyo thamani ya biashara ni dhana pana inayohitaji uchambuzi wa kina wa faida, mali, madeni, hatari na tathmini ya fursa ya ukuaji.
Una maneno mengi ambayo haya make sense, labda nikupe mfano Yanga wali ingia mkataba wa billion 41 na Azam media kwenye issue ya TV rights, sasa kama Azam wametoa hio pesa sio kwamba wali nunua hisa no! ni TV rights tu hio club ina thamani kiasi gani? nyie mlivyo pigwa na Mhindi mnataka kila mtu apigwe kizembe
 
Eti tuna hekari 7 hiyo ni asset. We unazijua aseti?

Viongozi wenu wamewaaminisha kuwa huyo wa juu mmemzidi kwenye thamani na nyie mlivyo mapimbi mmejaa

View attachment 3468088
😂😂 Dah na hyo ya chini Msimu wa masika hapatamaniki kama dampo....aisee jamaa sijui anawachukuliaje mpk anawadhihaki kwa kuwaita Wala mihogo😂
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Kujua uongo hakuhitaji kujua ukweli wote, bali kunahitaji uwezo wa kugundua mgongano kati ya madai na uhalisia.(Contradiction between assertions and reality)

Uongo mara nyingi hujifichua kwa kupingana na mantiki, takwimu, au mazingira halisi.

Hii ndiyo sababu hata bila kujua thamani sahihi ya klabu ya Yanga, mtu anaweza kusema kwa uhakika kuwa madai ya bilioni 100 ni ya kupotosha.
Unatumia nguvu sana ku-argue mambo ya kipuuzi.
Simba ilikuwa na thamani ya 41 billion mwaka 2017.
Mwaka 2017 simba ilikuwa na mikataba ya kifedha isiyozidi 1bn.
Ilikuwa haiuzi merchandise katika mfumo unaoeleweka.
Ilikuwa na kikosi cha mostly 1bn.
Jengo lao la msimbazi na assets nyingine wala hazikufikia 2bn.
But ilikuwa na thamani ya 41bn (2017). Tuseme serikali ingeichukua Simba kwa kuwanunua wanachama na mwekezaji na kuiweka hiyo 41bn kwenye soko la fedha kama utt-amis leo ingekuwa na shilingi ngapi? Hiyohiyo Simba ya matambala mabovu aliyoinunua Dewji ilikuwa haina chochote cha maana, leo ingekuwa na shilingi ngapi kama 2017 ilikuwa na 41bn.
JIBU: 109 bn.
 
Mkuu umesoma Fedha

Kuna kitu kinaitwa Present Value,Market Value , Real Value,Future Value

Mfano Umenunua Gari milioni 40 leo,Hii ni Current Value lakini leo hii unaweza uliza bei la gari hilo hilo unataka kuliuza ukaambiwa Market Value au Bei ya soko ni milioni 30 kumbuka hiyo ni siku moja umelitoa Yard na umeuliza bei mita kadhaa nje ya Yard

Yanga wanaongelea kama watataka kuuza share ,Narudia kama watataka kuuza share wanaongele Future yaani Future Value

Future Value ya yanga watakapoanza kuuza shares ni 100 bilulions lakini ukitaka kupata thamani leo wakiwa hawajaanza kuuza share unafanya Discounting

Discounting ni nini? Ni kitendo cha kuirudisha thamani ya kitu kwa bei ya sasa yaani Je nikikupa milion 20 leo kwa ajili ya nyumba yako ,miaka mitano ijayo itakuwa na thamani gani hiyo milion 20

Sasa Bilion 100 za ya yanga kimehesabu kuna mambo ya kuzingatia

1.Uimara wa shilingi yetu( Strengh of our currency)

2.Mfumuko wa bei (Inflation)

3.Discounting rate au rate of return ,Hii inapatikana kwenye masoko ya hisa na masoko ya Bonds zipo
Makadirio ya Future Value yamepitia tathmini gani ya kimahesabu?
  • Je, ni nani aliyefanya valuation hiyo ya bilioni 100?
  • Imetumia model gani ya kifedha—DCF (Discounted Cash Flow), comparables, au asset-based valuation?
  • Iwapo hakuna ripoti rasmi ya tathmini, hiyo bilioni 100 ni namba ya kufikirika tu.

Thamani ya sasa ya Yanga ni kiasi gani?

Ili kuhesabu Future Value, lazima ujue Present Value kwanza. Je, Yanga kwa sasa ina thamani ya kiasi gani kwa kutumia vigezo vya:
  1. Mapato ya mwaka
  2. Mali halisi (assets)
  3. Faida halisi (net profit)
  4. Brand equity
Halafu Future Value ni lini hasa?
Madai yako ya future value hujayawekea time frame maalumu, ni mwaka gani? miaka mitano, kumi? au hamsini? Hujaweka bayana umesema tu future value, hata mwaka ujao ni future.

So tunaweza kuwa tunabishana hapa kumbe future value ambayo uliikusudia ni miaka 100

Ni asset gani haswa ambazo zinatumika ku determine hesabu ya future value?
 
Una maneno mengi ambayo haya make sense, labda nikupe mfano Yanga wali ingia mkataba wa billion 41 na Azam media kwenye issue ya TV rights, sasa kama Azam wametoa hio pesa sio kwamba wali nunua hisa no! ni TV rights tu hio club ina thamani kiasi gani? nyie mlivyo pigwa na Mhindi mnataka kila mtu apigwe kizembe
Kwanza, mkataba huo wa bilioni 41.64 (ambayo Yanga hupokea bilioni 34.8 baada ya VAT) ulielezwa kuwa ni wa Yanga TV—channel maalum ndani ya kisimbuzi cha Azam Media inayorusha maudhui ya Yanga pekee.

Swali la msingi hapa

Je, unaweza kutaja channel namba ya Yanga TV kwenye kisimbuzi cha Azam? Ikiwa haipo, basi mkataba huo unakuwa ni muendelezo wa porojo za viongozi wako kuendelea kuwadanganya mashabiki wake so basically hauwezi kutumia hiyo taarifa kama kipimo cha Club valuation.

​

😂😂 Dah na hyo ya chini Msimu wa masika hapatamaniki kama dampo....aisee jamaa sijui anawachukuliaje mpk anawadhihaki kwa kuwaita Wala mihogo😂
Hawa majamaa ni wajinga sana nashangaa sijui kwanini hawastuki licha ya jitihada zote hizi nazotumia kuwafumbua macho.

Yaani wakati nawazindua fikra kwa kuonesha jinsi wanavyodanganywa na viongozi wao anakuja mmoja wao anasema sababu ya Yanga kustahili thamani ya bilion 100 ni kutokana na mkataba wa TV rights ambayo Yanga waliingia na Azam kuwa na Yanga TV kwenye kisimbuzi cha Azam.

Yaani anakuja kutetea uongo wa sasa (bilion 100) kwa kutumia uongo wa zamani (Yanga TV)

Huyu member bado anaamini kuna channel ya Yanga TV ina run kwenye kisimbuzi cha Azam.
 
Unatumia nguvu sana ku-argue mambo ya kipuuzi.
Simba ilikuwa na thamani ya 41 billion mwaka 2017.
Mwaka 2017 simba ilikuwa na mikataba ya kifedha isiyozidi 1bn.
Ilikuwa haiuzi merchandise katika mfumo unaoeleweka.
Ilikuwa na kikosi cha mostly 1bn.
Jengo lao la msimbazi na assets nyingine wala hazikufikia 2bn.
But ilikuwa na thamani ya 41bn (2017). Tuseme serikali ingeichukua Simba kwa kuwanunua wanachama na mwekezaji na kuiweka hiyo 41bn kwenye soko la fedha kama utt-amis leo ingekuwa na shilingi ngapi? Hiyohiyo Simba ya matambala mabovu aliyoinunua Dewji ilikuwa haina chochote cha maana, leo ingekuwa na shilingi ngapi kama 2017 ilikuwa na 41bn.
JIBU: 109 bn.
Nipe hizo data zinazoonesha Simba ilikuwa na thamani ya 41bilion mwaka 2017
 
Kwanza, mkataba huo wa bilioni 41.64 (ambayo Yanga hupokea bilioni 34.8 baada ya VAT) ulielezwa kuwa ni wa Yanga TV—channel maalum ndani ya kisimbuzi cha Azam Media inayorusha maudhui ya Yanga pekee.

Swali la msingi hapa

Je, unaweza kutaja channel namba ya Yanga TV kwenye kisimbuzi cha Azam? Ikiwa haipo, basi mkataba huo unakuwa ni muendelezo wa porojo za viongozi wako kuendelea kuwadanganya mashabiki wake so basically hauwezi kutumia hiyo taarifa kama kipimo cha Club valuation.

​

Wewe akili yako ni fupi sana TV rights ni channel?
 
Unatumia nguvu sana ku-argue mambo ya kipuuzi.
Simba ilikuwa na thamani ya 41 billion mwaka 2017.
Mwaka 2017 simba ilikuwa na mikataba ya kifedha isiyozidi 1bn.
Ilikuwa haiuzi merchandise katika mfumo unaoeleweka.
Ilikuwa na kikosi cha mostly 1bn.
Jengo lao la msimbazi na assets nyingine wala hazikufikia 2bn.
But ilikuwa na thamani ya 41bn (2017). Tuseme serikali ingeichukua Simba kwa kuwanunua wanachama na mwekezaji na kuiweka hiyo 41bn kwenye soko la fedha kama utt-amis leo ingekuwa na shilingi ngapi? Hiyohiyo Simba ya matambala mabovu aliyoinunua Dewji ilikuwa haina chochote cha maana, leo ingekuwa na shilingi ngapi kama 2017 ilikuwa na 41bn.
JIBU: 109 bn.
Huyo Muha ni mbishi hata uongee nini
 
Back
Top Bottom