Kipi hujaelewa hapo na source nimekuwekea au hujaona?
Zingatia sana maneno yaliyo bolded, italic na yaliyopo kwenye brackets
Ngoja nikuwekee kwa mtindo huu labda pengine utaelewa vizuri zaidi:
Klabu ya Yanga imeingia Mkataba wa miaka 10 na Azam Media wa haki za matangazo za Klabu kupitia Yanga TV wenye thamani ya Bilioni 41.64 pamoja na VAT lakini yanga itapokea kiasi cha Bilioni 34.8 za kitanzania.
www.eatv.tv
Hiyo link hapo juu ni taarifa rasmi ya mkataba unaosema Yanga waliingia mkataba wa miaka 10 na Azam Media kwa ajili ya
Yanga TV, wenye thamani ya Tsh bilioni 41.64 (pamoja na VAT), lakini Yanga itapokea Tsh bilioni 34.8.
Mpaka hapa tunakubaliana bila shaka kuwa mpaka hatua hii wote tunaelewana.
Sasa, mkataba huu ulieleza wazi kuwa Yanga TV ingekuwa na channel maalum kwenye kisimbuzi cha Azam, ikirusha maudhui ya klabu ikiwemo mazoezi, maandalizi ya mechi, vipindi vya mashabiki n.k. Hiyo ndiyo maana ya “TV rights” katika muktadha wa mkataba huu. (Hapa sijui kama tunaelewana)
Lakini mpaka leo hii:
- Hakuna channel ya Yanga TV kwenye kisimbuzi cha Azam. (Hapa tunaelewana)
- Hakuna namba ya channel inayotambulika. (hapa pia tunaelewana)
- Hakuna maudhui yanayoonekana kama ilivyoahidiwa. (Hapa napo tunaelewana)
Kwa hiyo,
project haipo, na kwa mantiki hiyo,
mkataba haujatekelezwa kama ulivyotangazwa. (Hapa sijui kama utakubali kuelewa japo panaeleweka)
Sasa wewe umedai kuwa Yanga inalipwa na Azam Media bila kuwepo kwa hiyo Yanga TV. Ni kweli Yanga inalipwa, lakini swali ni:
Je, inalipwa kupitia mkataba gani?
- Ni huu wa Yanga TV ambao haujatekelezwa?
- Au ni kupitia haki za matangazo ambazo Azam Media hulipa kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kupitia Bodi ya Ligi?
Ikiwa ni mkataba wa pili, basi hiyo siyo
exclusive TV rights ya Yanga, bali ni mgao wa kawaida wa klabu zote. Na kama ni mkataba wa kwanza, basi
tuonyeshe hiyo channel iko wapi—vinginevyo, tunajadili nadharia ya kufikirika.
Kwa hiyo, kabla ya kusema Yanga anaingiza bilioni 41 kwa TV rights,
thibitisha kwanza kuwa hiyo project ipo active. Vinginevyo, ni sawa na kupewa picha ya samaki wakati una njaa—hauwezi kula picha, wala haikusaidii.